Tunapenda kuwafahamisha kuwa wale wajasiriamali wenzetu walioamua kushirikiana nasi kusambaza huu udongo kwa sasa tumewezeshena tunawatakia mafanikio mema, na wasisite kujitokeza hapa kuelezea mafanikio yao.
Tunafuraha kuwa tumeweza kama tulivyoahidi kujiwezesha 100% bila riba, tumejipatia mtaji wa bidhaa, ingawa ni mdogo kwa kuanzia lakini tukumbuke kuwa mwanzo siku zote ni mgumu, tumewasafirishia walio nje ya Dar, tunawaahidi kuwa hatuishii hapo, tutasimamia kila hatua ili tuhakikishe kuwa sote tunafanikiwa.
Tunawaomba wote wawasiliane nasi mara kwa mara ili kuhakikishia tunabadilishana mawazo na tunaelewa matumizi yote ya udongo huu na vipi una faida kwa watumiaji kuliko makemikali wanaotumia sasa hivi.
Asanteni sana.
Zainab