Yu wapi mwanasiasa John Mnyika katika taswira ya siasa Tanzania?

Kajuni

JF-Expert Member
May 27, 2009
483
186
Salam?

Miezi sita imepita tangu upate fursa ya kurudi tena mjengoni kupitia UKAWA-Chadema. Vipi kulikoni mbona hausomeki? Yale makeke yako siku hizi mbona hatuyaoni mtaani /jimboni kwako mpaka mjengoni?

Huku Mbezi -Msumi ulituaidi kufuatilia miundombinu ya maji,barabara,Shule etc lakini mambo ni kama yalivyokuwa miaka 5 iliyopita je ni kweli kwamba kutokana na mabadiliko hapo chamani umebanwa mbavu kwani hukumkubali Manywele? Je ni kweli wewe ni team Slaa?

Wananchi wako tulikuwa na matumaini makubwa sana kwako lakini inawezekana tulivyofikiria sivyo. Na pumzi imekuishia? Basi kama ndivyo tuachie Jimbo letu wewe ukapumzike.

Naomba kuiwakilisha.
 
Kuna Mbunge wa CCM( Kasulu) Jana kasema Bungeni Mnyika amelazwa Mhimbili anaumwa kichaa.!

Nadhani wanaojua watatujuza ukweli.!
 
Huyu jamaa alikuwa vocal cha ajabu kawa mpole kama pundamilia na hasikiki! Uwakilishi wa Jimbo la Kibamba upo mashakani.
Myika sio yule tuliye mfahamu?!! Jamani wenye taharifa Mh. amepatwa na nini?
 
Mbona juz alikuwa huku mbez mwisho.....
Alikuwa na agenda gani? Barabara zote za ukanda huu zimegeuka maandalizi:
1. Mbezi Kinyerezi kupitia Malamba
2.Mbezi Msumi mpaka Madale Tegeta
3.Mbezi Msakuzi
4.Mbezi Mpiji
Hizo ni barabara chache kubwa ambazo zipo hoiiiii
Kweli tulifanya makosa pengine yule mama anayesuka twende kilioni angetuvusha. Sasa Myika naona kabanwa mbavu na mambo ya siasa za ndani.
 
Ilaumu Serikali sio mh. Mbunge yeye mbunge jukumu lake ni kuwasemea wananchi ndani ya bunge na kufuatilia utekelezaji, bunge lenyewe limekuwa bubu, halirushwi live unategemea utamsikia
 
Usitusemee barabara zetu zitajengwa ila na hii mvua unadhani anaweza kufanya chochote?
 
Alikuwa na agenda gani? Barabara zote za ukanda huu zimegeuka maandalizi:
1. Mbezi Kinyerezi kupitia Malamba
2.Mbezi Msumi mpaka Madale Tegeta
3.Mbezi Msakuzi
4.Mbezi Mpiji
Hizo ni barabara chache kubwa ambazo zipo hoiiiii
Kweli tulifanya makosa pengine yule mama anayesuka twende kilioni angetuvusha. Sasa Myika naona kabanwa mbavu na mambo ya siasa za ndani.
Siamini mnayosema lakini niwajibu wenu kukumbusha jukumu ni lake.
 
Mizuka..
Neno hoja/singi kwao ni kama upofu..

Sasa mleta mada unataka JJM akakujengeni barabara..??!
 
Kuna Mbunge wa CCM( Kasulu) Jana kasema Bungeni Mnyika amelazwa Mhimbili anaumwa kichaa.!

Nadhani wanaojua watatujuza ukweli.!

Nadhani usichopenda kutendewa wewe usimtendee mwenzako.Hata siku moja usimuombee binadamu mwenzko mabaya.Sasa huko kwenye wadi ya vichaa ataenda yeye Mbunge wa CCM Kasulu
 
Alikuwa na agenda gani? Barabara zote za ukanda huu zimegeuka maandalizi:
1. Mbezi Kinyerezi kupitia Malamba
2.Mbezi Msumi mpaka Madale Tegeta
3.Mbezi Msakuzi
4.Mbezi Mpiji
Hizo ni barabara chache kubwa ambazo zipo hoiiiii
Kweli tulifanya makosa pengine yule mama anayesuka twende kilioni angetuvusha. Sasa Myika naona kabanwa mbavu na mambo ya siasa za ndani.
Bajet ya halmashauri ...imeziweka kwenye mpango barabara tajwa zote hapo...juu.....rejea ,bajet ya halmashauri ya kinondon.....
 
Katibu mkuu wa Chama cha siasa tena kikuu cha upinzani kuteuliwa Daktari Bingwa wa Kichaa cha Binadamu badala ya wanasiasa wazoefu waliokifikisha chama kilipo akiwemo Mnyika ni kuwadhalilisha viongozi wengine. Acheni apige kimya!
 
Ilaumu Serikali sio mh. Mbunge yeye mbunge jukumu lake ni kuwasemea wananchi ndani ya bunge na kufuatilia utekelezaji, bunge lenyewe limekuwa bubu, halirushwi live unategemea utamsikia
Sasa mbona kimya hatumsikii? Nadhani amepoteza mwelekeo?
 
Hizo barabara mbovu mnataka mnyika afanye nini? Ajenge au? Kwanini JPM asifanye ziara ya kushitukiza kwenye barabara hizo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom