Yuko Wapi Philip Mangula?

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Katika harakati za kukiokoa Chama Cha Mapinduzi ilionekana kuwa Philip Mangula na Abdalahman Kinana wangeweza kufaa. Mangula akaukwaa Umakamu wa Mwenyekiti. Lakini cha kushangaza mzee Mangula hasikiki kabisa. Au ameona siasa wazifanyazo akina Kinana, Nape na Mwigulu za kukimbizana na wapinzani siyo saizi yake?
 
Ameingia mitini, baada ya mkwara wake alioutoa wakati alipoukwaa umakamu Mwenyekiti kuwa katika kipindi cha miezi 6 ya uongozi wake, kuwa atahakikisha kila aliyepata uongozi ndani ya CCM kwa rushwa atamng'oa, hivi sasa ni zaidi ya mwaka tokea atoe mkwara huo mzito, hajafanikiwa kumng'oa hata mwanamagamba mmoja!!!
 
Katika harakati za kukiokoa Chama Cha Mapinduzi ilionekana kuwa Philip Mangula na Abdalahman Kinana wangeweza kufaa. Mangula akaukwaa Umakamu wa Mwenyekiti. Lakini cha kushangaza mzee Mangula hasikiki kabisa. Au ameona siasa wazifanyazo akina Kinana, Nape na Mwigulu za kukimbizana na wapinzani siyo saizi yake?

Mkuu, pengine dhamiri inamshitaki baada ya kugundua kwamba ahadi aliyoitoa pale mwanzo ya kuwashughulikia wote waliopata uongozi kwa rushwa haitekelezeki kwani kwa hilo ndani ya chama hakuna aliye "msafi" ukianzia na Mwenyekiti mwenyewe! Na "utu uzima wake" hakika unafiki wa kufanya siasa za kina Mwigulu & Nape, ingekuwa ni fedheha sana! Ni busara zaidi akajiepusha na majukwaa hayo!
 
Yule mzee amekutana na vijana wasiojua siasa ndani ya chama chake.. Wenye siasa za majitaka.. Naona anajuta kuukubali uteuzi wake..
 
Hakika nimeshangazwa Na ukimya mkubwa wa Mh.Mzee Philip Mangula.Mzee huyu amekuwa kimya kiasi ambacho imenilazimu nimtafute nijue nini kimemsibu Mzee wetu.Kikubwa nilitaka nimshauri akishauri chama chetu CCM kama kiruhusu mikutano ya hadhara ili tuweze kujipima kama wananchi wana imani Na chama chetu CCM.
 
Mzee anaheshima zake ndio maana amenyamaza si unaona hata Katibu Mkuu wake wa chama!! Matamko kawachia mavuvuzela kama kina Kigwangalla, nepi, kairuki, slow slow, na wanaomtafuta faru John!!!!!
 
Back
Top Bottom