Yepi Yanayomkuta Mkuchika

Yepi Yanayomkuta Mkuchika

nankwanga

Member
Joined
Dec 30, 2011
Posts
44
Reaction score
6
George Mkuchika tangu mapema mwezi wa 3 amekuwa akikosa watu kwenye mikutano yake huko Newala na kwa siku ya jana tarehe 14/03/2013 Mjini Masasi.

Kutokana na fedheha anayopata anasukumia lawama upinzani haswa Chadema na kufananisha vyama vya upinzani kuwa sawa na upele au jipu ambalo halipaswi kuwepo kwenye mwili.

Kitu ambacho viongozi wengi wa Chama tawala wamekuwa wakijaribu kukifanya ni kujaribu kupotosha jamii kuwa upinzani ni dudu baya sana la kuepukwa..

Wananchi wameamka sasa hata huku kusini ambako kulionekana kulala.
 
Huyu jamaa tulisikia hakushinda wakati wa uchaguzi uliopita. Sasa anachojaribu kufanya ni kwenda kutafuta huruma za wananchi. Nadhani anapata malipo sahihi ya dhuluma zake. Angefanya vizuri tangu huko mwanzo wananchi wangekuja kwenye mikutano yake.
 
Idadi ya Wafuasi wa Chadema Mtwara ni sawa na Idadi ya wafuasi wa CUF Kibororoni au Machame!
 
Idadi ya Wafuasi wa Chadema Mtwara ni sawa na Idadi ya wafuasi wa CUF Kibororoni au Machame!
1/Sasa inakuwaje CHADEMA iwe tishio kwa CCM hapo Mtwara?

2/Kwanini kila kukicha CCM tunahangaika na kuitukana CHADEMA hapo Mtwara?

3/Kwanini Mkushika, Hawa Ghasia nk wanahaha usiku na mchana kuinusuru CCM isife dhidi ya CHADEMA hapo Mtwara?

4/Kwanini kila kukicha CHADEMA inakuwa gumzo la mji wa Mtwara?
 
Wakuu,
Mkuchika wiki iliyopita alikuwa Newala na alichofanya ni kuwapigisha wana Newala kura za siri na kupitia yeye anadai wana Newala wanaunga mkono gesi kwenda Dar es salaam! Lengo la huyu mheshimiwa siyo zuri zaidi ya kutupiganisha...
 
Labda anatafuta ulaji tu.Pole ni bora kufa maskini kuliko kuwa mnafiki
 
Mhmnn..hao wapiga kura za siri aliwapa ngapi? Vituko vya magamba haviishi. Huyu mwajina wangu hatari sana.
 
Mkuushika, wala asijisumbue. Anatakiwa kuwaambia wana ntwara kwamba. GEC HAITOKO, ------ AKASADDAMIWE HUKO CHNA, nakwambia mikutano yake itatapika mara dufu
 
Mhmnn..hao wapiga kura za siri aliwapa ngapi? Vituko vya magamba haviishi. Huyu mwajina wangu hatari sana.

lengo lake ni kuharibu tu! anasema wana newala wanaunga mkono gesi isafirishwe..wana newala wote si ccm!
 
:high5::dizzy::A S angel::fear::A S shade::A S-heart-2::lying::high5::high5::rockon::rockon::rockon:😛layball:😛layball:😛layball::nono:
 
huyu jamaa sijui anaupata wapi ujasiri huu wakujaribu
kufanya mambo ambayo watu wapo tayari kufa..ya masasi na mtwara yeye hakuyaona na sasa anajidai kufunga masikio...naamini Wana newala siyo waoga kama anavyodhani...
na haya yatamgarimu sana...
 
Labda anatafuta ulaji tu.Pole ni bora kufa maskini kuliko kuwa mnafiki

ulaji gani mkuu wa kujenga chuki na kuweka migogoro ndani ya wanakusini? na watanzania kwa ujumla? no more time for them to ruin us!! we are coming
 
Na jana kapata aibu yake hapa Masasi kwenye kijimkutano chake kilichohudhuriwa na magamba ya kijani tu.
Yaani ni aibu baadae utasikia akisema watu wa Masasi wamekubali gesi itoke
Ni aibu ilije na ni mwisho wake kisiasa huo
 
Idadi ya Wafuasi wa Chadema Mtwara ni sawa na Idadi ya wafuasi wa CUF Kibororoni au Machame!

Mbona unajikanganya mkuu, utafananishaje Mtwara ambayo ni Mkoa na kamji kama Kiboroloni?

Ukirudi kwenye mada Mtwara ni Mkoa wenye Halmashauri sita (Mtwara vijijini ndio ya sita- kule kwenye gesi nyingi) na Wilaya tano (Mtwara Mjini, Tandahimba-wazalishaji wa korosho nyingi na tamu kuliko zote ulimwenguni, Newala, Masasi Na Nachingwea- kule kwenye makambi ya JW na mashamba mkubwa).

Sehemu ambazo CUF walikua na nguvu ni tatu tu(Mtwara Mjini, Tandahimba na Newala) but sasa CHADEMA wamekuja kwa kasi na kushika hatamu kwenye halmashauri nne (Mtwara Mjini, Mtwara Vijijini, Masasi na Nachingwea).

Tandahimba na Newala ni fifty-fifty kwasababu ya Bw. KATANI (Mbunge wa Wananchi wa Tandahimba ambao wana undugu wa damu na Wananchi wa Newala- Familia nyingi za Tandahimba asili yao ni Newala, pia Bw. Katani ni Naibu Katibu wa CUF Vijana Taifa).

Hivyo kwasasa CUF hawana chao tena kwa ujumla Wananchi wengi wanaipenda CHADEMA.

NB: Dr. Slaa alivyochaguliwa kuwa katibu mkuu wa CHADEMA ziara ya kwanza ya kukijenga chama ilianzia mikoa ya kusini na Katika Wilaya ya Tandahimba (kuanzia 2010 ilikua strong hold ya CUF) kata ya Kitama Kitongoji cha KITAMA-1 ndio tawi la kwanza la CHADEMA lilifungulia wilaya ya Tandahimba, enzi hizo ilikua wilaya ya Newala.
Miaka hiyo CUF ilikua haijakanyaga Kusini.
 
George Mkuchika tangu mapema mwezi wa 3 amekuwa akikosa watu kwenye mikutano yake huko Newala na kwa siku ya jana tarehe 14/03/2013 Mjini Masasi.

Kutokana na fedheha anayopata anasukumia lawama upinzani haswa Chadema na kufananisha vyama vya upinzani kuwa sawa na upele au jipu ambalo halipaswi kuwepo kwenye mwili.

Kitu ambacho viongozi wengi wa Chama tawala wamekuwa wakijaribu kukifanya ni kujaribu kupotosha jamii kuwa upinzani ni dudu baya sana la kuepukwa..

Wananchi wameamka sasa hata huku kusini ambako kulionekana kulala.
Atajuta ata wakati wa uchaguzi Almashauri ya wilaya Newala si ndio iliyombeba,maana alikuwa anapumulia mashine,matawi mengi tu aliyafungua 2010 muda mfupi kabla ya uchaguzi siku zingine alikuwa haonekani,naumshauli sasa akifika newala aende tu kujipumzisha plateau,gesti aliyowajengea wana newala badala ya miundo mbinu na kuleta maendeleo.
 
Back
Top Bottom