Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,529

Wakazi zaidi ya 2,000 wa kijiji cha Chembeli kata ya Didia wilayani Shinyanga wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kufuatia mradi wa maji uliojengwa mwaka 2014 kuwekwa mabomba mabovu hali inayosababisha wakazi hao kuchangia maji ya kunywa na mifugo katika mabwawa yasiyo rasmi.
Wakizungumzia hali hiyo baadhiya wakazi wa kijiji hicho ambacho kinadaiwa hakijawahi kutembelewa na mkuu wa wilaya yeyote tangu kianzishwe wamesema licha ya mradi huo kujengwa na kukamilika mwaka 2014 mabomba yaliyowekwa yamekuwa yakipasuka mara kwa mara na kusababisha maji kukosekana hali inayowalazimu wanawake na watoto kutumia muda mrefu kutafuta maji.
Sylivester Mpemba ni mkandarasi anayelalamikiwa na wananchi kujenga mradi huo na kuweka mabomba mabovu amesema mradi umezingatia viwango lakini kwa sasa anafuatilia sababu zinazosababisha changamoto ya mabomba kupasuka
Kufuatia malalamiko ya muda mrefu ya wananchi mkuu wa wilaya ya shinyanga Bi.Josephone Matiro akalazimika kuingilia kati na kumuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga DC kuunda timu ya wataalamu na kuchunguza mradi huo ndani ya siku 30 na kurudisha majibu.
Chanzo; ITV