Young D atiwa mbaroni kwa kumshushia kichapo heavy jirani yake wa kike

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,495
Msanii wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ amejikuta mikononi mwa askari wa Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo jijini Dar kwa madai ya kuharibu simu na kushambulia mwili.

Habari toka kituoni hapo zinadai kuwa katika siku za karibuni, msanii huyo alimshambulia mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Nasra lakini pia aliharibu simu yake yenye thamani ya shilingi 600,000.

Makachero wa polisi waliovalia kiraia walivamia nyumbani kwa Young D, Sinza Mori na kumtaka ajisalimishe kituo cha polisi kwa amani lakini inadaiwa alileta ubishi ndipo askari hao wakalazimika kumpiga "tanganyika jeki" na kuondoka naye huku akiwa kifua wazi.

“Mbaya zaidi, alikuwa hajavaa shati ni suruali tu, ikabidi aende polisi hivyohivyo. Unajua hawa wasanii wetu bwana sijui huwa wanawaza kitu gani katika ustaa wao,” alisema moja ya majirani zake.

Habari zaidi zinasema kuwa, Nasra na Young D ni wapangaji wa nyumba moja lakini hawana uhusiano mzuri kwani mara kwa mara wamekuwa wakikwaruzana kwa sababu ambazo hazijulikani kirahisi.

“Siku ya tukio, inasadikiwa kuwa walikwaruzana sana, ndipo dogo (Young D) akaamua kumvaa mwanadada huyo na kumpa vitasa (ngumi) kisha kuivunja simu yake,” aliongeza jirani huyo.

Katika Wabongo Fleva wanaotamba, Young D naye yumo ambapo amepata jina kupitia vibao vyake viwili, Ujanjaujanja na Kijukuu.

Mmoja wa askari mwandamizi wa Kituo cha Urafiki alipohojiwa uhusu hatima ya mwimbaji huyo alisema: “Upelelezi unaendelea, ukikamilika atapelekwa mahakamani.”

Source: Bongo Movie.
 
Young.....as time goes atakuwa old then ataona alilolifanya angetumia kanuni Na Sheria angeitwa ADULT
 
Back
Top Bottom