Zanzibar balaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar balaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, May 29, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2][/h]


  Na Mwinyi Sadallah  29th May 2012
  [​IMG] Makanisa mawili, nyumba ya mtawa vyachomwa
  [​IMG] Chuo cha Mwalimu Nyerere nacho chashambuliwa  [​IMG]
  Tairi la gari likiwa limechomwa moto kwenye barabara itokayo Mikunguni kuelekea Amani katika vurugu zilizoendelea jana katika mji wa Zanzibar na vitongoji vyake.


  Wakati viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani wakikutana na viongozi wa dini Zanzibar, vitendo vya hujuma ikiwemo uchomaji wa makanisa na miundombinu ya taasisi vimeendelea na Jeshi la Polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu.

  Vurugu za wafuasi wa uamsho zilizoanza Jumamosi na kuendelea hadi Jumapili, ziliendelea tena Jumapili usiku hadi jana mchana, huku makanisa mawili yakichomwa moto, nyumba ya watawa pamoja na nyumba ya walinzi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Bububu, Mkoa wa Mjini Magharibi nayo yakichomwa.

  Makanisa yaliyochomwa moto ni Kanisa Katoliki la Mtakatifu Mikael lililoko eneo la Mpendae ambalo lilichomwa saa nane mchana baada ya kikundi cha watu wasiopungua 20 waliokuwa na silaha za jadi kulivamia na kuchoma mabenchi ya waumini kwa kutumia matairi ya gari yaliyomwagiwa petroli.

  Padri wa kanisa hilo, Ambrose Mkenda, alisema watu hao waliwatishia walinzi na baada ya kukimbia waliingia ndani ya kanisa na kuanza kufanya vitendo vya hujuma, na kuchoma mali zilizokuwemo ndani vikiwemo vinanda.

  Alisema pia Kanisa Katoliki lililopo Tomondo lilichomwa moto juzi sasa sita usiku.

  “Kabla ya matukio hayo, tuliomba kupatiwa ulinzi kutoka kituo cha Polisi Madema, tukaambiwa suala letu linashughulikiwa, lakini hadi sasa hatujajua limefikia hatua gani,” alisema Padri Mkenda.

  Watu hao pia wanadaiwa kuchoma moto nyumba inayotumiwa na watawa katika mtaa wa Welezo saa 5:30 usiku, tukio ambalo lilienda sambamba na uchomaji moto wa nyumba ya walinzi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere huko Bububu Kisiwani.

  Vurugu hizo zilisababisha kufungwa kwa barabara na kuathiri usafiri katika mtaa wa Daraja Bovu, Amani, Mwanakwerekwe ambapo wafuasi wa Uamsho walichoma moto matairi ya gari na kubeba vyuma vizito na kuvitupa katikati ya barabara pamoja na magogo ya minazi na mawe.

  Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi lililazimika kupeleka magari manane na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU). Magari hayo ni Land Rover zenye namba PT 4007, PT 2089, PT 2086 na PT 2080 pamoja na gari la kikosi cha Valantia KVZ lenye namba KVZ 109 na kuwatawanya wafuasi wa Uamsho.

  Kitendo cha kufunga njia kiliathiri mfumo mzima wa usafiri hasa kwa wanafunzi, walimu, wafanyabiashara na wakazi wa maeneo husika huku baadhi walionekana wakibubujikwa machozi kutokana na moshi wa mabomu ukichanganyika na moshi wa matairi yaliokuwa yakichomwa moto.

  Askari hao walionekana wakiwasaidia walimu hao njia za kupita ili kuepuka kupigwa mawe na wafuasi wa Uamsho waliokuwa wakijikusanya na kuimba nyimbo za kuupinga Muungano pamoja na kuwakejeli askari hao.

  WAZIRI NCHIMBI, MWEMA WATUA ZANZIBAR


  Jana saa tano za asubuhi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emanuel Nchimbi, akiwa amefuatana na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Said Mwema, walikutana na viongozi wa kidini wakiwemo wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (Jumaza), wadau wa sekta ya utalii na waandishi wa habari katika makao makuu ya Jeshi hilo.

  Viongozi hao walizungumzia mustakabali mzima wa kurejesha hali ya amani na utulivu huku Waziri Nchimbi akisema kwamba jambo la msingi ni umuhimu wa viongozi wa kidini kusoma sheria ambazo zimewekwa kwa ajili ya kuwalinda wananchi.

  Alisema Jeshi la Polisi halitakubali vitendo vya uvunjifu wa amani.

  Aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi litaendelea kulinda Katiba na sheria na hakuna mwananchi yeyote atakayekuwa juu ya sheria na kuwataka kujiepusha na vitendo vya vurugu.

  Alisema vitendo vya kuchoma makanisa moto na uvunjaji wa haki za msingi za kikatiba za wananchi ni kinyume cha sheria kwa vile ibara ya 19 ya Katiba ya Zanzibar inatoa haki kwa kila mwananchi kuwa na imani yake ya dini na uhuru wa kuabudu.

