Yusuf Manji amekatwa udiwani Mbagala

Yusuf Manji amekatwa udiwani Mbagala

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267

Manji (katikati) akiwasili kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam


Kwa mujibu wa taarifa za ndani ambazo mtandao huu umezipata zinaeleza kwamba jina la Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji inasemekana limeenguliwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Udiwani Kata ya Mbagala Kuu.

Vyanzo vinaeleza kuwepo kwa mchezo mchafu ‘figisufigisu’ katika ‘kulikata’ jina lake, wakati alishinda kwa kishindo kwenye kura za maoni akiomba kuteuliwa na chama chake cha CCM kugombea nafasi hiyo.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo walijazana kwenye ofisi ya chama hicho mkoa wa Dar es Salaam wakisemekana kukipinga kuenguliwa kwa Manji, huku wakitaka ufafanuzi wa kina juu ya sababu zilizotumika kuliondoa jina lake mpendwa wao.

Hata hivyo mpaka sasa Chama Cha CCM hakijatoa tamko juu ya sakata hilo.


Mtandao huu ulijaribu kufanya mazungumzo na Manji lakini alidai hayuko katika hali yake ya kawaida kutokana na kusumbuliwa na maradhi hivyo hakuwa tayari kuzungumza chochote kwa muda huo na kuomba akimilishe kile kilichompeleka kwenye ofisi za CMM Mkoa.

Baada ya zoezi la kuzungumza na Manji kukwama, mtandao huu ukaona ni vyema kuzungumza na baadhi ya wanachama ambao walikuwa wamepiga kambi kwenye ofisi hizo kusubiri hatma ya mgombea wanaedai ndiye chaguo lao.

Chanzo: ShaffihDauda
 
Jamaa bado wanakatana tu.CCM wametoa tamko kwenye magazet ya jana niliskia,moja wapo ni kwamba alitumia hila kwenye uchaguz. Labda Manji alizidisha ila CCM unapataje uongoz bila hila?
 
Madabida ana roho mbaya sana yule baba aliye fanana na popo. Embu fikiria mtu ametengeneza ARV fake ndio ashidwe kumkata MAnji
 
Wampitishe tu huyo muhind asye ijua hata mbagala yenyewe
Ataadhibiwa na ukawa
 
Ndio wamemkata, nilishangaaa sana walimptishaje mwanzoni. Aibu imewatawala basi wakaamua kumuondoa!1
 
Bado sijaelewa mantiki ya Manji kugombea udiwani, halafu Mbagala wakati yeye anakaa sea view Upanga..!
 
kote ana miji midogo na mikubwa SEA VIEW NI ENEO LAKE LA MAMBO FULANI

Ha ha ha Mkuu.. So unadhani udiwani ilikuwa ni njia ya kumuweka jikoni vinapopikika vyakula..? Maana sifa moja ya Manji ni uwezo wake wa biashara ya ardhi..
 
ha ha ha mkuu.. So unadhani udiwani ilikuwa ni njia ya kumuweka jikoni vinapopikika vyakula..? Maana sifa moja ya manji ni uwezo wake wa biashara ya ardhi..
swadaktaaaaaaaaaaaa
 
swadaktaaaaaaaaaaaa

Nakumbuka sakata la viwanja vya Bakwata pale Chang'ombe.. Na alivyoweza kuvigawanya fasta viwanja baada ya "kuuziwa" na yeye akaviuza vpande.. Manispaa panamuhusu sana Mkuu..
 
Ahamie ule upande mwingine maana CCM siyo mama wala baba yake.
 
nakumbuka sakata la viwanja vya bakwata pale chang'ombe.. Na alivyoweza kuvigawanya fasta viwanja baada ya "kuuziwa" na yeye akaviuza vpande.. Manispaa panamuhusu sana mkuu..
lile eneo bado lina uzio tu ila inaonekana wameachia kukaza
 
Back
Top Bottom