Yupo wapi winga machachali (The Game Changer) Bwana Mdogo Tepsi Evance?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,288
12,789
The football fan NALIA NGWENA nimejikuta namkumbuka kijana machachali Teps Evance winga mwenye kasi na winga anayeipiga miguu yote (kulia na kushoto).

Nilipomuuona kipindi kile ameitwa Timu ya Taifa (taifa stars) kutokana na umri wake niliona ni msaada mkubwa sana kwa taifa letu kutokana na Talanta/kipaji alichokua nacho bwana mdogo Tepsi Evance.

Huyu ni namba Saba (7) mwenye kasi mwenye kujua chenga hakika ni winga wa mpira haswaa bwana mdogo ana talanta ya mpira kichwani mwake.

Msimu umeisha bila ya kumuona Tepsi Evance na kila nikichungulia game za Azam Fc sioni hata jina lake kwa upande wa sub.

Mnaojua/wenye taarifa ya huyu bwana mdogo mwenye talanta kubwa kuliko hata Pape osumane Sakho na Kibu Denis aje atuambie huyu bwana mdogo yupo wapi?

Screenshot_20230609-131807.jpg
 
Alienda kwa wanambogomaji kwa mkopo lkn sasa karudi kwa wauza ngano yupo mitaa hiyo kashindwa kupenya kwenye kikosi cha matajiri hao
 
Dogo hawezi kutoboa kwenye game ya bongo,anapenda sana malaya na anakula bange kupitiliza...

Nimekaa nae sana pale 5star lodge ubaruku...

Kama alilewa na posho ya 200k kila week pale mbarali unadhani atatoboa kwenye 2mil chamazi..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom