Yuko wapi Nyaronyo Kicheere jamani

MKEHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
716
Reaction score
1,144
Nyaronyo Kicheere wakati huo akiandikia magazeti ya MAWIO na Mwana HALISI akinikosha sana kwa style yake ya uandishi akifikisha ujumbe kwa njia ya uchekeshaji wenye ukweli ndani yake .

Mwalimu huyo wa zamani huko Morogoro kwa sasa akiwa wanasheria akiandika kwa ku refer kabila lake la Kikurya. Aliandika mambo mengi sana ya kufurahisha.

Lakini si peke yake hata Mbwambo wa gazeti la RAIA MWEMA nae kapotea. Magazeti hayo yakiandika habari za kuvutia sana.

Kusema kweli siku hizi hata gazeti sinunui kwa sababu sioni wanacho kiandika. Naona kama media houses zime paralyse. Mwaka karibia wa pili sinunui gazeti japo vitabu nasoma sana. Waandishi wa magazeti wakati huo wakiwa na nguvu kweli za kuset agenda. Nakumbuka sana akina Salva Rweyemamu wakiwa New Habari wakitikisa kweli kweli mpaka wakafika hatua ya kuwa maafisa habari wa Ikulu
 
Huyu mtu nafikiri kwa sasa ana cheo kikubwa serikalini.

Uandishi wake unatoa hamasa kwa msomaji, huichoki makala yake
 
Nyaronyo Kicheere yupo Dar es Salaam, anajishughulisha kama Mwanasheria. Kuna kijiwe kimoja huwa anakuja kila wiki pale CBD. Mzima wa afya.
 
Sasa kama hununui gazeti mwaka wa pili sasa wao watakula wapi, maana kuandika hakulipi kabisa siku hizi...
 
Mimi

Nawakumbuka, NYASIGO CORNEL, ARISTIKO KONGA, Rai enzi hizo.... Pia Prof Charles Bwenje Raia Mwema....ilikuwa raha
Umenikumbusha mbali sana mkuu umemsahau
Mihangwa na padre privatus karugendo (Rip)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…