Yanga yaivimbia Azam TV

Yanga yaivimbia Azam TV

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
mazoezi.jpg

`Wazchezaji wa yanga wakiwa katika mazoezi kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Wakati Yanga wakigomea mechi zake kuonyeshwa live na Televisheni ya kampuni ya Azam, Shirikisho la SokaTanzania (TFF) limesema timu itakuwa na haki na mechi zake za nyumbani pekee kama zionyeshwe au la.
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema hawapingani na uamuzi wa Yanga, lakini mechi ambazo hazitarushwa live ni zile za nyumbani pekee ambazo Yanga wana haki nazo na siyo za ugenini kama wanavyotaka.
Sisi hatuna tatizo nao kama wameamua hivyo, lakini suala lao lakutaka mechi zote zinazowahusishawao zisionyeshwe haitawezekana bali ni zile tu za nyumbani, lakini za ugenini siyo mali yao hivyo hawana haki nazo,alisema Wambura.
Mwishoni mwa wiki TFF, bodi ya ligi (TPL) pamoja na Kampuni ya Azam waliingia mkataba mnono wa kiasi cha Sh168,000,000 kuonyesha mechizote za Ligi Kuu kupitia kituo cha Azam TV, pamoja na kila klabu kuvuna zaidi ya sh 100 milioni.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema jana uamuzi uliofikiwa na kamati ya utendaji juuya kuonyeshwa kwa mechi hizo hauna maslahi yoyote kwao. Sanga alisema kuonyeshwa kwa mechi zao kunalenga kuwakandamiza badala ya kuwanufaisha kwa maendeleo ya klabu.
TPL haikutangaza zabuni kwa televisheni nyingine za ndani na nje ili kutoa ushindani wa kweli katika kupatikana televisheni ya kuonyesha mechi hizo. Hatukubaliani na uamuzi uliofikiwa wa kuingia mkataba bila ya kutangaziwa zabuni hizo kupitia televisheni nyingine kama ITV, TBC, Zuku pamoja na Star tv,alisema Sanga.
Alisema kuwa mmoja wa wajumbe wa TPL ni makamu mwenyekiti wa Azam FC ambaye ahauwezi kumtenganisha na Azam Media Limited.
Hauwezi kumtenganisha makamu mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed na Azam Media Limited, alisaini mkataba na Simba kama mkurungezi, jambo linalotufanya tusiwe na imani naye, alisema Sanga. Hatuoni sababu ya kuingia huko kwa sababu udhamini wao haulengi kutusaidia bali ni kutudidimiza,
sisi tunasimamia msimamo wetu wakutoonyeshwa kwani tunaamini Yanga ni klabu kubwa,alisema Sanga.
Timu nyingine zote ni shindani na haingii akilini kuamini kuwa Yanga ama timu nyingine yoyote itafanyiwa usawa mbele ya Azam ambao ndiyo wamiliki wakuu, alisema Sanga.
Kwa upande wa Mjmjumbe wa Kkamati ya Uutendaji ya Yanga, Musa Katabaro alisema Azam Media Limited haipaswi kuonyesha Ligi Kuu kwa sababu wao wana timu katika ligi hii. Katabaro alisema kwamfano Afrika Kusini, Super Sport hairuhusiwi kuonyesha ligi ya nchi hiyo kwa sababu wana timu katika mashindano hayo.
Bodi ya ligi kwa sasa imeteuliwa kwa muda na uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba, kwa nini kuwe na haraka ya kuingia mkataba na siyo tusubiri viongozi wapya watakaoingia madarakani,?alihoji Katabaro.

MCL
 
yanga wacha wajitoe si wana esa za unga na za epa?
 
yanga wacha wajitoe si wana esa za unga na za epa?

Tafuta point ya kuongea acha usengerema wewe katafute basha kama unawashwa huko nyuma pesa za unga anazo azan meneja wenu wa Zamani kelbu kibabayu wewe
 
Shida watu wa tff hwana elimu,,eti mechi ya ugenini si mali yao na tutaonesha,,,yaani hapo wanajidanganya sana hawa mabwana,kwanza nani huwa anawatafsiria mikataba na kuielezea,,,,i pitty tz soccer,,msemaji mwenyewe yule hata hafai,sijui nani alimpa,,yule bwana wallace karia ndo namshangaa kabisa anaongea ka anadhani yanga ni timu ya waganga njaa,,,
tuko nawe Bwana Manji,,kudos
 
Mimi nashabikia Simba
but Yanga wana point kwa hili
Mkuu hapo ni vita ya biashara tuu kwani mwenyekiti wa Yanga hawezi kuruhusu klabu yake itumike kutangaza bidhaa za watu wengine wakati bidhaa zake zikidoda madukani, si hoja nyingine asilan si wawajua Yanga na sera yao ya UDOSI.
 
