Hao wa ofisini na mtaani sina shida nao nataka nizungumzie hao wa kanisani...
Kwanza lengo la wewe kwenda kanisani unalijua au unaenda kwa mazoea....kama lengo unalijua ni lipi??? Ujue binadamu tunatofautiana....walio wengi wanaenda kanisani kupata neno liwafae katika maisha yao ya kila siku ya kumtafuta Mungu na hatimaye uzima wa milele...watu wa namna hii hudhani kuwa kila mtu anaenda kanisani kwa lengo hilo. Kwa mtu anayeenda kanisani kwa lengo la kumtafuta Mungu huwa hapuuzii mambo madogo madogo....anajua akichelewa kanisani,akiwahi kutoka,akivaa nguo ya kukwaza wengine,asiposoma biblia ibada yake haikukamilika na akiona ndugu yake anafanya jambo ambalo yeye huwa linamcost hawezi kunyamaza,lazima atamuonya maana ndivyo neno linavyosema.
Hao wanaokufuatilia wasamehe bure...wao wanadhani mko safari moja kwa hiyo wanajitahidi kukushtua wanapoona unafanya mambo yanayokuweka mbali na Mungu. Nafikiri ni vema ukawaweka wazi tu kwamba hayo mambo kwako si muhimu sana sidhani kama wataendelea kukufuatilia...yangu mimi ni hayo tu