Elections 2010 Yu wapi mgombea mwenza wa CHADEMA?

Naona leo CCM imepandisha dau maana mnajipanga kama wanne kabla hamjaanzisha mada kibudu

Ama kweli ukimshika Simba sharubu, utajeruhiwa....

Sipati majibu hapa zaidi ya matusi na kejeli. Au ndo mambo ya mkuki kwa nguruweeee..


Wapi JF, naombeni majibu.....


Nawakilisha Oktoba 31
 
alichemsha Jangwani ndo maana wamemficha yeye ndo aliongea pumba pale jangwani mpaka matangazo ta TV yakakatwa.


Usitake kuongea uwongo na kuwadanganya watu, matangazo yalikatwa wakati Marando anawataja mafisadi kwa majina, alipoanza kusema takukuru......matangazo yakatwa.
 
...Ukisikia kukwama kimawazo ndio huko sasa huyo mgombewa mwenza ndio atakayeongoza nchi au Rais au? yale yale Uchaguzi si lazima kushinda!!!
 
:dance::dance::dance::dance::dance::dance:anafanya kampeni nadhani mtamuona siku ya kuapishwa so punguza presha
 
Ukweli, Chadema hawakuwa tayari kwa ajili ya kinyang'anyiro cha urais. Wanafahamu vizuri kabisa kwamba Slaa alikuwa anatetea kiti chake cha Karatu na Mbowe baada ya kugaragazwa ile 2005 na Kikwete akaona njia pekee kutomvaa mwaka huu kwani kipigo kingekuwa kikubwa zaidi. Akajipima akaona ubunge ndiyo size yake kugombea. Sasa Slaa kugombea urais ni kwamba amelazimishwa lakini pia baada ya yeye nae kuwawekea masharti magumu Chadema kuwa baada ya Oct 31 waendelee kumpatia stahili zake alizokuwa akizipata kama mbunge. Slaa aliamua kuwapa kisogo wana karatu kwa ajili ya mkataba huo akijua wazi hawezi kushinda urais na vilevile lolote lingeweza kumtokea Karatu kama angeamua kugombea ubunge.


Nini kilichotokea?

Chadema kwa vile haikuwa na mgombea, basi ilibidi wakurupuke na kuanza kukamatia yeyote ambaye alikuwa karibu, walijaribu kichinichini kuwashawishi baadhi ya big name ndani ya CCM hasa wale ambao wanawaponda kwa kuwatuhumu sana, lakini wakapigwa chini. Baada ya kukurupuka huko kwa Slaa, wakagundua kuwa hawana mgombea mwenza, wakataka kuwa-fool CUF kwamba waunganishe nguvu na Hamad Rashid awe mgombea mwenza. Lakini wakasahau kuwa tayari walishavunja makubaliano na CUF katika chaguzi mbalimbali ambazo CUF waliomba kusimamisha mgombea mmoja wa upinzani. Kana kwamba haitoshi Chadema ilionesha dharau kubwa kwa CUF kwamba wao wana uwezo wa kwenda kwenye uchaguzi peke yao matokeo yake jimbo la Busanda na Mbeya Vijijini wakayakosa CCM ikaendelea kuyashikilia.


Baada ya mambo kuwa magumu na kutokukubalika zaidi Zanzibar, Chadema ilichofanya ni kutafuta 'bora mgombea mwenza' ili itimize masharti ya NEC lakini wakijua kabisa wanachofanya ni kuwahadaa wa Zanzibar kwani hawana mpango wowote na Muungano. Kwahiyo basi mgombea mwenza yule yupo kama figure tu kwa ajili ya kutimiza masharti ya NEC na wana uhakika kuwa kuwapo kwake sitatizo kwani hawawezi kuupata urais na yeye kuwa makamu wa rais.
Falsafa iliyopo hapo ni kwamba tayari chadema walikwisha shindwa uchaguzi kabla hata mchakato haujaanza na ukitaka kuthibitisha hivyo fuatilia kampeni zao hakuna lolote wanaloelezea zaidi ya hadaa na mambo ya kufikirika tu.

Hopeful this time mgombea mwenza huyu 'hawatamjumbe' ili kusogeza uchaguzi mbele. Maana 2005 walipoona wanazidiwa duh...!!!


Hiyo Red inaonyesha jinsi unavyokurupukia mambo. Nec wanatoa masharti ya rais na makamu wa rais au ni katiba ya nchi ndiyo inabainisha? Go to school!!!!
 
MASHEIKH MWAKA HUU HATUSHIKIKI. ndugu yangu amezinduka na ameona bora akajilalie.
 
Kwani ni kosa kumuulizia huyu mgombea mwenza? Tatizo liko wapi naona wengine wamepanic hadi wanaitana wapumbavu. Duh hiyo kali...Ni vema mwenye jibu akalitoa na sio kutoa maneno ya kejeli au huyu mgombea ana tatizo? Mbona kila mchangiaji analikimbia hili swali?

Kwa sababu CV yake haikidhi viwango!!!! Habari za kuaminika ni kwamba huyu ni STD 7. Huenda inaogopwa kuwa watu watachelea kumchagua kwa sababu huenda siku moja nchi ikatawaliwa na Std7! Mbona wagombea wenza wa vyama vingine tunawasikia?

Kwa kweli ingekuwa uungwana ikajibiwa tujue aliko badala ya kutoa maneno ya kejeli
 
mgombea mwenza wa chadema leo yuko mkoa wa kaskazini pemba katika majimbo ya kojani na ole




 
:smiling:CHADEMA kumtambulisha Makamu wa Rais kwa Wananchi kwenye sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Nne. Mh. Dr. Wilnroad Slaa:smiling:

Mitanzania bwana inaenda kwenye uchaguzi hata haijui inachagua nini?
 
Mgombea mwenza wa Slaa?Sijamuona katika kampeni na sehemu mbalimbali muda kwa mrefu.Yuko wapi huyu ndugu yetu?


nimeshaeleza na narudia tena kutoa maelezo,mgombea mwenza wetu yuko pale mwalas(mwanakwerekwe language school) anjifua katika ingilishi kozi!! we vipi?? unadhani anaweza kuwa makamu gani wa rahisi asiyejua kusema hata hawayu?? thenki yu??? welkamu??? silaha anatafuta kura yeye ananoa kichwa,kwani ilikuwa ni sapuraiz attack kuwa mgombea mwenza!
 
wanaona aibu kumleta hadharani kwani huwa wanajidai chama cha wasomi,sasa yamewakuta na mgombea mwenza wa darasa la tatu alafu wakatudanganya eti ni darasa la saba!! lol!
 
Kama wewe ni mwanasisiem huna jipya wala sera,nakuonea huruma maana hata mungu haya anayaona ubinafsi mlionao unatisha hivi mnawafikiria lakini walioko huko vijijini mateso wanayoyapata?? Au watajiju na ni hivyo basi hukumu yenu mungu anaijua dhuruma mnayoifanya ya ufisadi nani asiyejua,dr.aliyasema hayo yote wengine wakacheka leo zakia mengo aliyekua waziri wa fedha leo yuko wapi,mabilioni yanaibwa watu hawana habari,wakowapi mauditors,kazi mnayo tupeni(chadema) nafasi maana safu nzima kwanza imeenda shule ya kiroho itambuayo shida za walioko chini
 
Back
Top Bottom