Yupi ni Golikipa Bora kwa Sasa Duniani?

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
Baada ya juzi golikipa Gianluigi Buffon kuweka rekodi mpya ndani ya Serie A ( Ligi Kuu ya Italy) ya kucheza dakika 974 bila kuruhusu wavu wake kuguswa, wengi wameanza kumpa sifa ya kuwa anastahili kuwa golikipa bora kwa sasa duniani.

Lakini ubora mdogo wa timu pinzani katika ligi ya Serie A inaweza kuwa sababu ya Juventus na akina Buffon kuendelea kung'aa japo sikatai Buffon anajua sana katika umri wake wa miaka 38 bado anaendelea kuonyesha umahiri wake langoni.

Bila kuonyesha mapenzi au ushabiki, kwa sasa ni kipa yupi ni bora zaidi duniani kati ya hawa
wafuatao?
1. Gianluigi Buffon - Juventus
2. Thibaut Courtous - Chelsea
3. Manuel Neuer - Bayern Munich
4. David De Gea - Man Utd
5. Jan Oblak - Atletico
 
Kama kawaida uzi unaeleaelea tu ila nikianza kuchangia wenye chuk wataanza BRAVO huyu ndiye golikipa bora kabisaaa duniani
 
Keylor Navas. He is underrated, but the truth he's the best of all mentioned above.

485755180-goalkeeper-keylor-navas-of-real-madrid-in-gettyimages.jpg
 
Manuel Neuer ndio bora kwa sasa. Hata kwenye fifro iliyotolewa mwezi january yeye ndio kachaguliwa kusimama golini.

Pili huwezi kuwa kipa bora then ukacheza vilabu vya ajabu. Hao uliowataja hapo juu wote wanaonekana wazuri kutegemeana na aina ya uchezaji wa mabeki. Kwa mfano kwenye ligi tano bara barani ulaya yaani, laliga, epl, serieA, Bundesliga na ligi1 Oblak wa Atletico de Madrid ndio amefugwa magoli machache kuliko makipa woooote wanaocheza vilabu vikubwa huko ulaya.
 
Msimu huu Hugo Lloris amekua wakawaida sana..Jack Butland amesima sana zaidi epl season hii...Lakini kwa ubora na kila siku namshangaa ni huyu De Gea...definately Fergie's last greatest signing..Ok pia kuna Donarruma , dogo miaka 16 lakini ndo kipa number 1 wa AC Milan kwa sasa, Dogo katisha sana msimu huu...lastly ni huyu jamaa tunamuita the Beast..Jan Oblak...Strong Mentions pia kwa Petr Cech..Kevin Trapp pia, ameweza kusimama na kumuweka Sirugu bench..Keylor Navas nae dah..! lakn Mignollet ndo the biggest disappointment na Cassilas huko Porto
 
Back
Top Bottom