Yanga yatikisa kiberiti Tusker

JuaKali

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
776
118
Uoungozi wa klabu ya soka ya Yanga umesema kuwa timu yao haitashiriki mashindano ya Kombe la Tusker, kutokana na wachezaji wao wengi kuwepo kwenye kikosi cha timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa klabu hiyo, Iman Madega alisema kuwa upo uwezekana mdogo wa klabu yao kushiriki kombe hilo.

Madega alisema kuwa Yanga wakishiriki mashindano hayo watakosa muda wa kufanya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, itakayoanza Januari 10 na Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Stars, inayojiandaa kucheza na timu ya taifa dhidi ya Sudan katika mashindano yanashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya nchi zao, wanatarajia kucheza Novemba 29, jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zitarudiana tena baada ya wiki mbili nchini Sudan.

Madega alisema kuwa kutokana na ratiba jinsi inavyojionyesha hawatakubali kuingia kichwa kichwa kushiriki kombe hilo, kwani timu yao inaweza kuathirika katika maandalizi mengine.

Alisema kuwa mazingira ya kiufundi hayaruhusu timu hiyo kushiriki mashindano hayo kutokana na wachezaji wao tegemezi watakuwa hawafanyi mazoezi ya kutosha kwa ajili ya ligi hiyo.

Hata hivyo, alisema kuwa kabla ya kufikia kutoa maamuzi ya kutoshiriki mashindano hayo leo au kesho wanatarajia kukutana na viongozi wenzake pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo Mserbia Dusan Kondic kwa lengo la kujadiliana na kutoa msimamo wao.

Madega alisema kuwa katika kikosi cha timu ya Taifa, wachezaji 11 wanatoka timu yao.

Alisema kuwa kutokana idadi hiyo, Kondic hataweza kupanga timu wakati wa mazoezi akiwa na wachezaji 17 waliosajiliwa na klabu hiyo.

Madega alisema kutokana na mkanyagano huo maandalizi ya timu ya Taifa na kombe la Tusker yatavuruga mazoezi ya klabu hiyo.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo mashindano hayo yamepangwa kuanza Desemba 15 hadi 27 jijini Dar es Salaam.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom