Yupo wapi Mwanasiasa Iddi Simba.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,224
6,468
Habari zenu wanajukwaa. Mtakumbuka miaka ya nyuma alikuwepo mwanasisa nguli Iddi Simba. Aliwahi kuwa Mbunge wa Ilala na waziri ktk wizara mbalimbali humu nchini. Sijamsikia siku nyingi wala kupata habari zozote zinazomuhusu. Hivi gwiji hili la siasa lipo wapi na linafanya nini sasa?
 
Hakuna kinacho salia chini ya jua,wakati wake ulishaisha kamaivo.
Hata uweje katika maisha lazima kuna siku utaisha na kupotea kabisa hasa kwenye ulimwengu wa siasa.
Hata makonda na Magufuli tutakuja kuwasahau kama huyo Iddi Simba.
 
Ngoja nikae kimya...kuna mahali hua namuona ila kimuonekano afya yake inaonosha hayuko poa nadhani ni uzee
 
Habari zenu wanajukwaa. Mtakumbuka miaka ya nyuma alikuwepo mwanasisa nguli Iddi Simba. Aliwahi kuwa Mbunge wa Ilala na waziri ktk wizara mbalimbali humu nchini. Sijamsikia siku nyingi wala kupata habari zozote zinazomuhusu. Hivi gwiji hili la siasa lipo wapi na linafanya nini sasa?
Baada ya yale mambo ya UDA hakuna namna ni kukaa kimya tu.
 
Back
Top Bottom