Hahahaa, wewe utakuwa ulikuwa unakaa Bweni la Ujamaa kwa Mwalimu Mwakyembe.
Nakumbuka enzi hizo, siku moja alikuwa kajifungua Chemba anajipigia gitaa lake wala hana habari kumbe nje vijana kibao tumekaa tukiburudika mziki. Watu wakashindwa kuvumilia wakamwita na akatoka nje na kushangaa umati wa Wanafunzi. Jamaa wakamletea kiti na watu wakawa wanachagua nyimbo na anatupigia kama onyesho la saa moja. Akalalamika vidole vinauma na tukampigia makofi ya kumshukuru.
Nilikuja kukutana naye miaka ya 80 mwishoni kama sikosei mitaa ya Dar ila sikumbuki alikuwa akifanya kazi wapi.
Home mate alikuwa akilipiga gitaa si kawaida. Headmaster wa Kazima alipata shida sana kujua amfanyeje kwani Kindaza inasemekana alitishia kuacha shule ili awe Mwanamuziki aweze kupata fedha za kuwahudumia Wadogo zake - RESPECT kwa hilo ndugu Kindaza. Mwisho wakaishi kuwa wanamruhusu Jumamosi anapiga sijui hadi saa NANE na hapo wanamruhusu arudi shuleni.
Mie nilikuwa Dogo sana mwaka huo na sidhani hata utaweza kunikimbuka. Ila Mwaka wetu ndiyo ulikuwa na Wachezaji wengi wazuri sana wa Mpira ukiacha wale Mastaa kama Jabir Kasenga, Mapilau? Adolf Kondo, nk maana sisi tulikuwa na hawa wanaojaziajazia minofu kama Sunday Kalonga, Ferruz Hanzuruni, Musa Zuberi, Athman Mtoro na wengine kadhaa huku Mwalimu wa Mpira akiwa Mwalimu Shaban (Na yeye kutoka Tabora ila ni Marehemu siku nyingi sasa).