Zaidi ya wanajeshi 80 wauwawa Yemen

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Waasi wa Houthi wawashambulia wanajeshi wa serikali wanaosaidiwa na kikosi cha muungano, kwenye mkoa wa Marib na kuwauwa zaidi ya 80 na kuwajeruhi wengine wengi

Zaidi ya wanajeshi 80 wa Yemen wameuwawa na wengine wengi walijeruhiwa kwenye shambulizi la kombora na ndege zisizokuwa na rubani yaliyofanywa na waasi wa Houthi katikati ya Yemen.Vyanzo vya taarifa hii ni maafisa wa afya na jeshi.

Mashambulizi hayo yamefanyika Jumamosi na yanafuatia miezi kadhaa ya utulivu kiasi katika nchi hiyo inayokabiliwa na vita kati ya waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran na serikali inayotambuliwa kimataifa na ambayo inasaidiwa kwenye vita hivyo na jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia.

Waasi wa Houthi walishambulia msikiti mmoja katika kambi ya kijeshi iliyoko kwenye mkoa wa kati wa Marib kiasi kilomita 170 Mashariki mwa mji mkuu Sanaa wakati wa sala ya Magharibi,kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi vilivyozungumza na shirika la habari la AFP.

Chanzo kutoka hospitali ya mjini Marib ambako wahanga wengi waliojeruhiwa walipelekwa kimesema wanajeshi 83 waliuwawa na 148 walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Mara kwa mara suala la idadi ya wanaouwawa katika mgogoro wa Yemen ni linazusha ubishi nchini humo lakini idadi hii kubwa ya wanajeshi waliouwawa Marib inaonesha kuwa ni moja ya shambulio baya kabisa lililosababisha umwagikaji mkubwa wa damu kwa wakati mmoja tangu vita hivyo vilipoanza mwaka 2014,waasi wa Kihouthi walipoudhibiti mji mkuu Sanaa.

Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani na makombora yamefanyika siku moja baada ya wanajeshi wa serikali wanaoungwa mkono na kikosi cha muungano kuanzisha operesheni kubwa dhidi ya Wahouthi katika mkoa wa Nihm Kaskazini mwa Sanaa. Mapigano kwenye eneo hilo la Nihm yanaendelea leo, Jumapili kwa mujibu wa duru ya kijeshi, na waasi kadhaa wameuwawa na wengine kujeruhiwa duru hiyo imeeleza.

DW SWAHILI
 
Hii ya kushambulia wanaoswali haijakaa sawa, lakini kiislamu kama kundi moja liko vitani inabidi lijigawanye, moja lilinde wenzao waswali, likimaliza then nalo liilindwe na lile kundi jingine nalo liswali
 
Mkuu bado hakuna mantiki sana point hapa ni kuacha kusali muda unaojulikana. Kuwashambulia waislamu ni vyepesi maana unajua fika lazima waswali wakati fulani. Wangekuwa dini nyingine ni muda wowote hivo ukishambulia nyumba yao ya ibada watakufa wachache. Hata vita ya 1973 Egypt waliishambulia Israel siku ya Yom Kippur ambayo ni sikukuu hivo watu walikuwa mapumziko. Kule Korea, Japan, Vietnam na China ambush kama hizi unawapata wachache tu. Na kitu kingine hii ni drone and missile attack, kuweka walinzi nje hakuzuii.
 
Eti wanajeshi wa serikali...wale Ni mamluki wa Saudi Arabia sio wanajeshi wa serikali ya yemen
Kwanini unawaita mamluki? Kwani hao sio raia wa Yemen sema tu wanasaidiwa kifedha,silaha, Mafunzo na utawala wa Saudia?

Kama kusaidiwa na taifa hasimu ni mamluki basi hata Houthi wanaosaidiwa na Iran pia ni mamluki vilevile
 
Ni wasudan,morroco,Saudi,wahindi na raia wachache.
Jeshi halisi la iliyokuwa Yemen,walijiunga na houthis,ndo maana wana hizo missile,zinatoka kwenye maghala ya ilokuwa jeshi la Yemen,
 
Kwanini unawaita mamluki? Kwani hao sio raia wa Yemen sema tu wanasaidiwa kifedha,silaha, Mafunzo na utawala wa Saudia?

Kama kusaidiwa na taifa hasimu ni mamluki basi hata Houthi wanaosaidiwa na Iran pia ni mamluki vilevile
Kuhusu houthi kusaidiwa na Iran mfano kwa kuwapa silaha,sio kweli,angalia ramani na ujue Yemen iko blockaded na jeshi la maji la Saudi na Egyptian,
Kwa hiyo uwezekano wa kuingiza silaha toka iran Ni mdogo.
Iran inaunga mkono houthi na imepeleka kikundi kidogo Cha wataalamu ambao ndo wanaushirikiano na houthi na jeshi la Yemen,kuimprove guidances system ya makombora
 
Hivi Iran huo uchumi wake bado haujadondoka tu.. maanake miaka yote hi wanafadhili makundi kibao middle East.

Sent using Jamii Forums mobile app
GDP ya Iran Ni Karibu dola billion 500.
Kwa kulinganisha GDP ya Israel ni inachezea billion 300 maximum.
Hata hivyo mfano bajeti ya msaada kea hezbulah ya lebanan kwa mwaka haizidi dola milion 300,
Vikundi vya militias vya Iraq,PMU wanapokea mishahara toka wizara ya ulinzi ya Iraq,
Vikundi vilivyoko Syria ndo vinategemea msaada was Iran,lakini Ni vidogo bajeti hawezi dhidi USD milion 500 kwa mwaka
 
Kumbe!
Basi pia watu hao wako committed Sana kufa kwaajili ya Iran. Coz kwa bajeti Kama hiyo ndogo mnakubalije kupigana dhidi ya adui went nguvu alsaudi, Israel, na NATO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ya kushambulia wanaoswali haijakaa sawa, lakini kiislamu kama kundi moja liko vitani inabidi lijigawanye, moja lilinde wenzao waswali, likimaliza then nalo liilindwe na lile kundi jingine nalo liswali
Walinzi walikuepo ila nao pia wamekufa. Kaka usicheze na ballistics missile hazijawai muacha mtu salama juzi tu hapo iraq kambi ya US imekua kama handaki vile. Ndo maana EU+US kila siku wanapiga kelele kulaumu baliistic missile za Iran.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom