Yeast Infection Maambukizi ya Kuvu ( AFYA YA UZAZI KWA WANAWAKE ) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yeast Infection Maambukizi ya Kuvu ( AFYA YA UZAZI KWA WANAWAKE )

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Feb 25, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Wanawake wengi watapata maambukizi haya katika maisha yao. Maambukizi haya huwasha, ni chungu lakini ni rahisi kutibu. Walio na ugonjwa wa Sukari huambukizwa haraka kwa sababu ya sukari nyingi katika damu yao. Pia kwa wanao ugua Ukimwi. Daktari atakupa madawa ya kutibu.
  Nini dalili za maambukizi ya kuvu?
  • Kuwashwa ndani na nje ya uke.
  • Golegole nzito yenye gamu kutoka kwenye uke
  • Uchungu au hali ya kuchomeka unapokojoa au kushiriki ngono
  • Ngozi iliyogeuka nyekundu sehemu ya uke
  • Golegole inayotoka katika uke yenye harufu mbaya
  • Ishara kujitokeza juma moja kabla ya kwenda hedhi.

  Unatibu vipi maambukizi haya.


  Kama umewahi kuambukizwa basi unaweza kununua kirimu ya anti-fungalna ujipake, ikiwa hujawahi kuambukizwa basi muone daktari akushauri.

  Utazuia vipi maambukizi ya ukungu

  • Wacha kutumia dawa za kuua bakteria - antibiotics ikiwa si lazima
  • Kunywa maziwa mala - yorghurt kupiga vita bakteria
  • Usivae chupi zinazokubana sana. Vaa chupi za nyuzi za pamba na zisizikubane
  • Osha mikono na iwe imekauka kila wakati
  • Jaribu usitumie marashi, poda na sabuni za marashi kuosha sehemu nyeti
  • Osha sehemu nyeti kila mara na uhakikishe umekausha vizuri
  • Jaribu kuimarisha kiwango cha sukari katika damu yako
  • Tumia kondomu na wacha kushiriki ngono ukitumia midomo.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Maambukizi ya mfereji wa mkojo.

  Hutendeka bakteria zikiingia katika kibofu cha mkojo. Unapokojoa, unahisi moto, usipotibu inaweza kuzidisha maambukizi. Hali hii huletwa na kushiriki ngono, na magonjwa ya zinaa.
  Ishara za mfereji wa mikojo kuambukizwa
  • Kukojoa mara nyingi
  • Ghafla kuhisi kukojoa
  • Uchungu au moto unapokojoa
  • Uchovu, damu katika mikojo, kuumwa na mgongo sehemu ya chini, kuumwa na tumbo

  Unatibu vipi?

  • Muone daktari na tumia antibiotics
  • Kunywa maji mengi
  • Meza vidonge vya kumaliza maumivu kama Tylenol na Panado
  Utazuia vipi ugonjwa huu
  • Kunywa maji mengi ili kuondoa baKteria mwilini
  • Jiweke msafi sehemu zako za siri
  • Kojoa unapojihisi
  • Jipanguze kutoka mbele hadi nyuma
  • Usitumie vipodozi vya kujipulizia
  • Vaa chupi zilizotengezwa kwa pamba
  • Nenda chooni baada ya kushiriki ngono, hakikisha mikono yako ni safi.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Magonjwa ya Zinaa

  Watu wengi hawapendi kuzungumzia magonjwa ya zinaa, lakini wengi huambulia kuyapata mara moja katika maisha yao. Kunyamaza hakusaidii.

  Wanawake wamo hatarini zaidi.


  Kwa sababu ya vile maumbile yao yalivyo, wana nafasi kubwa kupata magonjwa ya zinaa. Magonjwa kama kaswende, kisonono, Chlamydia huwa hayaonyeshi dalili zozote kwa wanawake. Wasipotibiwa, maambukizi huleta ugumba, wasiweze kupata mimba kabisa. Magonjwa mengine kamaHPV, Herpes, na Ukimwi huwa ya maisha. HPV yaweza kuleta saratani baadaye unapozeeka.

  Waweza kuzuia na kutibu magonjwa ya zinaa

  Jifunze jinsi ya kuongea na mpenzi wako ili kushiriki ngono kwa usalama. Tumia kondomu, jifunze kujizuia au zingatia mke mmoja. Hata kama wewe ni msagaji (lesbian), pia unahitaji kushiriki ngono kwa usalama.


  Ngono za Usalama.

  Ngono salama: Fanya jambo la sawa
  Ngono ni sehemu muhimu kwa maisha ya mtu mzima, lakini usipojikinga waweza kupata mambo usio tarajia, au magonjwa ya zinaa ambayo ni hatari kama ukimwi. Mnaposhiriki ngono na mpenzi wako tumieni mipira ya kondomu, mnapofanya mapenzi bila kondomu, hatari ya kuambukizana magonjwa ipo.

  Jinsi gani ya kushiriki ngono kwa usalama?

  Unapomfahamu mpenzi wako ndio bora na salama. Ngono ya usalama ni hatua yoyote unayochukuwa kupunguza magonjwa ya zinaa. Magonjwa mengi ya zinaa husababisha ugumba/tasa, ulemavu wa watoto na maumivu. Kujikinga, kuwa muaminifu kwa mpenzi mmoja na fanya maamuzi ya busara.

  Ni zipi njia bora za kuzuia maambukizi?
  • Tumia kondomu
  • Usiguse vidonda vitokanavyo na magonjwa ya zinaa
  • Msishiriki ngono ikiwa mpenzi wako ana vidonda sehemu nyeti au maambukizi yoyote.
  • Nenda kwa uchunguzi kwa daktari kila mara
  • Ukiwa umeambukizwa pata matibabu mara moja.

  PMS- Shida Wakati wa Hedhi

  Wanawake wengi huwa na mabadiliko ya kimwili na hisia kabla, baada na wakati wa hedhi. Haijulikani vizuri ni nini kinachosababisha PMS. Dalili huja wiki moja au mbili kabla ya hedhi. Watu wengi hutoa mzaha kuhusu PMS na hawaichukulii kwa uzito. Ukweli ni kuwa hali hii huweko. Waweza kuwa hamu kubwa ya chakula fulani, kuumwa na matiti, kuvimba mwili na mabadiliko katika hisia.
  Ishara zake ni zipi?
  • Kubadilika kwa hisia
  • Kukasirika upesi
  • Kulia bila sababu
  • Kuwa na wasiwasi
  • Tamaa ya chakula
  • Maumivu tumboni au mgongoni
  • Kufura au kuumwa na matiti
  • Kuvimba mwili
  Utatibu vipi PMS?

  Kati ya wanawake 5 mmoja ana PMS. Mabadiliko ya hormone huleta dalili za PMS. Kuna mambo unaweza kufanya ilikukufanya uwe na raha.
  • Kula vyakula bora vya kujenga mwili
  • Pumzika, fanya mazoezi ya uvutaji pumzi ndani na nje
  • Meza dawa za kutuliza maumivu kama Panadol
  • Tumia chupa yenye moto kujikanda sehemu ya tumbo inayouma
  • Mueleze daktari wako maumivu yakizidi.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi Wa Matiti

  Katika nchi nyingi saratani ya matiti ndio inayojulikana sana miongoni mwa wanawake.Kutambua mapema ikiwa unayo shida kutasaidia kuokowa maisha yako.

  Kuna njia mbili za kuhakikisha maisha bora.

  Jifanyie uchunguzi wa matiti kila mwezi.

  Kila mwezi jichunguze , ili ufahamu kama kuna mabadiliko katika matiti yako.Chunguza vibonge na ishara zingine mapema.

  Jifunze mengi kuhusu saratani ya matiti na jinsi ya kujichunguza mwenyewe.

  Fanya Mammogram kila mwaka

  Mammogram ni picha za x-ray zinazo onyesha matiti kwa undani.Daktari hutumia picha hizi kuhakikisha vibonge vya aina yoyote havimo ndani ya matiti,hii ndio njia mwafaka ya kuchunguza saratani ya matiti

  Ukiwa na umri unaozidi miaka 40 unahitaji kufanya uchunguzi wa Mammogram kila mwaka.Kama jamaa yako wa karibu, mama , nyanya, au shangazi wamewahi kupatikana na saratani ya matiti,basi anza kufanyiwa uchunguzi miaka 10 mapema.

  Mammograms husaidia kuvumbua
  asilimia 85-90% ya kesi zote za saratani ya matiti. Jichunguze na daktari wako akuchunguze kila mara.

  Uchunguzi wa fupa nyongo - Pelvic Exams

  Uchunguzi wa fupa nyongo (pap-smear) kila wakati ndio njia bora kuangalia afya yako. Chunguzwa magonjwa ya zinaa, mimba na saratani za mlango wa kizazi nakadhalika. Uchunguzi huu unaweza kuupata katika hospitali za mikoa na kliniki za jamii bure au kwa daktari wa kina mama (gynaecologist)

  Uwe kijana au mzee, umeolewa au la, mwenye hisia nyingi za ngono au la, uwe msagaji au mwenye wapenzi wengi, uchunguzi wa afya yako utaokoa maisha yako.

  Uchunguzi wa fupa nyongo unahusu nini?
  • Kuelezea kujihusu, historia yako na ya familia ya kiafya
  • Uchunguzi katika maabara kuhusu magonjwa ya zinaa
  • Kushauriwa
  • Uchunguzi wa matiti
  • Uchunguzi wa fupa nyongo.
  Ukingo wa Uzazi

  Ukingo wa uzazi ni nini?
  Huu ni wakati wanawake hufikia kikomo cha kupata damu ya hedhi na kutoweza kuzaa. Muda huu huanza kutoka umri wa miaka 40. Hali hii yaweza kuanza polepole au kwa ghafla. Ukingo wa uzazi huathiri kila mwanamke tofauti.
  Kuna aina za upasuliwaji unaoweza kuleta hali hii. Kwa mfano, katika 'hysterectomy' tumbo la uzazi likiiondolewa, itasimamisha hedhi zako . Pia ovari zote mbili zikitolewa, hali hii huja mara moja licha ya umri wako.

  Dalili za ukingo wa uzazi
  • Siku za hedhi kubadilika badilika
  • Kuumwa na viungo
  • Hali ya kusahau mambo
  • Mabadiliko ya hisia za kimapenzi
  • Kutokwa jasho kwa wingi
  • Kuumwa na kichwa
  • Kukojoa kila mara
  • Kuamka mapema kuliko kawaida
  • Hali ya kukauka ukeni
  • Kubadilika kwa hisia
  • Kukosa usingizi
  • Kutokwa jasho usiku

  Utapambana vipi na dalili hizi?

  • Matibabu ya hormone, kama vile; vidonge na krimu ya kuweka ukeni
  • Fanyisha viungo vyote mazoezi, fanya mazoezi ya kuinua uzito na kunyorosha misuli.
  • Kula kwa wingi matunda na mboga na vyakula visivyo na mafuta nyingi. Pia kula vyakula vilivyo tengenezwa na soya.
  • Wanawake wengi pia hufaidika na ushauri wa mtaalamu wa afya ya akili wakati huu wa maisha yao.
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ahsante mkuu, itasaidia wengi sana!! watu tujenge tabia za kufuatilia mienendo ya afya zetu. Siyo unakuwa busy kutafuta pesa muda wote wakati afya unaihatarisha. Weekend njema!
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  big up mkuu!
   
 7. d

  debito JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  asante kwa ushauri umtusaidia wengi
   
 8. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Nashukuru sana mkuu kwa somo zuri, ngoja nilifanyie kazi. Pia ngoja niongeze material yangu.
   
 9. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  you are very good at reading different books, you are also a good inteprater..nice work thanx and much respect.
   
Loading...