Z`bar withdraws passports of unregistered Comorians

Another Witch-hunt doomed to fail and only serve to taint SMZ's reputation.Pasi za uraia wa Jamuhuri ya Muungano issued mid 60's,were they revoked?
 
siasa tu hizo hata Amani Karume hajaukana uraia wake wa Malawi mpaka leo na wala baba yake hajafanya hivyo.
 
Mwanzo wa ngoma ni lele!!
Najua wanakoelekea msichekelee wanataka kutoa pasi za Zanzibar mwisho wa safari moja ni mwanzo wa safari nyingine. Hivi nikumbusheni uhamiaji haiko chini ya wizara ya mambo ya ndani na ni jambo la muungano au nazeeka vibaya. Hapo zamani when I was still active jeshini nafikiri jeshi ulinzi na polisi ni mambo ya muungano kwa hiyo Zanzibar hawaruhusiwi. Najua kwa ubabe walianzisha KMKM hapo sijui kama katiba ilipinda au ni sawa tu. Labda naota au siku hizi ukijisikia tu unamwaga radhi si Rais anacheka na kutabasamu!!!!
 
ndugu zanguni, ni lazima tuifahamu vizuri Katiba yetu kabla hatujaendelea mbele na hili suala. Suala la citizenship ni suala la Muungano, na kwahivyo SMZ haiwezi kutamka mambo kama haya without a node from DSM. Haya yote yanasukwa DSM!!!

Kikatiba SMZ haiwezi kuchukuwa hatua yoyote ile on citizenship on its own - sawa na kuwa SMZ haiwezi kuamua peke yake juu ya any issue on Foreign Affairs, Natural Resources, etc etc - kwani haya ni mambo ya Muungano tokea April 1964!. Kama wanaweza kuingilia mambo ya Muungano basi wajiunge na Umoja wa Waislamu au wachimbe hayo mafuta yao peke yao!

Hapa SMZ imetumiwa tu, lakini amri imetoka DSM ili lipunguke zogo hio 2010. Kwahivyo, tutumie akili zetu na tusipumbazwe kama watoto wadogo by those who hold power in DSM.
 
SMZ haiwezi kutamka mambo kama haya without a node from DSM. Haya yote yanasukwa DSM!!!


..any issue on Foreign Affairs, Natural Resources, etc etc - kwani haya ni mambo ya Muungano tokea April 1964!.

...Hapa SMZ imetumiwa tu, lakini amri imetoka DSM

Amri iliyotolewa ya SMZ kusitisha mikataba ilotiwa na s'kali ya Muungano kutafuta mafuta ZNZBar nayo ilitoka Dar? Maana mafuta nayo, kwa mujibu wa Katiba ambayo unasema tujifunze, mafuta ni ya muungano, au?
 
Last edited:
kumbe pale wapemba walivyo sema ni kweli kuwa wanataka kisiwa chao kijitenge nainga mkono wapemba wajitenge imekuwa sasa ni kibri cha watu wa unguja kujiona sana na kisiwa chao wakati utajiri wote walio wahi kuwa nao unatoka pemba hata hayo mafuta pia yako pemba nawaombea ukimbizi waende pemba hakuna biguza wao ni wenzenu lakini kumbukeni akina karume na hao wanao fanya njama hizo kuwa na wao sio kwao karume kazaliwa malawi na yeye hao watoto wake na wajukuu zake nao watafute kwao hili leo kwa wacomoro kesho kwa wabara wanao tumiwa kuja kujiandikisha znz na wao yatawakuta hayo
 
Zanzibar inatia aibu. Kama kuna watu wameishi kuanzia miaka ya 60's na unawaambia sio raia kwasababu babu zao walitoka morocco ni vichekesho na ubaguzi wa hali ya juu. Je watu watawekeza vipi kwenye sehemu yenye ubaguzi wa namna hii!

Tatizo la Zanzibar lipo kwa wahuni wachache mahafidhina ambao wao wanajiona kuwa Zanzibar ni mali yao na wana hati miliki ya kuongoza milele. Kila kukicha wanafikiri ni jinsi gani ya kupunguza kura za CUF na kuongeza zao, wakiisha ona kuwa wewe haupo upande wao basi wanakutafutia sababu yoyote ile kukunyong'onyeza. Hawa watu si wazalendo bali ni wasaliti wanaongalia maslahi yao zaidi ya maslahi ya Wazanzibar wote, na wapo tayari kuhatarisha maisha ya Wazanzibar kama wataona kuna tishio la kunyang'anywa uongozi kwa kura. Kazanzibar kenyewe hakafiki hata watu milioni, badala ya kujenga umoja wao wanaongeza mpasuko, na hii itaenda na kuwarudia wenyewe, kesho na kesho kutwa itamrudia Shamuhuna na kundi lake la wahafidhina wanaofukuzia madaraka 2010.
 
Last edited:
Sehemu hii ya Jamhuri ya Muungano kweli haina viongozi na wanatia aibu taifa la Tanzania, Wangazija wa Zanzibar ni raia kamili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wao wapo Tanzania kwa zaidi ya generations nne au tano vipi leo wanaambiwa si raia?

Wangazija wapo Dar es Salaam wapo Mtwara wapo Tanga Wapo Moshi Wapo Arusha na sehemu zote za Jamhuri ya Muungano. Zanzibar haina wizara ya mambo ya ndani vipi wao wanaweza kumvua mtu uraia, mambo ya uraia yapo chini ya Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, kama waziri ataeleza kuwa watu wenye asili ya Ngazija sio raia basi iwe
kwa wote wanaoishi katika Jamhuri ya Muungano na sio wale wa Zanzibar peke yao.

Hawa viongozi wa Zanzibar wameanza ubaguzi siyo leo tu walianza kwa wananchi wa kisiwa cha Pemba kwa kuwabana katika nafasi za uongozi, elimu na hata mahitaji muhimu. Kiongozi wa kweli huwezi kuwabagua wananchi wako hata kwa maendeleo,

Ubaguzi wao hautoishia hapo wakimaliza kwa Wangazija watawabagua wananchi wanaotoka Bara hivyo hivyo na Wahindi na watu wenye asili ya Uarabuni.
Wakati umefika kwa Rais Kikwete kuwakemea viongozi wa Zanzibar kwani kuwaachia wataitia doa kubwa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania mbele ya jumuia ya Kimataifa.
 
Kunahitajika tamko kutoka kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar au Tanzania kwa kifupi ,hapa atolee tamko kuhusiana na hili maana hata hapa Tanzania Bara wapo Wangazidja na kwa siku hizi za karibuni kumetokea urafiki mkubwa kiasi ya Comoro kutaka kuwa ni moja ya sehemu ya Tanzania ,kutokana na amani na utulivu.

Ila kitu kimoja ambacho nahisi ndio kinachopelekea uchochezi huu kutoka kwa Viongozi wa SMZ nao ni kuona kuwa hawana sapoti kutoka kwa jamii hii ya WaComoro wanaoishi pale ZnZ ,kwa maana wamelichonga hili ili kupunguza wapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao na ukishapita uchaguzi litakuwa kama halikusemwa ,hapa waComoro wataekewa kizingiti cha kupiga kura kwa kuwa si wananchi wazalendo ,hesabu za SMZ ni kuwapunguza wafuasi wa CUF kwa kadiri itakavyowezekana ,lakini kwa hili naona wanajidanganya ,Zanzibar hakuna atakaeipigia kura serikali iliyopo madarakani kwa msemo mwengine hakuna atakaeipigia kura CCM ,hilo ndilo linalovuma hivi sasa katika visiwa vya Zanzibar.
 
Hii issue ikiingia kwenye International media na UN wakiijua itasababisha ZNZ na Serikali ya Muungano kunyimwa misaada. Hizi zote ni kampeni za CCM za uchaguzi mwaka 2010 ambazo zinaweza zikaipeleka pabaya TZ. SMZ na Serikali ya muungano acheni UJINGA wenu.
 
Huku ni kukosa kazi za kuchangamsha akili maana badala ya kujenga, tunazidi kubomoa. Zanzibar kuna watu wameanza kupitiwa na usingizi mnono wa madaraka wanajisahau.Ivory Coast iliharibika na vitu vya aina hii hii. Ngoja tusubiri tuone wakina yakhe wanatengeneza nini kwa usumbufu huu wanaouanzisha

Mkuu elwa kuwa SMZ wanawategemea Bara wanajuwa kuwa wakitaka lolote watatekelezewa ikiwa askari wa kwenda kutowa Roho watu au kufanya unyama wa aina yoyote ile watapelekewa.
 

Kunahitajika tamko kutoka kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar au Tanzania kwa kifupi ,hapa atolee tamko kuhusiana na hili maana hata hapa Tanzania Bara wapo ...

Yakhe, na wewe Mwiba upo Bara? Baniani mbaya kiatu chake dawa.

Huyu Mwiba ni sampuli ya Wanzanzibari wengi walivyo, hawaishi kulia kuonewa, kutaka kujitoa, lakini kiukweli wanapenda Tanzania, vinginevyo wangeshaondoka zamani. Wanajua Zanzibar hakuna kitu, kakisiwa kale hata polisi wao hakana! Wanadeka tu, maana wanadekezwa. Bara wanawaangalia tu wanavyodeka, bado hajajitokeza mtu wa kusema imetosha, wengi wanaogopa kuwa wa kwanza kuambiwa walivunja Muungano.

Ila yana mwisho, kuna siku kichaa mmoja wa Bara atawafukuzilia mbali. Mizengo Pinda ameshatoa dalili hizo za kutojali political correctness. Atakuja kichaa zaidi ya Pinda kukata ngebe zao za sitaki nataka. Yana mwisho.
 
Ninafikiri hizo quote mbili hapo juu zinatosha kumjibu huyo muheshimiwa labda kama analingine kuhusiana na hao watu
He argued that as per Chapter 39 of the Laws of Zanzibar, the status of the people of the Comorian origin were not the Sultan subjects and were therefore considered as “aliens.”

Apertheid South Africa pia ilikuwa na sheria,justice na sheria vitu mbili tofauti.
 
Bluray,
Mkuu wangu Zanzibar haina passport lakini haya ndio mawazo ya Viongozi wa Zanzibar. Jana ilikuwa wabara kuingia na pass, sijui wafukuzwe ni wahamiaji, basi hili la Wakomoro ndio litakalo imaliza Zanzibar...Yaani serikali hiyo imegusa pabaya... Sasa ndio utasikia vita ya siasa ndani ya Zanzibar, vita ambayo haitakwisha leo wala kesho kwa sababu nijuavyo mimi Zanzibar ni nchi inayoitamba kwa sababu ya Wakomoro. Wooote wanaopiga kerlel za Muungano na haki za Zanzibar ni Wakomoro kwa asili..

Bara tunawavumilia kwa kila hali sii kwamba hatufahamu asili zao ila ni ktk kutambua Historia ya nchi hiyo ktk mkusanyiko wa makabila mengi ya dunia... Huu ndio mwanzo mkuu wangu utaisikia vurugu hii ikipamba moto kabla ya uchaguzi.. Sii ajabu bakora zikatemmbea..

Kwa maana hiyo hili ni zengwe la kutungwa Dodoma lakini chonde chonde na kutumiwa kwa manufaa ya wengine.
 
What a F..........Sultan subjects stand for!..

Sheria nyingine jamani aaaah! ama kweli Miafirka Ndivyo Tulivyo.





Huu ndio mseto! Kwani si tunajigamba kuwa tumewaondowa masultani halafu tunawarefer kwenye utaifa wetu . Pole sana sisi na hizi njaa zetu.
 
Wangazija ni very smart people :)
1968 walitakiwa kukataa kuwa French subjects na kuwa Zanzibar subjects. Wengi waliokuwa mashule wakati huo ilibidi wajiandikishe kuwa Wazanzibari ili waweze kufanya mitihani.

Wale ambao hawakuwa na mitihani ya kufanya walikauka na kuendelea kushikilia pasi zao za kifaransa. Ndio maana utakuwa Wangazija wamejaa Europe kwa sababu wengi wamedai hati za kifaransa.

Hawa ndio wanaoleta matatizo ya tamko hili kutolewa...hatuna dual citizenship...undumilakuwili haujahalalishwa BADO. Sasa wanaotaka kuwa Wanzanzibari, wamepewa tena nafasi wajiandikishe.
 
Ninafikiri hizo quote mbili hapo juu zinatosha kumjibu huyo muheshimiwa labda kama analingine kuhusiana na hao watu

Mungu wangu ni aibu hii na nikifikiria niliwahi kumtetea huyu Muheshimiwa kumbe hahitaji na anapaswa kuchukuliwa kama alivyo. Kukubali kutumiwa huku ukijiaibisha ni Noma Noma kweli Bwana Mwinyichumu!
 
Hivi kwani sheria ya uraia inasemaje?

Kwani ukiishi kwenye nchi nyingine miaka mingi unakuwa raia automatically? Si kuna sheria na taratibu za kuupata uraia? Kwanini baadhi ya Wakomoro hawakuzifuata hizo taratibu na wengine walizifuata?

Tusianze kulalama bila sababu za msingi, wanachofanya Zanzibar ni kutekeleza na kusimamia sheria zao za uhamiaji, siyo ubaguzi!


Zanzibar baada ya Mapinduzi ikiendeshwa na kauli ya Karume na sio Sheria na Karume aliwatangazia Wacommoro wote ni Raia wa zanzibar na hata Wahiundi na wengineo na kupewa kadi za uraia. Sasa sheria gani walioivunja hao Wacommorow? Hii ni jaja ya CCM kwani mmeshasahau ya Ali Nabwa aliekuwa mwiba kwa SMZ?
 
Zanzibar bana, hamkosi jambo? Miye nilidhani huu ndiyo wakati wa kumjua na kumrudia Mola kumbe nyie mnaaza kuwatafuta Wa-Comoro? Inachekesha! Inaleta kichefucefu! Inaonyesha ufinyu wa fikra za viongozi!

Baada ya Wa-Comoro, watafuata Wa-BARA, Baadaye Wa-Pemba baadaye...

Mnaturudisha nyuma walahi!


Haha!haha! Usinichekeshe. Masterminds wafukuzwe? Kama umekosa kiwanja huko Bongo njoo tu Zanzibar lakini usije ukamtaja Mbongo mwenzio Lipumba, wewe utakuwa sawa na hao Wacomorro.
 
Amri iliyotolewa ya SMZ kusitisha mikataba ilotiwa na s'kali ya Muungano kutafuta mafuta ZNZBar nayo ilitoka Dar? Maana mafuta nayo, kwa mujibu wa Katiba ambayo unasema tujifunze, mafuta ni ya muungano, au?

Kwani NEC walisemaje kuhusukauli hizo? Wao wameenda mbele kwa kuwaamuru SMZ kuwanyamazisha hao wanaoshabikia jambo hilo. Hapo Mkuu mkono wenu hautoki, upo tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom