Yuko wapi Raila Odinga wa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yuko wapi Raila Odinga wa Tanzania?

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by IsayaMwita, Aug 29, 2008.

 1. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikijiuliza maswali lukuki, wako wapi watanzania(wapiganaji) wanaoweza kutukwamua hapa tulipo? tumekwama, hatuna mwelekeo, wale tuliowaamini nao wameingia MITINI
  Maswali ya kujiuliza:

  (a) je ni kweli hatuna watu wazalendo kama akina Odinga wa pale Kenya?

  (b) Ni nini mtizamo wa vyama vya upinzani siku za usoni hapa Tanzania?

  (C) Dhamana ya demokrasia hii CHANGA Iko mikononi mwa nani kwa sasa?

  Wana JF naomba tutafakari ni nani mkombozi wa taifa letu hili kwa siku za usoni? je yawezekana akatoka ndani ya CCM? ama anaweza akatoka ndani ya vyama vya upinzani?
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyo mtu anaweza kuwa wewe au mimi!We can make the change if we want too.If we are all in need of change it is us to make the change and not other people!
  Got it doug!
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ndiyo, Raila alitoka upinzani akajiunga na Moi, akatoka tena kwa Moi akajiunga na Kibaki. Alipoachana na Kibaki watu kwa mamia wakapoteza maisha baada ya uchaguzi. Nadhani ni debatable kama hama hama yake ilikuwa in the best interest of kenyans. It is my considered opinion that we have thousands of Ogingas in Tanzania, we only need to think if we really need them.
   
 4. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kevo,

  Lakini kevo nchi hii bado kuna tatizo unaweza kuona kama watanzania wamehamasika na kuelekeza hisia zao kipinzani lakini siku ya siku unakuta jamaa wameshinda sijui inakuaje
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sasa kumbe umeshatambua tatizo lilipo ehhhh!Dawa ni kulitibu tuu basi!Kujiuliza kwa nini wanashinda?Je wanaiba kura,au tunaonekana wapinzani kwa nje ila siku za uchaguzi tunaishia kuwapigia kura?ama tumekosa elimu maridhawa kuhusiana na siasa?ama sisi wenyewe ndio tumejipa likizo ya kufikiri?
   
 6. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  gagnija,

  Wewe unashauri nani tumpeleke kule ndani ya CCM, ili ang'oke na wanachama wa kutosha ndani ya ccm? ama ndiyo tayari yumo, ila inawezekana kama Tambwe hiza, Kabulu wanaweza kulejea katika vyama vyao, ama ninyi mnaonaje?
   
 7. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Isaya,

  Mimi namuona Raila kama msaliti wa wananchi ambaye yuko tayari kufanya chochote for personal gains. Alipojiunga na Moi KANU ilikuwa ile ile ambayo alikuwa akipingana nayo siku zote lakini kwa kuwa alikuwa anapewa uwaziri ikawa OK. It is very unfortunate that ukabila Kenya umeota mizizi to the extent that Raila will always have people who rally behind him regardless of what he does. Tunao kina Raila wetu Tanzania na hilo ni moja ya mambo yanayoniumiza sana. Can you imagine kuwa Mrema na mapungufu yake yote mpaka leo hii bado ana wafuasi?
   
 8. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  gagnija;

  Utakuwa umekosea sana tena sana kumuita Raila Msaliti wa wananchi wa Kenya, tambua kuwa Raila wakati anajiunga na KANU hakupewa uwaziri bali alipewa nafasi ya katibu wa chama ambacho kilikuwa kimeungana na Ford Kenya, nadhani hii ilikuwa ni janja ya kukimaliza chama cha KANU. Tazama muda ulipotimu ndipo akang'oka na wabunge wengi wa kanu pamoja na mawaziri wa KANU.

  Bado sijakupata hata kidogo unapomulinganisha Raila na Mrema, kwani mrema hakika ameididimiza demokrasia yetu kwa kipindi kirefu, hakua tayari kushaurika, alikuwa mbabe na hata mwishoe akajikuta amepoteza mwelekeo, haitoshi mrema hakusoma nyakati.

  Bado tunahitaji akina Raila katika nchii hii, bado najiuliza ni nani Raila wa nchi hii?
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Gagnija,

  With this kind of thinking kama yako si ajabu inakuwa taabu kumpata shujaa kama Odinga hapa nchini. Akitokea moja akaanza kuichachafya CCM, sisi hao hao tutamwita majina mengi tu kama mroho wa madaraka tukiongozwa na hao hao ambao wamekuwa madarakani miaka nenda rudi. Tutaanza kumuona kama mtishia maendeleo kama siku zote tukiitikia wimbo wa mafisadi wa CCM wakiongozwa na mizee kama Kingunge. Tutatafuta kila sifa ya ubaya dhidi yake kwa kisingizio cha amani na utulivu bila kujua tunazidi kuwakumbatia hao hao mafisadi wakiongozwa na mkuu wa kaya.

