kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA afariki dunia
Jul 22, 2019 13:06 UTC
Yukiya Amano Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 72.
Ofisi ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) mjini Vienna Austria imethibitisha kufariki dunia mkurugenzi mkuu huyo.
Yukiya Amano mwanadiplomasia wa Japan alizaliwa mwaka 1947 na kabla ya kuchukua wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomikia (IAEA) aliwahi kuhudumu kama balozi wa Japan huko Vietnam, Marekani na Ubelgiji.
Alichukua wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) mwaka 2009. Licha ya kuwa, muda wa uongozi wa Amano ulitarajiwa kumalizika mwaka 2021, lakini hivi karibuni alitangaza kuwa, anatarajia kujiuzulu mwezi Machi mwakani kutokana na sababu za kiafya.
Yukiya Amano alikuwa na nafasi muhimu mno wakati wa kufanyika mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1.
Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa salamu za rambirambi na kumtaja Amano kama mtu aliyekuwa mahiri katika kutekeleza majukumu yake.
Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema katika ujumbe wake wa salamu za rambirambi kwamba: Nimehuzunishwa na kifo cha Yukiya Amano. Alikuwa mtu muwajibikaji na daima hakuegemea upande wowote bali alikuwa akihudumia jamii ya kimataifa.
Rafael Grossi mwanadiplomasia wa Argentina na Cornel Feruță mwanadiplomasia wa Romania wanatajwa kuwania kiti cha Yukiya Amano.