Zaidi ya wasichana 700 walioshindwa kuendelea na elimu wasaidiwa nyenzo za kujipatia kipato

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,589
2,000
wazazi.jpgWasichana zaidi ya 700 walioshindwa kuendelea na Elimu ya Sekondari katika Jiji la Tanga wamepewa nyenzo mbali mbali zitakazowasaidia kujipatia kipato ikiwemo vyerahani, vyote vikiwa na thamani ya Shilingi zaidi ya Milioni 153 ili kuepuka vitendo vya u katili na ndoa za utotoni dhidi yao.

Akizungumza mbele ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo,Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika la Maendeleo la Brack nchini, Bi, AMINA SHABAN amesema utafiti walioufanya katika mikoa mbali mbali nchini umebaini kuwa wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikisha miaka 18,wasichana wawili kati ya watano wanafanyiwa ukatili wa jinsia.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Shirika la Brack nchini, DOTO MNYABI amesema hatua hiyo lengo lake ni kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa makundi ya vijana hasa wasichana ambapo pia wanawawezesha kwa mikopo ili wajikwamue na umasikini.

Kufuatia hatua hiyo,Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Mhandisi ZENA SAID amewataka baadhi ya wazazi Jijini Tanga kuhakiki sha wanatoa ushirikiano kwa wat oto wao kwa kuwaruhusu wapewe mafunzo ya ujasiriamali kwa sababu kipaumbele cha serikali ni kusisitiza wananchi wajiajiri badala ya kutegemea kazi za maofisini.


Chanzo; ITV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom