Bingwaman
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 548
- 288
Zaiko Langa Langa wakipiga live katika studio za televisheni nchini Zaire mwaka 1975. Quality ya video hii ni ya hali ya juu sana pamoja na kwamba imerekodiwa karibu miaka 40 iliyopita. Waimbaji kutoka kushoto ni Lengi Lenga, Bimi Ombale, Nyoka Longo na Mbuta Mashakado. Katika solo ni Felix Manuaku Waku, ambaye wengi wanakubali kuwa ni mpiga gitaa hodari zaidi aliyewahi kutokea nchini DRC. Wanamuziki wengine wanaoonekana hapa ni Teddy Sukami (rhythm), Zamuangana Enoch (bass) na Ilo Pablo (drums).
Last edited by a moderator: