Zaidi ya watoto na vijana milioni 1.3 wamefungwa duniani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Umoja wa Mataifa umesema kiasi ya watoto na vijana milioni 1.3 wako kizuizini ulimwenguni kote. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa watu wapatao 410,000 walio chini ya umri wa miaka 18 wako gerezani.

Ripoti hiyo imesema vitendo vya unyanyasaji na dhuluma ni vya kawaida katika vituo hivyo na watoto wanakosa pia huduma bora za afya na fursa za masomo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa vijana 330,000 wako kizuizini ulimwenguni kote wakihusishwa na uhamiaji na watoto na vijana 430,000 hadi 680,000 wanashikiliwa katika nyumba au vituo kama hivyo.

Teresa Ngigi, mwanasaikolojia katika shirika lisilo la kiserikali linalotoa huduma za kiutu na kimaendeleo kwa watoto la Ujerumani, SOS anasema nyumba nyingi zinafanya kazi kama taasisi za kijeshi ambako watoto wanatumikishwa kama wanajeshi.

Ngigi amesema madhila wanayopitia watoto hao ni makubwa na kwamba vituo hivyo sio kwa ajili ya kuwafundisha nidhamu bali ni kuwapa adhabu.
 
Back
Top Bottom