IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
- Thread starter
-
- #21
Nakubalina na wewe kabisa. Hii amani tunayodanganyiwa ndiyo inayotuponza na tunachezewa kama watoto wadogo. Tusipochagua kuingia mitaani na baadhi yetu kuwa tayari kutolewa kafara hatuendi popote na ni vyema tukakaa kimya tu na kwaacha mafisadi watese.
Noamba wanaharakati waunganishe watu waingie barabarani, huu ndio ukombozi uliobakia kwa mtanzania. Tusiangalie sana nani atakuwa Raila wetu, maadam sasa hayupo tuanze tu kidogo kidogo kisha material condition itatupatia mtu, awe anatoka CCM ama kwingineko hatutajali sana.
Amkeni watanzania, haki kamwe haipatikani kwenye sahani, haki inapiganiwa.
Susuviri,
Nakushuru kwa kuchangia hoja iliyoko mbele yetu, swali langu nini kifanyike ili tumpate mkombozi wa taifa hili? najua wapo watu wema wenye uchungu na taifa hili, najua wapo wanaokesha kuliombea taifa hili, natambua kuwa tupo tunaoteswa na mafisadi najua.
Hebu watu kama akina ,MALANDO, TAMBWE HIZA, KABULU, MWAKYEMBE, OLE SENDEKA, MAMAKILANGONA na wengine wengi wenye uchungu na taifa hili ni kwanini wasikisaliti chama hiki cha CCM? ni kwa nini wasitukomboe? ni kweli kwamba huku kwenye upinzani(viongozi) hatuna mtu mathubuti wa kututetea na wale wachache wanaothubutu hawana nafasi katika vyama vyao, wanabaki kuwa wabunge na si vinginevyo.
IsayaMwita, USITAFUTE MKOMBOZI! Jikomboe. That is my message.
Raila Odinga is not a hero to everyone, kwa other Kenyans he is the deivl personified. Kwa hiyo usitake kutafuta mtu mmoja. Angalia dynamics and the environment. Tujenge pamoja taifa inayofuata sheria na inayofuata misingi ya haki za binadamu.
Hatutampata Raila Odinga au Obama au whoever tunamtafuta, because tunahitaji weneywe kufanya mabadiliko then a leader will eventually arise ambaye atatusikiliza sisi na kutusaidia kujenga. Usitake mtu aibuke na aje na mawazo how to do it. Watanzania sisi siyo watoto ni watu wazima, we are thinking people and we know what we want nd what to do. Tatizo viongozi wetu wamekuwa wakitu-treat kama watoto wadogo.
Susuviri;
Tunapoongelea mtu anayeweza kufanya mabadailiko ndani ya taifa letu, hasa hulenga wale viongozi wenye mitizamo chanya, napenda kukuuliza swali kidogo tu, hebu mtu kama wewe wawezaje kujikomboa(kisiasa)? usisahau kuwa hata diwani wako hakujui, sasa wawezaje kujikomboa? ndipo nikabainisha kuwa kuna kila haja ya kuwa watu(viongozi) wanaoweza kutukomboa na si vinginevyo,
Nadhani uongozi na fikra zenye tija katika jamii zinahitajika, sitegemei mtu yeyote kusimama na kuweza kujikomboa hasa kisiasa, ni ngumu kama nikel, tuwe na mwelekeo na kuendelea kuwashawishi wale tunaodhani kuwa wakisimama na CCM wataleta changamoto na si vinginevyo.
Isayamwita,
Obama alikuwa nani miaka mitano iliyopita na sasa yuko wapi? Mtu kama Zitto alikuwa nani miaka mitano iliyopita na sasa yuko wapi?
Timiza wajibu wako na kuna siku Tanzania itakuja pata kiongozi wa maana.
Viongozi hawatoki mbinguni, tunao kila siku. Mazingira ndiyo yanawafanya wengine wafanikiwe kuwa viongozi bora wakati wengine wanaporomoka. Endelea kujenga mazingira bora ambayo ni kujituma, kufuata sheria na haki.
