blogmaster
Senior Member
- Aug 15, 2015
- 167
- 74
Kampuni ya simu ya Zantel imetoa msaada wa kompyuta 21 na huduma ya intaneti bure kwa vyuo saba vya walimu pamoja na shule ili kuboresha na kukuza mfumo wa elimu kupitia mafunzo ya habari na teknolojia ya mawasiliano.
Msaada huo wenye thamani ya Sh milioni 34 umetolewa wiki moja tu baada ya kampuni hiyo kuzindua mtandao wa kasi wa 4G pamoja na kutanua upatikanaji wa mtandao upande wa bara.
Kompyuta hizo ambazo zimeunganishwa na mtandao wa intaneti kwa muda wa miezi mitatu zitasaidia kukabiliana na uhaba wa walimu wenye ujuzi katika teknolojia ya mawasiliano visiwani Zanzibar.
Vyuo na shule zitakazopokea msaada huo ni pamoja na Chuo cha Biashara cha Zanzibar (Unguja), Shule ya Chasasa (Pemba), Chuo cha Taifa cha Ualimu (Unguja), Chuo cha Ualimu Kiembe Samaki (Unguja), Chuo cha Ualimu Michakaeni (Pemba), Chuo cha Ualimu (Unguja) na Chuo cha Ualimu Kitogani (Unguja).
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu ya Zantel, Benoit Janin, alisema lengo la Zantel ni kushirikiana na serikali kukuza na kuboresha teknolojia na mawasiliano na kusaidia vyuo vya ualimu vinavyotoa mafunzo hayo ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji wao.
“Ni matumaini yetu mchango huu utasaidia kuendeleza elimu ya teknolojia na mawasiliano na kuwanufaisha walengwa kwa kuwawezesha kutekeleza majukumu yao na hivyo kuongeza wataalamu,” alisema Janin.
Mkurugenzi wa Bodi wa Zantel na Ofisa Mtendaji wa Millicom Africa, Cynthia Gordon, alisema walimu ndio msingi wa maendeleo kwenye taifa lolote na ndio maana Zantel imewapa kipaumbele katika miradi yake ya kijamii.
“Daima Zantel tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tunaboresha sekta ya elimu kwa Wazanzibari na kama tunavyojua elimu ya teknolojia na mawasiliano ni muhimu kwa dunia ya sasa,” alisema Gordon.
Katika hotuba yake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Riziki Pembe Juma, aliipongeza Zantel kwa jitihada zake inazofanya kwa kushirikiana na serikali katika kukuza na kuboresha elimu visiwani Zanzibar.
Zantel imekuwa ikitoa michango mbalimbali kwenye sekta ya elimu visiwani Zanzibar ikiwemo kusaidia ununuzi wa vitabu kwa maktaba kuu ya Zanzibar na pia kutoa msaada kwenye shule za msingi kama vile Kisiwandui na pia ukarabati wa madarasa katika shule ya Mikanyageni mkoani Pemba.