Yupo wapi Patrick Tsere?

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Aliwahi kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Karatu kupitia CCM mwaka 2005 na kubwagwa na Dk Willbroad Peter Slaa.

Baadae aliwatumia wananchi watatu wenyeji wa Karatu kufungua kesi dhidi ya Ushindi wa Dk Slaa, kesi ambayo ilitetewa na Tundu Antipas Lissu hatimae kuibuka kidedea.

Wakati akiwatumia wananchi hao kulalamikia ushindi wa Dk Slaa aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke lakini mwanzoni mwa mwaka 2010 Rais alitengua uteuzi wake katika mabadiliko aliyoyafanya katika Wilaya mbalimbali nchini na kuhaidi kwamba Patrick Tsere atapangiwa kazi nyingine.

Sababu za kutenguliwa kwake hazikujulikana na tangu siku hiyo hadi leo sijasikia yupo wapi majeruhi huyu wa siasa za Karatu.
 
Hivi muuliza swali anaishi nchi gani mpaka asijue issues za kitaifa. Kama alijua kwamba aligombea ubunge na akashindwa, kujua yuko wapi sasa hivi ingekuwa ni rahisi.
 
Hivi muuliza swali anaishi nchi gani mpaka asijue issues za kitaifa. Kama alijua kwamba aligombea ubunge na akashindwa, kujua yuko wapi sasa hivi ingekuwa ni rahisi.

Mbopo,
Ndugu yangu nafuatilia sana maswala ya kitaifa ila taarifa za huyu Patrick Tsere sikuziwahi kuzisikia tangu alipotenguliwa ukuu wa Wilaya pale Temeke. Nadhani hata alipoteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi sidhani kama Press release ilitoka. Nashukuru kwa wachangiaji kunipa update za huyu majeruhi. Tumuombee Mungu abaki na huo ubalozi wake na siku Dk Slaa atakapotembelea Malawi kama Rais wetu baada ya 2015 yeye ndiye awe mwenyeji wake.
 
Nadhani popote pale alipo kawe hatosahau alivyonusurika mikononi mwao Wamachinga wenye hasira pale Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Huo ndiyo uliokua mtihani mkubwa zaidi kwake katika utumishi wa Temeke jiji Dar es salaam.
 
Alipojitia kwenda kumwakilisha Mkuu wa Mkoa wa wakati huo kwenda kuwasikiliza Wamachinga na matatizo yao, nakuambia kulimtoka unyoya mbele ya wana VIBINDO kiguu na njia hao.
 
Amepotezwa Malawi huko anasubiri OC ndio ale....njaa tupu ubalozini huko!!! Acha abwabwaje maana njaa inahamia kichwani!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom