Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
AMEKUWA ORIGINAL
Najua unalalamika kuwa mumeo kabadilika sana sikuhizi, zamani hakuwa hiyo, alikuwa mtu mwema mwenye mapenzi, alikufungulia mlango wa gari kabla yeye hajaingia, alikusogezea kiti ukae kabla yake, alikuwa mwepesi kusema sorry baby, aliwahi nyumbani na kusema kila anakokwenda. Najua unalalamika kuwa mara tu baada ya kuoana miaka michache mbele ukaanza kuona mabadiliko.
Ngoja nikwambie, huyo hajabadilika, amekuwa original. Haiwezekani awe mzuri kwa kamuda kafupi tu wakati anakutafuta halafu gafla kakupata anabadilika, huyo alikuwa kimeo bin mkangafu miaka yote ila kwasababu alikuwa na kiu na wewe aliamua kutoa gamba kama cobra, ili umwone ni malaika Gabriel kumbe nyoka aitwaye Lusifa, alishika ndoano maana alikuwa anataka samaki, leo anaona ameshamvua samaki ndoano ya nini tena?.
Sasa kama na wewe uliingia kwa kukurupuka ukidhani unaelekea Yerusalemu, ukafumba macho yote usisikie cha kuambiwa sasa leo ngoma imerudi kuwa original, hiyo ndio ile uliyoikiri kuwa NITAMPENDA, NITAMLINDA HADI KIFO KITUTENGANISHE.
Usipoangalia utamwomba Mungu akuletee kifo.