  Nakuomba uijue kwanza historia ya watu kama Raila Odinga kabla hujakurupuka kwa kuwapa lawama za kipuuzi kama unavyojaribu kuelezea. Alikuwa tayari kuachia hata Uwaziri kwa kutokubaliana na Raisi wake. Na sasa kama Waziri Mkuu amem"overshadow" Rais Kibaki kiasi cha kuonekana anaendesha serikali kwa sababu ni mtu wa vitendo. Imefika mahali Raisi Kibaki anakaa pembeni kama mtazamaji akiangalia mwanamume anavyotimiza wajibu. Raila Odinga siyo "yes man" - hakuwa kwa Moi na siyo kwa Kibaki.

  Adui wetu mkubwa Tanzania kwa sasa si MAFISADI wala CCM wala JK - ni sisi wenyewe wananchi kwa kuridhia hiyo hali. Tunafikiri tukikaa kama watazamaji huo ukombozi utakuja kama "MANNA" kutoka mbinguni. Uovu tunatembea nao, tunalala nao na kuukumbatia, tunausujudu na kuusifia na tumeufanya sehemu muhimu ya maisha yetu. Sasa akitokea mtu kama Odinga sina shaka hatutamkubali kwa sababu tumeshachagua upande wa unyenyekevu - hatutaki vurugu. Watanzania ndivyo tulivyo...............
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Watanzania wote ni akina Odinga, kinachotakiwa ni kuhakikisha wanafanya uchaguzi mzuri wa viongozi wao. hatima yetu ipo mikononi mwetu, iwapo tutaendelea kukubali kudanganywa kila siku kwa vijisenti, tutaendelea kuliwa. hatuna wa kumlaumu kwanza zaidi ya sisi wenyewe, halafu ndio tuwalaumu hao mafisadi
   
 11. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,658
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Waswahili wanakwambia "Usione vinaelea, vimeumbwa". Hivi huyo Raila Odinga unaijua vilivyo "pedigree" yake kwa maana ya historia ya kisiasa ya familia yake au unamsikiaga tu? Unaambiwa Raila Odinga upinzani anao kwenye damu na aliupata tokea akinyonya ziwa la mamake kabla na baada ya Kenya kupata uhuru. Babake Oginga Odinga alikula sahani moja na Jomo Kenyatta wakati wa harakati za kupigania uhuru na alitokea kuwa mpinzani mkubwa wa Kenyatta na dhidi ya KANU na Moi baada ya Uhuru na kufariki kwa Kenyatta, akiwa kama sauti na mwakilishi wa kabila la Waluo dhidi ya ukiritimba wa na Wakikuyu kwenye nyanja za siasa na utawala. Kwa mantiki hiyo, sidhani kama kuna mtu hata mmoja Tanzania ya leo unayeweza kumlinganisha naye.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mimi ningependekeza atokee mtu mmoja tu mwenye ushujaa kama wa Mpemba Seifu ni kiongozi ambae hajawahi kutokea katika Tanzania ,ni kiongozi ambae alimkabili Mwalimu Nyerere ndani ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wazungu wanasema face to face na kumwambia Zanzibar tutanunua mafuta sehemu yeyote tuitakayo akikusudia kulijibu suala la Zanzibar inunue mafuta kutoka Bara ,mwsisho Nyerere alibwaga manyanga na kumualika chai Chamwino kwenda kumpa mikoba.
  Kama hamfahamu Seifu amepewa Uchifu wa Wakurya na hadi hii leo ni kiongozi anaepewa heshima za juu anapotembelea anga za huko na wanamwamini kabisa ni mtu asiemuonea haya yeyote yule na anampa ukweli na kumwacha hoi ,haogopi kuambiwa amekosea adabu au ana dharau wakubwa kwani Seifu anaamini kabisa katika kutafuta maisha bora kwa kila raia ni lazima woga uwondolewe na kila anaekosea aambiwe kweupe hadharani na ndivyo anavyofanya ila tatizo la Seif hapendelei kuona mtu anauliwa kwa ajili ya siasa mambo ambayo kila mtu atapita na kuyaacha hapa hapa duniani yakijiendesha kivyake vyake.
  Ila akipatikana mtu dizaini za Odinga zikichanganyika na dizaini za mtu kama Seifu basi naamini kabisa uovu wa CCM ungelikuwa matatani.
   