Kwa mazingira ya sasa ya Tanzania, hata tukimpata Odinga wa TZ, hatafanikiwa maana atatimuliwa na kupotea baada ya muda mfupi. Ukisoma kashfa na matusi wanayopokea watu kama akina Mrema hapa JF, juwa sisi wananchi bado hatujawa tayari kuwaunga mkono watu ambao wamejitolea maisha yao kupigania haki. Hata Odinga sawa na Mrema, ana makosa yake mengi tu, ila Wakenya wamemkubali kwasababu wanajua pamoja na makosa yake kama binadamu lakini muda wote kajitolea kusaidia kuleta ukombozi wa kweli wa Kenya.
Mazingira ya siasa za Kenya na Tanzania ni tofauti sana.
IsayaMwita, USITAFUTE MKOMBOZI! Jikomboe. That is my message.
Raila Odinga is not a hero to everyone, kwa other Kenyans he is the deivl personified. Kwa hiyo usitake kutafuta mtu mmoja. Angalia dynamics and the environment. Tujenge pamoja taifa inayofuata sheria na inayofuata misingi ya haki za binadamu.
Hatutampata Raila Odinga au Obama au whoever tunamtafuta, because tunahitaji weneywe kufanya mabadiliko then a leader will eventually arise ambaye atatusikiliza sisi na kutusaidia kujenga. Usitake mtu aibuke na aje na mawazo how to do it. Watanzania sisi siyo watoto ni watu wazima, we are thinking people and we know what we want nd what to do. Tatizo viongozi wetu wamekuwa wakitu-treat kama watoto wadogo.
Waswahili wanakwambia "Usione vinaelea, vimeumbwa". Hivi huyo Raila Odinga unaijua vilivyo "pedigree" yake kwa maana ya historia ya kisiasa ya familia yake au unamsikiaga tu? Unaambiwa Raila Odinga upinzani anao kwenye damu na aliupata tokea akinyonya ziwa la mamake kabla na baada ya Kenya kupata uhuru. Babake Oginga Odinga alikula sahani moja na Jomo Kenyatta wakati wa harakati za kupigania uhuru na alitokea kuwa mpinzani mkubwa wa Kenyatta na dhidi ya KANU na Moi baada ya Uhuru na kufariki kwa Kenyatta, akiwa kama sauti na mwakilishi wa kabila la Waluo dhidi ya ukiritimba wa na Wakikuyu kwenye nyanja za siasa na utawala. Kwa mantiki hiyo, sidhani kama kuna mtu hata mmoja Tanzania ya leo unayeweza kumlinganisha naye.
Njabu Tha Dude;
Mkuu hakika acha utani, hapa tunajadili hoja na si mzaa , kweli unataka utuambie kuwa hakuna mtu mwenye fikra njema kama za Raila hapa Tanzania? kweli sisi sote hatuna fikra za kimapinduzi kama za Raila? nadhani sisi fikra hizo tunazo ila uoga na upumbavu umetujaa na si vinginevyo,
Swali dogo naomba ulijibu hapa, je akina Slaa,Mwakyembe, anna kilango , na hata Zitto si mfono wa Raila?
Naona hapo kwa kiasi kikubwa ushajijibu mwenyewe. Tatizo si kukosekana "fikra za kimapinduzi", bali ni historia ya kisiasa ya nchi haichangii kuleta kiongozi wa upinzani mwenye wasifu aliyonao Raila. Hao uliowataja kwa pekee yao hawana mvuto mkubwa wa kisiasa kama aliyonao Raila na sidhani kama wanaweza kupata mamilioni ya wafuasi waliyo tayari kumwaga damu ikiwezekana kutetea haki zao.
Mwiba: huyo Dude achana naye anapenda sana kuponda wenzake lakini hana point. Kwa kusema eti Odinga amenyonya katika ziwa la mamake upinzani ni uvivu wa kufikiri na kuonyesha haelewi swali.
Odinga is not a 'pedigree' or golden boy or someone special. He is someone who grabbed the opportunity that presented itself. He was intelligent enough to realize it. Tanzania tusitake kupata Messiah wa kutukomboa. Huyu Dude anataka kutukatisha tamaa, but I tell you we don't need Odingas in Tanzania, we need the right opportunity and good timing. Unafikiri all people ambao wako CCM kama akina Mwakyembe are happy? No!! But currently they see no option. It is a mentality problem nothing more. Odinga took a gamble and he did loose in one or another just like Kenya also suffered, lakini they were ready to sacrifice. Je, watanzania tuko tayari kusema liwe vyovyote vile hata ikibidi kuwa na vita lakini hatukubali hali hii? NO WAY!! Until we reach that point of real desperation, don't look for outsider to come and help but help yourself. There's no Messiah waiting to be born, we are all the ones who can make change.
