Kuna fununu kuwa kuna matatizo kwenye ndoa yake na mumewe,sasa naomba mtupatie habari zaidi mnaofahamu kuhusu hilo.
Matatizo yake ya ndoa yanakuhusu nini wewee? Badala ya kufikiria majanga yanayoitafuna hii nchi, na jinsi ya kuyaepuka, unapoteza muda kuulizia matatizo ya mtu ya ndoa!
Kuna vitu kama
(1) Hali ya huduma za afya
(2) Elimu - Walimu, vitendea kazi, mitihani n.k
(3) Miundo mbinu...reli, barabara, ndege (TRL, ATCL) ajali za kila siku za mabasi.
(4) Umeme - Mabwawa, hali ya mvua, mashine chakavu tokea enzi za mkoloni, hatima ya DOWANS
(5) Maji - Mgao wa maji, na kukosekana kabisa kwa huduma za maji, hasa vijijini.
(6) Ulinzi na usalama - Mabomu kulipuka ovyo - uwajibikaji wa serikali kuhusu mabomu, matokeo ya maafa etc
- Polisi kutumia silaha ovyo kutawanya watu kwenye matukio
(7) TISS - Siri za ndani za nchi kuvuja ovyo - kukosekana kwa nidhamu ya kazi ndani ya waajiriwa wa TISS
(8) Vyombo vya habari - Mengi na wenzake wanavyotumia vyombo vyao vibaya
(9) Bei za vitu kupanda bila sababu maalum (MAFUTA/SUKARI/UNGA/NYAMA etc) na serikali kukaa kimya.
(10) Foleni za magari zinazozidi kuongezeka kwanye miji mikubwa (Dar, Mwz, Ars etc)
NA MENGINE MENGI TU.....
WE UNAULIZIA NDOA!!!! KWELI WE NICKNAME!!!!!!!!!!!!!