Yuko wapi Timothy Ng'winamila?

Nafikiria kuwasiliana na wale jamaa wa Redio Habari Maalum, hope wanaweza kuwa na kanda za huyu mtumishi. Watu bwana na huduma zao. Nikipata habari zake ama nyimbo zake nitakujulisha mkuu.
Jamaa si alikuwa anarekodia kenya? Kasha la mwana mpotevu linaonesha address za nairobi, na nilijua ni mkenya
 
rmashauri, et al

Nimeongea na jamaa wa Redio Habari Maalum. Kwa haraka hawakuweza kunipa jibu, ila wamenishauri kuwaandikia email wanisaidie kufanya utafiti maabarani kwao. Nikipata jibu jema nitakujulisha.

Shalom.
Ulipata jibu lolote mkuu? Nina usongo na nyimbo zake jamani
 
Ina sikitisha sana kumpoteza ndugu yetu kwenye ulingo wa nyimbo za injili. nina kanda moja hapa huwa inanifikisha mbali sana. " NI HERI UAMINI YA KWAMBA MUNGU YUPO NA USIMKUTE KULIKO KUTOKUAMINI NA UKAMKUTA". HATA NYIMBO ZAKE KWA YEYOTE ALIYE NAZO ATUTUPIE KWENYE MTANDAO INAWEZA KUTUFARIJI SANA
Jamani, kama ulipata nishirikishe
 
Rehema ni yake......imba kwa sauti ya Timothy, nilipata taarifa kwamba yuko Dodoma au mpwampwa nadhani, kilichonisikitisha Timothy alishaacha uimbaji amekuwa mtu wa mataifa
God forbid!!!
 
Rehema ni yake......imba kwa sauti ya Timothy, nilipata taarifa kwamba yuko Dodoma au mpwampwa nadhani, kilichonisikitisha Timothy alishaacha uimbaji amekuwa mtu wa mataifa
Kwa sasa yuko wapi?
 
Hii post najua ni ya zamani kidogo. Nimekuwa nikitafuta habari za Timothy Ngw'inamila au nyimbo zake pia. Nimefanikiwa kupata nyimbo zake hapa: Timothy Ngw Inamila unaweza kudownload pia. Barikiwa sana!
Mkuu aksante sana, nyimbo nilizozimis hatimaye nimezipata.

Mwanzoni nilipofungua kwa kutumia tube mate, ilinipeleka kubaya, ila nimetumia opera mambo safi.

Umeniongezea na album ambazo sikuwa nazo
 
Jamani kwa wapenzi wa nyimbo za injili jina la Timothy Ngw'inamila si geni masikioni mwao. Huyu mtu alikuwa maarufu sana kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za injili hadi miaka ya 90. Hivi sasa hasikiki kabisa. Je kuna mtu ana taarifa za aliko?
Hii nyimbo yake nilikuwa naikubali tokea enzi hizo na hadi sasa naikubali. Ndiyo maana nimeichagua miongoni mwa audio zake niitume tuburudike sote.
 

Attachments

  • Jifunze-kusameha.mp3
    9.2 MB · Views: 17
Hii nyimbo yake nilikuwa naikubali tokea enzi hizo na hadi sasa naikubali. Ndiyo maana nimeichagua miongoni mwa audio zake niitume tuburudike sote.
Mtu akipata nafasi ya kwenda AICT Butimba amuulizie Ibra,ukimpata Ibra habari za waimbaji hao wote nafikiri mtazipata.
 
Back
Top Bottom