Isayamwita umeleta hoja nzuri, good job!
Naona umesahau kwamba binadamu wote kwa asili wamezaliwa na "herd mentality". Bila ya kuwa na kiongozi jamii ya binadamu haiwezi kupata maendeleo yoyote ya maana. Umepoteza muda mwingi sana kuwajadili na kuwachambua Clinton, Obama na McCain, kwa nini? Mbona hukuishia kuandika waraka au kuhubiri injili yako ya jinsi Mmarekani wa kawaida anavyoweza "kuijkomboa" mwenyewe bila ya kuwategemea hao viongozi vinara wanaowania Urais?
Njabu Tha Dude;
Kwa kuwa sisi watanzania hatuna tamaduni za kujitolea muanga, ila ninachodhani kama tunaweza kujijenga na kujiamini sisi kwanza(wafuasi) hakika zile nidhamu za uoga zinaweza kututoka, tuna watu wa kutolea mifano, watu toka Mara ni watu wa mfano huo, tunaamini hata watu toka kigoma pia wanaweza kuwa na mfano huo,.
Kuhusu hawa Viongozi tulionao wanaweza kusimama kama tutawaunga mkono, Mtu kama Slaa, akipata support anaweza kufanya kitu na jamii ya kitanzania ikapona na hii mikono ya mafisadi, ama wewe unaonaje?
Tatizo lililopo hapo ni kwamba Katika inchi yetu hairuhusu mgombea (binafsi)huru, na kama ndiyo hivyo je pale CHADEMA Mbowe anaweza kupisha uwenyekiti ili tumuweke mtu mfano wa Raila? hapo mnapaonaje?
...........raila has explenary record and history..hapa nyumbani hakuna ..kwani wapuinzani wengi wa nyerere kama kambona.,mtemvus,kunambis ets ..walikuwa seized kisiasa na wala hawajaproduce offsprings wakali kisiasa...tanzania hakuna strong political family ninayoona zaidi ya karume na ali hassan mwinyi....nyereres hawafurukuti labda tungojee kizazi chao cha pili..hiki cha kwanza cha kina makongoro ..hakifurukuti unlike karume,mwinyi,kenyattas,railas ets....
ila tanzania kuna mwanasiasa kama JOHN POMBE MAGUFURI huyu ni admirer wa raila...na hopeful siku moja atafika mbali.....
issayamwita
Nadhani hili la ukabila ni kati ya socio-political dynamics ambazo zinafanya siasa za Kenya zitofautiane kimsingi na za Tanzania. Raila political base yake kubwa ni Waluo na Waluhya ambao kihistoria wamekuwa na upinzani mkubwa wa kisiasa na Wakikuyu. Tanzania haina siasa za ukabila, na ndiyo ndiyo maana wanasiasa kama Slaa na Zitto kamwe hawawezi kupata ufuasi kama aliyonao Raila. Labda kwa kiasi fulani Mpemba Seif Hamad jinsi alivyoiweka Pemba yote chini ya miguu yake kisiasa kila wakati wa Uchaguzi mkuu, lakini tatizo ni kwamba hana broad appeal inayojumuisha Wapiga Kura ndani na nje ya Visiwani. Hiyo ndiyo challenge kubwa ya siasa za ukabila.
phillemon mikael
Mbona umekata tamaa namna hii Mkuu? mbona hauna matumaini ya kuishi? umewahi kufika Mara? umewahi kufika Tarime? nenda leo kaone, njoo uone mkuu wangu, uone kuwa hauruhusiwi kuvaa yale maguo ya kijani(CCM) sasa kama tungekuwa tumeanzisha fikra kama hizi katika mikoa kama 5 tungeweza kuleta mabadiliko,
phillemon mikael ni lazima tuwe na fikra za kiukombozi, acha kudhani kuwa CCM ndiyo kila kitu, na hatuwezi kuteswa na hawa mafisadi, tutafurukuta hadi mwisho, tunasema maisha yetu kwa sasa yatakuja mikonnoni mwa mafisadi, kufa kwetu sawa tu.
