Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,314
- 72,740
Habari zilizonifikia hivi punde ni kuwa zaidi ya nusu ya walioteuliwa kushika nafasi ya Ukurugenzi wa Halmashauri za wilaya na miji siku chache zilizopita wataenguliwa wakati wa kuhakiki CV zao kwa kutotimiza viwango na sifa za kazi hiyo.
Uhakiki huo kumbe ni shinikizo kutoka Tume ya mipango na TAMISEMI walio hoji kuwa kazi hiyo muhimu kupewa watu wasio na ujuzi wala uzoefu wa usimamizi wa fedha na mipango ya maendeleo na sheria zake za Local Govt.
Wameshtuka kuwa mambo yatakuwa magumu huko mbele na yakikwama lawama ni kwao. Pia kuna uwezekano wa ripoti ya CAG ndani ya miaka miwili kuwa na madudu ambayo hayajapata kutokea katika historia ya serikali za mitaa.