ZANZIBAR: Askari matatani kwa kumbaka mlemavu

ZANZIBAR: Askari matatani kwa kumbaka mlemavu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Zanzibar. Polisi Mkoa wa Kusini, Pemba inamshikilia askari wa Chuo cha Mafunzo (Magereza) kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mlemavu wa viungo na akili.

Askari huyo wa kituo cha Kengeja, Agosti 23 alipelekwa Kituo cha Polisi Chakechake kuhojiwa akidaiwa kumbaka mlemavu huyo ambaye alikuwa jirani yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini, Sheikhan Mohamed Sheikhan alisema wanaendelea kumhoji askari huyo anayedaiwa kutenda kosa hilo miezi minne iliyopita.

“Mtuhumiwa ni askari wa chuo cha mafunzo tunamshikilia kwa mahojiano zaidi juu ya tuhuma zinazomkabilia,” alisema.
Alisema kabla ya kuhojiwa askari huyo, barua iliandikwa kwa kamishna wa vyuo vya mafunzo.

Sheikhan alisema iwapo askari huyo atabainika kuwa na hatia atachukuliwa hatua za kisheria. Askari huyo anadaiwa alitenda kosa hilo akifanya kazi Chuo cha Mafunzo Kituo cha Kengeja wilayani Mkoani, Pemba. Baadaye alipata uhamisho kwenda Unguja.

Wiki iliyopita mwanamke aliyebakwa mwenye miaka 25 alifanyiwa vipimo Hospitali ya Chakechake na vilionyesha ana mimba ya miezi minne na wiki mbili. Mwanamke alipoulizwa mhusika wa mimba hiyo alimtaja askari huyo.

Baba mzazi wa binti huyo alisema baada ya tukio hilo kulikuwa na jitihada za kulimaliza suala hilo kwa mwanaye kuolewa, lakini hakuwa tayari kufanya hivyo. Naye mama mzazi wa binti huyo alisema hakushirikishwa katika vikao vilivyoongozwa na mkuu wa kambi ya Kengeja, hivyo hana analojua. “Siku niliyopata taarifa kuwa mwanangu amepewa mimba niliieleza familia yangu, wenyewe wakawa wanakutana mara wanataka harusi mara fidia,” alisema.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Kengeja, Ramadhan Mwita alisema jambo hilo ni zito hawezi kulitolea maelezo na kwamba, msemaji ni mkuu wa Chuo cha Mafunzo kisiwani Pemba.

Hata hivyo, mkuu wa chuo hicho, Makame Kombo Ame alisema alipokea taarifa kutoka kambi ya Kengeja lakini hadi sasa hana maendeleo ya kesi hiyo.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) ofisi ya Pemba, jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili Zanzibar (Zapdd), Umoja wa watu wenye ulemavu (UWZ), mtandao wa kihabari wa Pemba today na baadhi ya wanaharakati wamelaani tukio hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Wakati ana mbaka hdi anapata mimba wtu wengine walikiwa wapi ? Kwa maoni yangu naona walikubaliana na kwakuwa yupo above 18yr na sio mwanafunzi basi hakuna kosa la jinai hapo kwani hata mlemavu anayo haki ya kushiriki tendo la ndoa pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pemba hakuna changudoa halafu dogo alizidiwa. Angekua Dar angepanda basi moja tu mia 400 toka Ukonga hadi Buguruni akaingia Mboka na buku 2 au 1 kama muda umekwenda. Ndani ya dkk 5 kesha pona kenye chocho. Hata angependa afanye kila siku. Kwa mwezi ingemkosti zi zaidi ya 60000 pamoja na korndorm
 
Tena unachagua unaye mnataka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo wanataka AMUOE HUYO DADA!!!!
Lakini kwa upande mwingine, naona huyo askari alifanya vema (kama ni kweli) kumpa penzi huyo binti, Na yeye pia ni mwanadamu, tena mwanamke anahitaji sex, but wanaume wanamkwepa kwa ulemavu wake.

Kwa hiyo anashitakiwa kwa kumpa mimba huyo dada kwa kuwa mlemavu au anashitakiwa kwa kukataa kumuoa?!!!!🙄🙄🙄
 
Wamesema kubaka kubakaaaaaaa
 
soma haka ka sehemu nime ka kopi kutoka kwenye siredi

Zanzibar. Polisi Mkoa wa Kusini, Pemba inamshikilia askari wa Chuo cha Mafunzo (Magereza) kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mlemavu wa viungo na akili.
aiseee sina neno tena
 
Back
Top Bottom