phillemon mikael kama mtu atashindwa kufanya mageuzi ya kweli hakika Tanzania Mpya haipo, lakini kama sisi sote tutaunganisha nguvu zetu kwa pamoja ukombozi wetu uko karibu,
phillemon mikael naomba ujiulize nini hatima yetu katika Taifa letu, nini hatima ya watoto wetu kama kila kitu mafisadi wanagawana?
issaya mwita...saluuti kamanda ..heshima mbele mkuu..unajua hadi leo najiulizaga zile asilimia 80 kiwete aliaipataga wapi wakati kuna mikoa kama ...mara,kigoma,mbeya .,iringa,kilimanjaro...est ambayo ina msimamo mkali...mimi naamini kwa miaka ya sasa hata mgombea ccm awe mzuri vipi ni vigumu kupata asilimia 80 kama hakuiba kura...ushindi wa asilimia 65 hadi 70 ndio likely kwa mgombea mwenye mass support kwa hali ya upinzani ilivyo.....nadhani kadiri uelewa wa wananchi unavyoongezeka tutarudi kwenye mass support ya asilimia 40 to 45 kwa wapinzani mwaka 2010...nadhani mwaka 1995 tulikuwa na ratio ya 60:40.....
hali ya wapinzani kutoelewana ilielekea kupandikizwa na ccm ndiyo iliyoangusha nguvu kubwa waliyoanza nayo..mwaka 1995...wakati mrema alipokuwa na nguvu ya kuangusha mawee..
nafurahi kusikia nguvu ya uelewa ya wananchi wa mara...mara zote napenda hawa ndugu zangu kwani sio wanafiki ...ukianzia kwa mwalimu..pale alipoamua kumpigia chapuo paul ndobbo .baada ya ccm kuweka mgombea mbovu......sasa nguvu ya wana mara inabidi tuione tarime...
issa hali ikoje tarime ???...nasikia ccm wanajipanga kushinda ...hasa kutokana na propaganda za kugombanisha umoja wa wapinzani ambazo inaonekana wanaelekea kufanikiwa......
phillemon mikael;
mkuu acha vituko, subiri uone awamu hii hapa tarime tunaweza kuwaletea mwandishi wa habari kule bungeni, naye si mwingine anaweza akawa kichele nyaronyo kama atapitishwa, sisi wanamara letu moja tu, unafiki kwetu mwiko na tutamtuma aje kutetea maslahi yetu na si vinginevyo.
Phillemon mikael; tunajua sisi wana mara ndiyo chachu ya siasa hizi za tanzania hii, mwalimu alionyesha njia na sisi tunafuata, tutaweza kama mtatuunga mkono
phillemon mikael; sisi sote tunaamini nchii ni yetu sote hakuna hata mmoja wetu anayestahili zaidi kuliko mwingine, nadhani sasa sisi wana jf tuamke sote tuwaelimishe ndugu zetu kule vijijini tunakotoka.
Phillemon mikael; kazi hiyo hapa tarime tumeimaliza, sasa tunaelekeza nguvu zetu msoma mjini na mwisho mwanza na kwingineko.
Swali hili usilikwepe wewe kama wewe umeweza kuielimisha jamii unayotoka? Jaribu sasa kuielimisha jamii yako mkuu na hapo ndipo tutajikwamua na hawa mafisadi.
..nyoronyo kicheere huyu mpiganaji namkubali kwa sana.....kuna wakati walikuwa na mombare matinyi ofisi ikiwa ya majira pale karibu na club ya yanga...wakiwa pia na kiona mbali[conrad..]..it was a great team.....nilikuwa mara moja moja napeleka makalas....mara moja moja sana ....walikwa wakilipa kama sikosei tzs 10,000 miaka ya mwanzo ya 90...
Isaya,
Mimi namuona Raila kama msaliti wa wananchi ambaye yuko tayari kufanya chochote for personal gains. Alipojiunga na Moi KANU ilikuwa ile ile ambayo alikuwa akipingana nayo siku zote lakini kwa kuwa alikuwa anapewa uwaziri ikawa OK. It is very unfortunate that ukabila Kenya umeota mizizi to the extent that Raila will always have people who rally behind him regardless of what he does. Tunao kina Raila wetu Tanzania na hilo ni moja ya mambo yanayoniumiza sana. Can you imagine kuwa Mrema na mapungufu yake yote mpaka leo hii bado ana wafuasi?