Zambia yanyakua Kombe la COSAFA 2019

Mawembasa1979

JF-Expert Member
Feb 26, 2015
2,153
2,502
Timu ya Taifa ya Zambia leo tarehe 08 Juni, 2019 imenyakua Kombe la COSAFA 2019 baada ya kuinyuka Timu ya Taifa ya Botswana kwa bao moja kwa bila. Bao la washindi liliwekwa kimiani na mshambuliaji hatari wa Timu ya Zambia aitwaye Tapson Kaseba katika dakika ya 78 ya mchezo. Katika mchezo huo mastaa kadhaa wa Zambia waliozoeleka na mashabiki wengi wa ndani na nje ya Zambia wakiwemo Cloutus Chama (Triple C) wa Timu ya Simba ya Tanzania na Kennedy Mweene wa Timu ya Mamelody Sundowns ya Afrika ya Kusini hawakuwepo kwa kuwa halikuwa chaguo la Kocha Ernest Chiyangi wa Timu ya Taifa ya Zambia. Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Kocha wa Timu ya Taifa ya Zambia alisema kuwa Botswana ina wachezaji wazuri ambao hawachezi kitimu kama ilivyo Zambia. Aidha, mchezaji kipenzi cha mashabiki wa Simba aitwaye Lazoulus Kambole anayechezea Zesco Un ited ya Zambia alicheza katika mchezo huo. Hata hivyo, hakuonesha kiwango kizuri cha uchezaji ukilinganisha na Tapson Kaseba kwani mara kwa mara alikuwa akianguka anapokuwa na mpira. Aidha, imeripotiwa kuwa mchezaji huyo ameshamwaga wino kwa ajili ya kujiunga na Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom