Nafikiria kuwasiliana na wale jamaa wa Redio Habari Maalum, hope wanaweza kuwa na kanda za huyu mtumishi. Watu bwana na huduma zao. Nikipata habari zake ama nyimbo zake nitakujulisha mkuu.
Nimeongea na jamaa wa Redio Habari Maalum. Kwa haraka hawakuweza kunipa jibu, ila wamenishauri kuwaandikia email wanisaidie kufanya utafiti maabarani kwao. Nikipata jibu jema nitakujulisha.
Ina sikitisha sana kumpoteza ndugu yetu kwenye ulingo wa nyimbo za injili. nina kanda moja hapa huwa inanifikisha mbali sana. " NI HERI UAMINI YA KWAMBA MUNGU YUPO NA USIMKUTE KULIKO KUTOKUAMINI NA UKAMKUTA". HATA NYIMBO ZAKE KWA YEYOTE ALIYE NAZO ATUTUPIE KWENYE MTANDAO INAWEZA KUTUFARIJI SANA
Rehema ni yake......imba kwa sauti ya Timothy, nilipata taarifa kwamba yuko Dodoma au mpwampwa nadhani, kilichonisikitisha Timothy alishaacha uimbaji amekuwa mtu wa mataifa
Rehema ni yake......imba kwa sauti ya Timothy, nilipata taarifa kwamba yuko Dodoma au mpwampwa nadhani, kilichonisikitisha Timothy alishaacha uimbaji amekuwa mtu wa mataifa
Hii post najua ni ya zamani kidogo. Nimekuwa nikitafuta habari za Timothy Ngw'inamila au nyimbo zake pia. Nimefanikiwa kupata nyimbo zake hapa: Timothy Ngw Inamila unaweza kudownload pia. Barikiwa sana!

Jamani kwa wapenzi wa nyimbo za injili jina la Timothy Ngw'inamila si geni masikioni mwao. Huyu mtu alikuwa maarufu sana kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za injili hadi miaka ya 90. Hivi sasa hasikiki kabisa. Je kuna mtu ana taarifa za aliko?