Zambia: Bunge limeahirishwa baada ya Mbunge kufariki kwa COVID-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Bunge la Zambia limelazimika kufungwa baada ya Msajili wa Bunge, Rogers Mwewa kufariki baada ya kupatwa na CoronaVirus

Mwewa aliugua na kufariki, ameshazikwa Julai 21. Makamu wa Rais, Inonge Wina alisema kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya COVID19 amelazimika kuahirisha bunge

Spika wa Bunge la Zambia, Patrick Matibini ataongoza katika zoezi la upimaji wa CoronaVirus kwa wabunge wote, zoezi linalotarajiwa kufanyika katika kliniki ya Bunge Lusaka

Karani wa Bunge amesema hadi sasa wabunge watatu wamekutwa na COVID19, pia wafanyakazi 10 wa bunge wamekutwa na maambukizi pamoja na wengine sita ambao sio wafanyakazi wa bunge

===

Zambia’s Parliament has been forced to adjourn after a legislator, Mr Rogers Mwewa, recently died from coronavirus.
The legislator from the North of the country recently fell ill and had tested positive for Covid-19. He died and was buried yesterday (Tuesday)

The country’s Vice President, Inonge Wina, said the escalating cases of Covid-19 had necessitated adjournment of the House.

Ms Wina bemoaned increasing cases of the virus despite the implementation of measures to combat its spread.

The Vice President and Speaker of the National Assembly, Patrick Matibini, will on Wednesday lead other MPs in a mass testing exercise at Parliament Buildings clinic in Lusaka.

Zambia’s health minister Chitalu Chilufya said the virus had spread exponentially the last few days.

The pandemic has spread to 44 districts in the country, he told Parliament.

Zambia’s Clerk of the National Assembly, Cecilia Mbewe, announced in a statement that as of July 15, the 19 cases recorded included three MPs, 10 National Assembly staff and six non-staff.

Zambia’s virus cases are commonly reported in urban areas, but fears are alive that the disease might spread into rural localities.

The cases have surged the past few weeks with 108 deaths recorded so far.

Due to the pandemic, the country’s economy has been left struggling with President Edgar Lungu moving to ask China for "debt relief and cancellation".
 
Pole yao na corona
Nimesikitika tu hapo Rais anaomba mchina ampe debt relief na cancellation... Zambia inaonekana waliingia mikopo mibovu sana na mchina
 
Nimekumbuka zile kauli za Ummy mwalimu alipokuwa anatangaza vifo vya corona,utasikia anasema "marehemu alikuwa na maradhi mengine". Nilikuwa najiulizaga kwamba corona ndio iliyosababisha kifo kwa marehemu ambsye alikuwa na maradhi mengine au maradhi mengine ndio yaliyo sababisha kifo kwa marehemu huku akiwa na corona kama ambavyo mtu anaweza kufa kwa malaria ila alikuwa anaumwa na mafua?

Sasa hivi hatusikii tena vifo vya corona yamebaki yale maradhi mengine tu kama zamani.
 
Huku Magufuli alisema hakuna kuahirisha bunge yaani tutafune tu pesa za wananchi
 
Back
Top Bottom