Yussuf mehboob manji, alhaj mtarajiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yussuf mehboob manji, alhaj mtarajiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bwana Mapesa, Oct 17, 2012.

 1. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,926
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Na Mahmoud Zubeiry

  1__MANJI.jpg
  MWENYEKITI wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Yussuf Mehboob Manji kesho anatarajiwa kwenda Makka, Saudia Arabia kufanya ibada ya Hijja.Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka kwa mtu aliye karibu na Manji zimesema kwamba, Manji ameamua kwenda kufanya ibada hiyo ya Hijja kufuata asili ya ukoo wao, wote waislamu safi.Ibada ya Hijja inatararajiwa kufanyika wiki ijayo Makka na kundi la mwisho la waumini wa dini ya Kiislamu litakalokwenda huko, linatarajiwa kuondoka kesho.Akikamilisha ibada ya Hijja, Manji atakuwa sawa na Mwenyekiti wa wapinzani wake wa jadi, Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, ambaye alikwenda kufanya ibada hiyo mwaka 1999 kwa ofa wakati huo akiwa bado Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania (TFF), sasa shirikisho (TFF).Manji amekuwa mfadhili wa Yanga tangu mwaka 2006, wakati klabu hiyo ikiwa chini ya Mwenyekiti, Francis Mponjoli Kifukwe na baada ya kuona jitihada zake za kuifanya Yanga iwe ya hadhi ya juu zinakwamishwa na viongozi, Julai 14, mwaka huu akaamua kujitosa kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo, katika uchaguzi mdogo.Ni miongoni mwa wafanyabiashara vijana wenye mafanikio makubwa, ambaye amerithi na kuendeleza vema utajiri wa baba yake, marehemu Mehboob Manji.
  Ibada ya Hijja ipo katika nguzo ya tano ya Uislamu; inayomtaka muumini wa dini ya Kiislamu mwenye uwezo kwenda kuitekeleza ibada hiyo na kuna imani kwamba baada ya ibada hiyo, muumini huyo hufutiwa dhambi zake za awali ila baada ya hapo, hatakiwi tena kurudia kufanya yaliyokatazwa na mafundisho ya dini hiyo na akifanya hivyo 'atajipalilia makaa ya moto' siku ya hukumu.
   
 2. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 595
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Manji ni Muislamu?!!!
   
 3. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  teja na makka duuuuuh ni sawasawa na kujisifia eti snoop dogg ni muislam....
   
 4. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe Hijja Firauni yoyote anaweza kwenda, Duuuuh.
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  huo uhakimu nani kakupa?!
   
 6. s

  salmar JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Kwani vatican hakuna ma firauni
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Haaaaaaaaaaaaaaaaa disco limeingia mmasai
   
 8. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ajiandae kwa kuwa akirudi atakuta watiifu kwa Sheikh Ponda watakuwa wamejiimarisha kutwaa mali zake.
   
 9. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Hivi sheikh ponda nae ameshawahi kwenda kuhiji
   
 10. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,926
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Wakuu thread imejieleza kwamba kwa kushirik ibada ya hijja muumin hufutiwa dhambi zake,labda dogo kaamua ku start afresh...
   
 11. salito

  salito JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Kwani misikitini au makanisani hakuna mafirauni?kule ni sehemu ya ibada tu,labda utuambie kama kuna kifaa cha kuwachuja mafirauni.
   
 12. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 13. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  kazi ipo!! :A S-coffee:
   
 14. Askari wa miguu

  Askari wa miguu JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani kakwambia yeye mkatoliki au Vatican ndio mnayoijua sana, ukishasoma Al Nuur uingiage na google kuna madhehebu kibao co kila mkristo unaemuona umekariri wa Vatican, ovyo!
   
 15. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  arejeshe kwanza zile pesa walizoshirikiana na Dr. Dau kuwaibia wanachama wa NSSF walipouziana bei ndogo kisha Manji akawauzia kwa bei kubwa kuliko maelezo.... ndipo aende kuhiji...
   
Loading...