Yote haya ni matokeo ya upinzani dhaifu...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yote haya ni matokeo ya upinzani dhaifu...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mirisho pm, Oct 26, 2012.

 1. mirisho pm

  mirisho pm JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 2,480
  Likes Received: 3,298
  Trophy Points: 280
  katika historia ya tanzania, upinzani umemark miaka ishirini hivi tangu uanzishwe rasmi., tofauti na matarajio ya wengi, kwamba angalau vitendo vya rushwa, matumizi mabaya au yasiyo ya lazima ya pesa za walipa kodi, kutoaminiana miongoni mwa jamii, uzembe wa kutoa huduma za msingi kwa jamii, tatizo la ajira, yote hayo yamekuwa yakiongezeka, hil halina ubishi.

  Sasa wadadisi wa mambo hata wananchi wa kawaida wamepoteza imani kubwa na upinzani kwa mising ifuatayo;

  mosi, baadhi ya viongozi wa upinzani kungangania madaraka, na kugombea nafasi za juu wao wenyewe tu..

  pili, baadhi ya viongoz wa upinzani kujihusisha na vitendo vya rushwa hasa wabunge, na pengine kuzitetea hasa wale wanaohusishwa nazo moja kwa moja, mf. nishati na madini, na wakat mwingine kuwakatisha tamaa wapambanj hawa hawa kukubali kuendesha magari ya kifahari wakati wao wenyewe wanayapinga majukwaani kwa nini wasikatae vitendo hivi kama sio mawakili wa siasa uchwara na siasa njaa zinazoitafuna nchi yetu kila uchao?

  MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Upinzani hawana dola! hawakusanyi kodi! kazi yao ni kushauri na kutoa sera mbadala na kuwaamsha watu.kusema ukweli bila upinzani hasa wa CDM kuanzia 2005 hii nchi ingekuwa imeshauzwa kitambo.

  Sema tuna rais Dhaifu! Serikali legelege! na upuuzi wa bunge under majority ya wapenda posho,rushwa,wanaolala hovyo kutoka chama tawala cha CCM.
   
 3. m

  mswald Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Like father like son!Suluhisho la matatizo yetu ni katiba iliokali na straight foward juu ya mambo ya msingi kama muundo/mfumo wa serikali, matumizi ya rasilimali za umma na uwajibikaji.Wala sio nanni kakaa Magogoni.Nikikumbuka wakati Kikwete anachaguliwa 2005 TULIKUA NA MATUMAINI SANA.Angalia miaka kumi sasa, tuko wapi??????
  Anayonia ya dhati kabisa ila mfumo alioukuta kuubadili bsio rahisi, sisi wananchi tuubadili kupitia KATIBA MPYA.
  Wapinzani njaa tu, watatupigisha MARK TIME na hatuna muda wakupoteza tena INATOSHA 50yrs, mchawi ni katiba.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Inawezekana una hoja ya msingi, ila hukuweza kuijenga vizuri. Huwezi kuulaumu upinzani ndani ya nchi hii kwasababu tu ya udhaifu na uovu wa serikali!
   
 5. b

  blueray JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Pole sana, mada yako umeijenga katika msingi wa tope!
   
 6. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  ni kweli kabisa muwasilishaji nakuunga mkono asilimia mia kwa mia lakini awali naomba nikuulizwe haya:-
  1. hv uchaguzi wa ndani unaondelea wa CCM tumeshudia rushwa iliyokithiri mpaka rais akikiri uwepo wa Rushwa hapo utasemaje?

  2. Hv wale mawaziri wawili kutoka wizara moja waliolumbana kisa naibu katolewa out na kampuni ya CCCC ni wanatoka upinzani?
   
 7. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,634
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Hivi tuhuma za rushwa uchaguzi BAVICHA zilikuwa ni sehemu ya kiwanda cha uongo au bado babu anafanya upembuzi yakinifu?
  Tusilikia mengi na vielelezo kubainishwa hatimae kombe limefunikwa na mwana wa haramu amepatikana si kupita tena.
   
 8. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,589
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani matokeo unayaona ni kutokana UJINGA wa watanzania walio wengi baadhi yao wakilewa fedha za ufisadi. Hata humu jamvini wamejaa wakitetea ufisadi na watawala wasiojali maslahi ya Taifa letu.
   
 9. m

  mdunya JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  pole kwa madhara ya A.R.V feki
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Watu wanabeza bure tu sasa. Iwapo hapo juu si hoja ni kipi sasa cha kujadilika hapa JF?! Jamani, mbona tunatanguliza kebehi kwa kila tusichokubaliana nacho? Mheshimiwa saana hapo juu kaleta hoja ya kwamba - iwapo upinzani unamiaka 20 sasa tangu urudi, ni kipi kimeufanya bado uonekane 'dhaifu' machoni pa wengine... na tumjibu kwa hoja basi ili kuelewesha jamii kwa ujumla. Ahsanteni.
   
 11. M

  Magadu Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapinzani njaa tu hawa.
   
Loading...