Yerusalemu – Kikombe cha kulewesha Mataifa

Yerusalemu – Kikombe cha kulewesha Mataifa

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Huo ni unabii ulioandikwa katika Zekaria 12:2 –
Tazama, nitaufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kulewesha kwa mataifa yote yaliyo pande zote…”

Mungu alimtumia Nabii Zekaria kutoa unabii huo wa ajabu kwamba Yerusalemu haitakuwa tu mji wa kawaida, bali utakuwa kikombe cha kulewesha.

Katika lugha ya Kiebrania, "kulewesha" inamaanisha kuchanganya akili, kupoteza mwelekeo, au kuvurugwa. Hivyo Yerusalemu itakuwa mji unaosababisha mataifa yashindwe kufikiri kwa hekima – wakifanya maamuzi ya vita, mashambulizi, au chuki, na hatimaye kujiletea maangamizi.

Mataifa mengi yanajaribu kushughulikia suala la Yerusalemu, lakini badala ya kutatua, yanazidi kulewa na kuchanganyikiwa kisera na kimwili – sawasawa na ilivyotabiriwa.

Unabii huo ni uthibitisho kwamba Biblia inasema kweli, na kwamba historia ya mataifa itaendelea kuzunguka Yerusalemu hadi Kristo Yesu atakaporudi kama Mfalme wa Amani.
 
Kifungu hicho cha Zekaria 12:2 kwa tafsiri ya BHN kinasema hivi:
"Nitaufanya mji wa Yerusalemu kuwa kama kikombe cha divai; na mataifa yaliyo kandokando yake yatakunywa na kuyumbayumba kama walevi..."
 
Sasa wewe una amini katika yesu mbona hao wa Jerusalem hawaamini yesu mpaka hivi sasa
 
Sasa wewe una amini katika yesu mbona hao wa Jerusalem hawaamini yesu mpaka hivi sasa
Soma huu uzi mwanzo mwisho utapata jibu:
 
Mkuu! Endelea kujaziajazia nyama.
Haya, karibu tena Kyenju ule nyama!

Zekaria alitoa unabii huo takriban miaka 2500.

Haya ni matukio mengine yaliyotimia baada ya Zekaria kutabiri au kutoa unabii:
1. Yesu kuingia Yerusalemu kwa punda
Huu ni unabii wa Zekaria 9:9
“Shangilia sana, ee Binti Sayuni! Piga kelele, Binti Yerusalemu! Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, ni mwenye haki, naye ana wokovu, ni mpole, naye amepanda punda, mwana-punda, mtoto wa punda.”

Unabii huo ulitimizwa wakati Yesu alipoingia Yerusalemu akiwa amepanda punda (Mathayo 21:1–9).

2. Kusalitiwa kwa Yesu kwa vipande 30 vya fedha
Nabii Zekaria alitabiri hivyo katika Zek 11:12–13
“Nikawaambia, Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe. Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha.”

Unabii huo ulitimia Yuda Iskariote alipomsaliti Yesu kwa vipande 30 vya fedha (Mathayo 26:14–15). Baadaye, fedha hizo zilitumika kununua shamba la mfinyanzi (Mathayo 27:5–10).
 
Soma kitabu cha Zekaria utaona matukio mengine yaliyotimia baada ya Nabii Zekaria kutabiri. Biblia ni kitabu cha kweli. Ndio sababu shetani anakichukia sana na kuwadanganya watu wasikisome, ili waendelee kukaa gizani, wasiujue ukweli wakawekwa huru.
 
Huo ni unabii ulioandikwa katika Zekaria 12:2 –
Tazama, nitaufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kulewesha kwa mataifa yote yaliyo pande zote…”

Mungu alimtumia Nabii Zekaria kutoa unabii huo wa ajabu kwamba Yerusalemu haitakuwa tu mji wa kawaida, bali utakuwa kikombe cha kulewesha.

Katika lugha ya Kiebrania, "kulewesha" inamaanisha kuchanganya akili, kupoteza mwelekeo, au kuvurugwa. Hivyo Yerusalemu itakuwa mji unaosababisha mataifa yashindwe kufikiri kwa hekima – wakifanya maamuzi ya vita, mashambulizi, au chuki, na hatimaye kujiletea maangamizi.

Mataifa mengi yanajaribu kushughulikia suala la Yerusalemu, lakini badala ya kutatua, yanazidi kulewa na kuchanganyikiwa kisera na kimwili – sawasawa na ilivyotabiriwa.

Unabii huo ni uthibitisho kwamba Biblia inasema kweli, na kwamba historia ya mataifa itaendelea kuzunguka Yerusalemu hadi Kristo Yesu atakaporudi kama Mfalme wa Amani.
kwamaana hiyo yesu ni massiah wa israel si wengine hatuhusu?
 
Angalia PM
Umesema niangalie PM? Hii Prophetic Message(PM) niliishaisoma zamani:
"Lakini yakupasa ufahamu jambo hili: kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wanaopenda anasa kuliko kumpenda Mungu: wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu kama hao."(2Tim 3:1-5).
 
Back
Top Bottom