beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Serikali imesema zaidi ya watanzania 408 wamekamatwa ughaibuni wakituhumiwa na kufungwa kwa kuingiza na kubeba madawa ya kulevya ktk nchi mbalimbali.
Hayo yamesemwa Bungeni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa KImataifa, Balozi Agustine Mahiga.
Akizungumzia Watanzania waliokamatwa kwa dawa hizo Mahiga amesema wanakabiliwa na adhabu hizo katika magereza mbalimbali duniani baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya kujihusisha na biashara haramu.
Mahinga alitaja idadi yao na nchi ambazo wanashikiliwa kuwa ni Brazil (41), China (266), Iran (68), India (9), Nepal (4), Oman (3), Thailand (14) na Umoja wa Falme za Kiarabu (3).