Ikitangazwa zabuni, kuna uwezekano klabu zikapata deal ya maana.
Milioni 100 siyo nyingi, ukizingatia kuwa mpira bongo una washabiki wengi sana, hata sometimes watu wa mataifa mengine hutushangaa.
Huku diaspora huwa tunaangalia kupitia star tv mechi zinazotangazwa, na wakirusha unaweza kuforwadiwa text kutoka nchi ya mbali tu.
Msikubali wakuu, soka la bongo baDO linaangaliwa sana.
 
Mkuu tatizo ni kuwa na viongozi wanasiasa katika vilabu vyetu.
 
Mkuu tatizo ni kuwa na viongozi wanasiasa katika vilabu vyetu.
Simba na Yanga ndiyo timu zinazoangaliwa sana. Kwa hiyo kwenye hela wakikwaruzana, hakuna atayefaidika. Kuna mabilioni hapo na lazima Yanga ipate angalau bilioni moja.
Na simba angalau milioni 120.
 
Million 100 ni pesa ndogo sana. TFF inachotakiwa waitishe zabuni na makampuni mbalimbali yashindane kwa uwazi kupata hiyo tenda ya kuonyesha. Kwenye ushindani ndio dau litapanda na ndio advantage kwa vilabu!.
 
Mimi nashabikia Simba
but Yanga wana point kwa hili

ebu nitoe tongotongo,hivi Azam TV ni kituo cha TV chenye frequency,kwenye ving'amuzi au ni kipindi tu katika Channel ten kinachoitwa Azam TV.kama wana kituo kinapatiknaje? majibu tafadhal
 
Mkuu hapo ni vita ya biashara tuu kwani mwenyekiti wa Yanga hawezi kuruhusu klabu yake itumike kutangaza bidhaa za watu wengine wakati bidhaa zake zikidoda madukani, si hoja nyingine asilan si wawajua Yanga na sera yao ya UDOSI.
Inawezekana ni wivu wa kibiashara kweli. Lakini hilo si jambo la msingi kwenye hoja hii. La msingi ni iwapo wanachodai Yanga kina msingi ama la. Tusimwangalie Manji, tuangalie hoja yake. Kwani mlevi tilalila akikukataza kulewa kwa sababu ulevi kupindukia una madhara, utabisha kwa sabau tu yeye ni mlevi?
 
Mkuu, mie sioni sababu ya baadhi ya viongozi wa Yanga kutumia nguvu kubwa kiasi hicho wakati vilabu takriban vyote vimetia sahihi jambo hili.
 
Mkuu hapo ni vita ya biashara tuu kwani mwenyekiti wa Yanga hawezi kuruhusu klabu yake itumike kutangaza bidhaa za watu wengine wakati bidhaa zake zikidoda madukani, si hoja nyingine asilan si wawajua Yanga na sera yao ya UDOSI.

hivi Manji anafanya biashara ya reja reja kama azam
 
ndugu zangu,soka la bongo ndivyo lilivyo,hata tufanye nini,hatuwez piga hatua,watu wote wana njaa,na siasa ndiyo inatuponza,ndiyo mana soka letu linabak kichwa cha mwenda wazim kila siku,si simba ya rage wala yanga ya manji,kila mmoja rage na manji wapo kwa maslahi yao pale! ili tuweze kujinusuru,vijana wenye weled wajaribu kushika hiz nyazifa ndipo tutaweza jikomboa,mmenisoma!
 
Mkuu, mie sioni sababu ya baadhi ya viongozi wa Yanga kutumia nguvu kubwa kiasi hicho wakati vilabu takriban vyote vimetia sahihi jambo hili.
Huo unaouzungumzia wewe ni uungwana, lakini ligi zinaendeshwa si kiungwana, la sivyo timu ambayo haishiki nafasi yoyote ya juu ila haishuki daraja isingeifunga nyenzake iliyo hatarini kushuka daraja. Ligi inaendeshwa kibiashara na kiushindani. Ndicho wanachopigania viongozi wa Yanga, ingawa sikatai wanaweza pia kuwa na wivu wa kibiashara ndani yake.
 
'siwaoni wakina MadameX aisee kwenye topik kama izi..............wapi madameeeee'
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom