Abdull Kazi
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 344
- 306
Ajali iliyohusisha magari manne imedaiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20 ktk eneo la Mkupuka, Kibiti wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo ni kwamba ajali ya kwanza ilitokea majira ya saa 4 usiku jana kwa gari dogo aina ya Toyota Hiace kuligonga Lori lililokuwa limeharibika njiani pasipo kuwekewa alama ya tahadhari na kusababisha vifo vya watu 15 na majeruhi.
Ajali ya Pili katika eneo hilo lilihusisha gari kubwa la abiria lililokuwa linatoka Kusini kuwagonga majeruhi wa ajali ya kwanza waliokuwa wakipakiwa katika gari la Halmashuri kuwahishwa Hospitali.
Kwa muda huu, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji yupo ktk eneo la tukio kwa ajili ya kupata maelezo ya kina.
Chanzo: MTU aliye katika eneo la ajali
=======
UPDATE:

JamiiForums said:MKUU wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu, ameifahamisha JamiiForums kuwa waliofariki katika ajali hiyo iliyohusisha magari matano, ni 21.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi, Machi 29, jioni ya saa 1.55 (19.55) na watu 10 walijeruhiwa ambapo wanne hali zao mbaya na wameshafikishwa Muhimbili watu sita wanaendelea vizuri.
Ajali ilianza kwa gari ya abiria Toyota Hiace T 948 CUX lililokuwa linaelekea Kibiti kugongana na Mitsubishi T 774 CJW lililokuwa likielekea Ikwiriri.
Hiace lilikua likili-ovateki Lori aina ya TATA, T 132 AFJ lililokuwa limeegeshwa barabarani na kukutana uso kwa uso na Mitsubishi.
Wakati polisi wakiwa eneo la tukio na juhudi za uokoaji zikiendelea, gari aina ya Scania Lori lilipita na kukaidi amri ya kulisimamisha na kugonga gari la Serikali, Land Cruiser STK 3531 pamoja na majeruhi na watu waliokuwa wakisaidia uokoaji.
Maiti 20 wameshatambuliwa na mwanamke mmoja juhudi za kumtambua zinaendelea hospitali ya Utete.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza alifika eneo la ajali usiku huo huo kuungana na Mkuu wa Wilaya na viongozi wengine wa vyombo vya usalama.
Viongozi hao walifanikisha kusaidia majeruhi kwenda Muhimbili Dar es Salaam jana usiku.
JamiiForums said:RPC ameifahamisha JamiiForums kwa kuwataja waliofariki kuwa ni Situs Mtanga (32) mkazi wa Ikwiriri, Nassoro Kajani (20) wa Ikwiriri, Juma Kitambulio (30) wa Mbagala, Salumu Makonde (50) wa Charambe na Shaban Bakari (30) kondakta wa Hiace, Mkazi wa Kibiti.
Wengine ni Ustadh Kalilambwe (34) wa Mbagala, Shafil Kipi (30) Mbagala, Masud Abilal (27), wa Mkuranga, Amin Mpemba (30), Japhet Ponsian (24) wa Dar es Salaam, Said China (21) wa Kimanzichana na Wasabi Sabil (45) wa Mbagala, Madadi Mangasongo (45) wa Jarib, Ramadhan Ally (23) wa Mbagala, Abdulrahman Kihemke (45) wa Kongowe, Fikiri Sauze, wa Vikindu, Seleman Mcharazi (47) mkazi wa Mbagala, Mustafa, mkazi wa Mbagala, Nywari Mshigani wa Dar es Salaam, Hassan Wasabi (18) wa Kibiti na mwanamke mmoja ambaye hajatambuliwa.