  “Mimi naamini kuwa dini ya Kiislamu hairuhusu unywaji wa pombe, lakini kuna watu waliotumia fursa ya vurugu hizo kuvamia baa, wakafanya uharibifu, wakachoma moto na wakachukua pombe na kuanza kunywa, sasa hao kweli ni waumini wa dini ya Kiislamu au wafuasi wa Uamsho?” alihoji Waziri Nchimbi na kuongeza:

  “Tusikubali wahalifu kutumia dini kufanya vitendo vya uhalifu, wajibu wetu sote ni kushirikiana na vyombo vya dola kudumisha amani na utulivu.”

  IGP Said Mwema alisema kutokana na mazingira yaliyopo Zanzibar hivi sasa, amelazimika kuendelea kuwepo visiwani hapa ili kutayarisha mpango kazi utakaosaidia kumaliza vitendo vya vurugu na uvunjaji wa sheria.

  Mwema alisema kwamba atakutana na viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali kwa lengo la kupanga mpango kazi huo utakaosaidia kurejesha hali ya amani na utulivu.

  Mwema aliongeza kuwa Jeshi la polisi limefarijika na kitendo cha Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, kwa kutoa tamko la kuwataka wananchi wa Zanzibar wakiwemo wafuasi wa Uamsho kuachana na vitendo vya vurugu, hatua ambayo imefungua njia ya kupata mafanikio katika kurejesha utulivu.

  UAMSHO WAKANA

  Wakati huo huo, kikundi cha Uamsho kimeibuka na kutoa tamko kuwa hakihusiki na vurugu zinazoendelea.

  Taarifa ya Uamsho imeeleza kuwa haihusiki na vitendo vyote vya uvunjifu wa amani vilivyotokea usiku wa kuamkia Mei 26, 2012.

  “Jumuiya inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini za imani tofauti. Kufanya hivo ni kwenda kinyume na (cha) mafundisho ya dini ya Kiislamu,” ilieleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu wa Jumuiya hiyo, Abdallah Said Ali.

  SMZ YAPIGA MARUFUKU

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imepiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote ikiwemo mihadhara ya aina mbalimbali ambayo haina kibali cha Serikali.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alisema mbali na kupiga marufuku mihadhara, pia serikali inawataka wananchi kuheshimu sheria.

  Waziri Aboud alisema serikali imeliagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na vurugu hizo katika mji wa Zanzibar.

  “Serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa mali zilizofanywa katika taasisi za umma, dini na watu binafsi,” alisisitiza Waziri Aboud.

  Katika taarifa hiyo, serikali imewapa pole wale wote walioathirika na vurugu hizo na imeahidi kuchukua hatua kali
  dhidi ya waliohusika kufanya vurugu hizo.

  TAG, KATOLIKI WALAANI MACHAFUKO Z’BAR

  Viongozi wa makanisa ya Tanzania Assemblies of God (TAG) na Katoliki nchini, wamelaani vikali vurugu zilizotokea Zanzibar zilizofanywa na wafuasi wa Uamsho) juzi.

  Vurugu hizo zilisababisha makanisa matatu kuchomwa moto hadi jana na mali nyingine kuharibiwa, likiwamo gari la Askofu wa Kanisa la TAG, Dickson Kaganga.

  Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabas Mtokambali, aliwataka viongozi wa serikali kusimamia sheria na haki na kudhibiti kauli na vitendo vitakavyowafanya baadhi ya Watanzania kudhani kuwa hawatendewi haki.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Anthon Makunde, aliwataka Watanzania kufahamu kuwa suala la amani ya nchi, siyo la viongozi peke yake, bali ni la Watanzaia wote.

  “Kila Mtanzania ana dhamana…dhamana ya kufanya hapa pakalike…kila Mtanzania atambue kuwa tukio la Zanzibar linamhusu…si suala la viongozi wa taifa peke yake,” alisema Padri Makunde.

  MUFTI SIMBA: NI MAMBO YA KISIASA, SIYO DINI

  Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba, amesema kilichotokea Zanzibar ni mambo ya kisiasa kwani kuwapo au kutokuwapo kwa Muungano hakuna msaada wowote kwenye Uislamu.

  Alisema historia ya Zanzibar imegubikwa na matukio ya ugomvi, ambao umekuwa ukizuka kila wakati.

  Kutokana na hilo, aliieleza serikali kwamba, kama Wazanzibari hawautaki Muungano wanastahili kusikilizwa ili kuepusha balaa.

  Hata hivyo, alisema madai yanaweza kuwa mengine na agenda ya wanaodai ikawa nyingine na kutolea mfano wa kitendo cha wanaopinga Muungano kwenda kuchoma makanisa.

  “Unapinga Muungano unaenda kuchoma kanisa. Kanisa la nini? Kwani Kanisa ndilo lililoleta Muungano?” alihoji Mufti Simba.

  Alisema kitendo cha kuchoma makanisa kimedhihirisha kuna kitu kilikuwa kimefichwa kwa kutumia dini.

  Kutokana na hali hiyo, alisema kama Wazanzibari hawautaki Muungano, wasitumie dini kupitisha agenda yao hiyo, badala yake wasubiri mchakato wa mabadiliko ya katiba wakatoe maoni yao kwa njia za amani.

  “Mnavunja makanisa ya nini. Na hawa nao wakivunja misikiti?” alihoji Mufti Simba.

  PROFESA LIPUMBA ATAKA UCHUNGUZI

  Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametaka vyombo vya dola kufanya uchunguzi kuwabaini watu wanaoendelea kufanya vurugu visiwani Zanzibar ili wachukuliwe hatua.

  “Kwa kweli hali katika visiwa vya Zanzibar siyo nzuri kutokana na kuripotiwa kwamba makanisa na mali mbalimbali kuchomwa moto. Hivyo, ni muhimu vyombo vya dola vikafanya uchunguzi wa haraka,” alisema Profesa Lipumba.

  Profesa Lipumba alilaani matukio hayo na kusema siyo tu yanaharibu mali, bali yanachangia kuleta mgawanyiko kati ya Wazanzibar na watu kutoka Tanzania Bara.

  Alitaka kuwapo kwa uchunguzi huru ambao hautamkandamiza mtu yeyote, lakini ufanyike kwa haki na watakaobainika kuhusika na vurugu hizo wafikishwe katika vyombo vya dola ili wachukuliwe hatua kali.

  MAREKANI YALAANI

  Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, amesema ghasia zilizotokea kisiwani Zanzibar juzi, zimechafua taswira, amani na mafanikio iliyojipatia kutokana uchaguzi wa mwaka 2010 katika serikali ya umoja wa kitaifa.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Balozi Lenhardt alisema kitendo kilichotokea siku mbili zilizopita visiwani Zanzibar kimechafua taswira na utulivu iliyokuwa inajivunia kwa muda mrefu.

  “Hali iliyotokea siku mbili zilizopita visiwani Zanzibar, imechafua taswira ya Zanzibar. Pia amani na mafanikio iliyojipatia katika uchaguzi wa 2010 iliyosababisha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kimataifa,” alisema Balozi Lenhardt.

  Alisema kudumisha amani visiwani Zanzibar kutaongeza idadi watalii na maendeleo kwa manufaa ya Wazanzibari pamoja na wageni wanaofika visiwani humo.

  Aliongeza kitu cha muhimu zaidi kwa sasa ni kila mtu kulinda maisha na mali za watu wasiokuwa na hatia na kuacha mapigano yasiyokuwa na faida.

  30 MAHAKAMANI
  Viongozi wawili wa Uamsho na Mihadhara ya dini ya Kiisilamu (JUMIKI), pamoja na wafuasi wao 28 jana walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe kwa makosa ya kufanya mkusanyiko isivyo halali na kusababisha uvunjifu wa amani.
  Washitakiwa hao ni Mbarouk Said Khalfani (45), Sheikh Mussa Juma Issa (57) na watu wengine 28 wakiwemo watoto walio chini ya umri wa miaka 18, ambao walifikishwa mbele ya hakimu Mohammed Ali Mohammed Shein.

  Upande wa Mashitaka ulidai kuwa washitakiwa hao wametenda makosa hayo kinume na kifungu cha 55 (1) (2) (3) na kifungu cha 56 cha sheria namba 6/2004 cha mwenendo wa makosa ya jinai cha sheria ya Zanzibar.

  Aidha, washitakiwa wengine ni Mbwana Hamadi Juma (50), Massoud Hamadi Mohammed (17), Mohammed Juma Salum (35), Abdulrahman Simai Khatib (19), Hashim Juma Issa (54) na Matar Fadhil Issa (54).

  Watuhumiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Janet Nora Sekihola kujibu mashitaka ya uzembe na ukorofi kinyume cha kifungu cha 181 (d) cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

  Washitakiwa walisomewa mashitaka yao kwa chini ya kifungu cha 74 (1) (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

  Watuhumiwa hao walikana mashitaka yao na kupewa dhamana ya masharti ya kuweka bondi ya Sh. 300,000 na wadhamini watatu. Hata hivyo, hadi mchana walikuwa bado hawajakamilisha masharti ya dhamana hiyo.


  Imeandikwa na Mwinyi Sadallah, Zanzibar; Richard Makore, Gwanaka Alipipi, Isaya Kisimbilu na Muhibu Said, Dar.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nataka Marekani waite hao wote waliofanya Machafuko ni Magaidi; ili wasiweze kwenda nchi yoyote au kupata pesa toka Nchi yoyote ile duniani.

  Mtu yoyote anayeshambulia Maendeo yasiyo na Usalama kwa Mabomu ni GAIDI
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu nngu007 hata ukiangalia picha zao kwa style ya madevu yao lazima watakuwa ni magaidi tuu
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hahahaha acha hizo mkuu daaa!
   
 5. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,001
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kinachonishangaza ni uongozi wa serikali kuonana na viongozi wa dini, so machafuko haya ni erikali dhidi ua uislam au?
   
Loading...