 13. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,658
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wee tushakujua kuwa ni mdini na mkabila kwa maana ya kwamba una tabia ya kuwafagilia na kuwatetea Waislamu na Wapemba/Waunguja. Elewa kwamba huyo Seif Shariff Hamad unayemsifia si yule wa Shaaban Mloo na wenzake enzi zile za Nyerere/Abeid Jumbe wakati wa machafuko ya hali ya kisiasa Unguja na Pemba, kujiuzulu kwa Jumbe na hatimaye Mwinyi kupewa urais wa Zanzibar. Huyu ni career politician aliyeelewa na kutambua kwamba CCM haipingiki wala kushindika na anaye-enjoy full-pension benefits za Waziri kiongozi mstaafu huku wakati huohuo akijifanya yupo mstari wa mbele kama naibu kiongozi wa CUF.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unaonyesha una matatizo ya akili ,huna wazimu lakini ni mfinyu wa kupambanua na kuyaelewa mambo kwa undani halafu ukayakubali ,watu dizaini zenu ni wale ambao mnakumbwa na kufagiliwa na fagio la propaganda ,mnanunulika kirahisi kwa maneno ya kuchonga ,na yakishawaingia katika akili yako inakuwa ni itikadi kwa upande wako hivyo inamuwia vigumu mtu kukufahamisha kwani inakuwa tayari kasumba imeshajengeka.

  Kwa ulivyoleta mambo ya Jumbe na kuunganisha na Seifu ndipo nilipokubaini ni mtu unaekokotwa na propaganda pengine kama ungeendelea kuhubiri ungelisema Seifu anataka kuleta waarabu ,inaonyesha hujui siasa zinavyokwenda na unashindwa kuelewa maana ya watu kusema siasa ni mchezo mchafu.

  Halafu nimekugundua kuwa ni mchovu wa kufikiri kwa kung'ang'aniza mambo yalioibuka kisiasa ,unajua wakati wa vita kuna nyimbo nyingi zinazuka na vita ikimalizika ,na hizo nyimbo nazo husita ,ila wewe bado unaziimba wakati vita ilishakwisha sasa sijui kwa miaka hii tuliyonayo kama nyimbo za wakati huo zitakusaidieni.

  Umemsikia Muhunzi akisema anamtambua karume kama Raisi wa Unguja ,hivyo wewe kama mfuatiliaji na mtu unaweza kufikiri ,ulitakiwa ujue hiyo ni nyimbo ya vita nyengine imeanza ile ya kutomtambua Raisi imeshapitwa na wakati.

  Using'ang'anie mbona walisema hawamtambui ? ndio mfano wako unaleta mambo ya Jumbe ,ndugu elewa kuwa watu hawazungumzii somo la historia hapa kuna siasa ambayo inabadilika kwa nyakati.
  Jaribu kutafuta hoja nyengine mpya kabisa za Jumbe hazitokusaidia kitu ,kwani haiwezi leo tukaingia vitani na Kenya tukamwita Kibaki nduli bali tutamtafutia jina jingine jipya linaloendana na wakati ,si umiona wahujumu uchumi sasa wanaitwa mafisadi ? yaani nakushangaa sana unaleta mambo ya Jumbe na Seifu na uarabu na udini au ualkaeda yaani nyimbo za uchaguzi za mwaka juzi na zaidi unakuja kuhadithia leo.Ndio nyie nyie mnaokazania Zanzibar wana historia ya mipasuko ,ila kumbuka tu siasa ya vyama vingi ilianza Zanzibar kuliko Tanganyika ,hivyo kwenye vyama vingi hakuachi mipasuko ,seuze ndani ya chama kimoja si tunaiyona CCM si imejaa mipasuko ambayo ukitazama unaona mpaka ndani.
   
 15. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,658
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Yakhee, huyo Seif Sharif Hamad ambaye ndiye pendekezo lako la Mwanasiasa anayemkaribia Raila Odinga kwa umahiri wa siasa za upinzania ana-enjoy mafaa kamili na yote ya pensheni ya Waziri Kiongozi wa Zanzibar hivi leo kulingana na sheria za serikali ya CCM (ambapo hadi hivi sasa ni Seif Sharif Hamad na Edward Lowassa pekee yao wenye hadhi pekee kama hiyo) huku wakati huohuo akijifanya ni mpinzani nambari moja wa CCM inayomsitiri kiuchumi kupitia pensheni na ruzuku kubwa. Sasa wapi kwa wapi yakhee? Hata mtoto wa darasa la tatu atang'amua hapa kuna jambo fulani si sawa!?
   
 16. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mwiba: huyo Dude achana naye anapenda sana kuponda wenzake lakini hana point. Kwa kusema eti Odinga amenyonya katika ziwa la mamake upinzani ni uvivu wa kufikiri na kuonyesha haelewi swali.
  Odinga is not a 'pedigree' or golden boy or someone special. He is someone who grabbed the opportunity that presented itself. He was intelligent enough to realize it. Tanzania tusitake kupata Messiah wa kutukomboa. Huyu Dude anataka kutukatisha tamaa, but I tell you we don't need Odingas in Tanzania, we need the right opportunity and good timing. Unafikiri all people ambao wako CCM kama akina Mwakyembe are happy? No!! But currently they see no option. It is a mentality problem nothing more. Odinga took a gamble and he did loose in one or another just like Kenya also suffered, lakini they were ready to sacrifice. Je, watanzania tuko tayari kusema liwe vyovyote vile hata ikibidi kuwa na vita lakini hatukubali hali hii? NO WAY!! Until we reach that point of real desperation, don't look for outsider to come and help but help yourself. There's no Messiah waiting to be born, we are all the ones who can make change.
  Isayamwita umeleta hoja nzuri, good job!
   
 17. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,658
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wewe nadhani umekimbilia kunipinga tu kwa sababu zako binafsi bila kufahamu au kutafakari vizuri unachoandika. Kenya siyo Tanzania mjomba, na there's no way Myakwembe can in any meaningful be compared or contrasted to Rala Odinga. Hakuna mtu alimyemjua Mwakyembe kabla ya kumaliza jukumu la kuongoza tume ya sakata la Richmond na bunge lilotawaliwa na chama chake cha CCM, wakati kwa Raila jadi ya siasa za upinzani alizaliwa na kukulia nazo. Kwa kifupi: kwa Tanzania ya sasa (arguably hata ile iloyopita ya enzi za Nyerere), hakuna political, social, ethnic na personal (in the sense of family) dynamics zinazoweza kuleta upinzania wa nguvu, machafuko na mapinduzi ya kisiasa kama ilivyotokea Kenya mwanzoni mwa 2008. Vitu havitokei tu bila sababu, umeelewa?
   
 18. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Njabu Tha Dude;

  Napenda kuwauliza ndugu zangu watanzania, hebu sisi watanzania mbona hatujampata mtetezi wa kweli? Mbona hatuna mitazamo mizuri na mstakabali mzuri wa siku za usoni? Ni nani sasa kimbilio letu kwa sasa? ni nani atakayeleta upinzani 2010 na CCM? ni nani jamani?

  Nadhani sisi tutabaki wasindizaji siku zote maneno mengi bila tija, huku tukiwasindikiza CCM, najiuliza watu kama MWANAKIJIJI, PUNDIT, JMUSH1, Mbona hamtaki kurudi nyumbani tupigane na hawa mafisadi wanaoiuza nchi yetu? mmebaki kudurusu hapa jamnvini huku mkisahau wanaofika ni wachache tu. lakini tunaendelea hata kukupongeza MWKJJ KWA KAJALIDA KA CHECHE, umeonyesha njia.

  Tupo kama MISUKULE(WATANZANIA), tuliokatwa ndimi, hata kutoa ishara ni kazi kwetu,NI NANI ATAKEYETUOKOA NA MIKONO YA HAWA MAFISADI?

  Tunawapongeza wale wachache wanaothubutu, watu kama SLAA, ZITOO NA wengine, hakika mungu awatetee, siku moja mtaingizwa ndani ya kitabu cha kumbukumbu, haijalishi hata kama maisha yenu yako hatarini.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 19. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Susuviri,

  Nakushuru kwa kuchangia hoja iliyoko mbele yetu, swali langu nini kifanyike ili tumpate mkombozi wa taifa hili? najua wapo watu wema wenye uchungu na taifa hili, najua wapo wanaokesha kuliombea taifa hili, natambua kuwa tupo tunaoteswa na mafisadi najua.

  Hebu watu kama akina ,MALANDO, TAMBWE HIZA, KABULU, MWAKYEMBE, OLE SENDEKA, MAMAKILANGONA na wengine wengi wenye uchungu na taifa hili ni kwanini wasikisaliti chama hiki cha CCM? ni kwa nini wasitukomboe? ni kweli kwamba huku kwenye upinzani(viongozi) hatuna mtu mathubuti wa kututetea na wale wachache wanaothubutu hawana nafasi katika vyama vyao, wanabaki kuwa wabunge na si vinginevyo.
   
 20. M

  Mavanza Member

  #20
  Aug 31, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubalina na wewe kabisa. Hii amani tunayodanganyiwa ndiyo inayotuponza na tunachezewa kama watoto wadogo. Tusipochagua kuingia mitaani na baadhi yetu kuwa tayari kutolewa kafara hatuendi popote na ni vyema tukakaa kimya tu na kwaacha mafisadi watese.

  Noamba wanaharakati waunganishe watu waingie barabarani, huu ndio ukombozi uliobakia kwa mtanzania. Tusiangalie sana nani atakuwa Raila wetu, maadam sasa hayupo tuanze tu kidogo kidogo kisha material condition itatupatia mtu, awe anatoka CCM ama kwingineko hatutajali sana.

  Amkeni watanzania, haki kamwe haipatikani kwenye sahani, haki inapiganiwa.
   
Loading...