Yanga yaivimbia Azam TV

Yanga yaivimbia Azam TV

Huo unaouzungumzia wewe ni uungwana, lakini ligi zinaendeshwa si kiungwana, la sivyo timu ambayo haishiki nafasi yoyote ya juu ila haishuki daraja isingeifunga nyenzake iliyo hatarini kushuka daraja. Ligi inaendeshwa kibiashara na kiushindani. Ndicho wanachopigania viongozi wa Yanga, ingawa sikatai wanaweza pia kuwa na wivu wa kibiashara ndani yake.
Mkuu, mie niliona ni maslahi ya biashara tuu hapa baada ya TFF kututhibitishia kuwa baadhi ya viongozi wa Yanga walikuwa wakishiriki mikutano hiyo. Sasa mwenyekiti wake ndio aliolianzisha kwa kukataa akidai ni kwa maslahi ya klabu yake wakati yeye ni mfanyabiashara mkubwa vilevile.
 
ebu nitoe tongotongo,hivi Azam TV ni kituo cha TV chenye frequency,kwenye ving'amuzi au ni kipindi tu katika Channel ten kinachoitwa Azam TV.kama wana kituo kinapatiknaje? majibu tafadhal

ni kama Zuku
wana decoder zao soon wataanza kuziuza
 
Million 100 ni pesa ndogo sana. TFF inachotakiwa waitishe zabuni na makampuni mbalimbali yashindane kwa uwazi kupata hiyo tenda ya kuonyesha. Kwenye ushindani ndio dau litapanda na ndio advantage kwa vilabu!.

Hivi sheria ya manunuzi ya umma haiwahusu TFF? Kama inawahusu kwa nini haya yanatokea? PPRA mko wapi? Kuna watu wana bip jela hapo TFF.
 
mazoezi.jpg


`Wazchezaji wa yanga wakiwa katika mazoezi kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam.


Dar es Salaam. Wakati Yanga wakigomea mechi zake kuonyeshwa live na Televisheni ya kampuni ya Azam, Shirikisho la SokaTanzania (TFF) limesema timu itakuwa na haki na mechi zake za nyumbani pekee kama zionyeshwe au la.
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema hawapingani na uamuzi wa Yanga, lakini mechi ambazo hazitarushwa live ni zile za nyumbani pekee ambazo Yanga wana haki nazo na siyo za ugenini kama wanavyotaka.
Sisi hatuna tatizo nao kama wameamua hivyo, lakini suala lao lakutaka mechi zote zinazowahusishawao zisionyeshwe haitawezekana bali ni zile tu za nyumbani, lakini za ugenini siyo mali yao hivyo hawana haki nazo,alisema Wambura.
Mwishoni mwa wiki TFF, bodi ya ligi (TPL) pamoja na Kampuni ya Azam waliingia mkataba mnono wa kiasi cha Sh168,000,000 kuonyesha mechizote za Ligi Kuu kupitia kituo cha Azam TV, pamoja na kila klabu kuvuna zaidi ya sh 100 milioni.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema jana uamuzi uliofikiwa na kamati ya utendaji juuya kuonyeshwa kwa mechi hizo hauna maslahi yoyote kwao. Sanga alisema kuonyeshwa kwa mechi zao kunalenga kuwakandamiza badala ya kuwanufaisha kwa maendeleo ya klabu.
TPL haikutangaza zabuni kwa televisheni nyingine za ndani na nje ili kutoa ushindani wa kweli katika kupatikana televisheni ya kuonyesha mechi hizo. Hatukubaliani na uamuzi uliofikiwa wa kuingia mkataba bila ya kutangaziwa zabuni hizo kupitia televisheni nyingine kama ITV, TBC, Zuku pamoja na Star tv,alisema Sanga.
Alisema kuwa mmoja wa wajumbe wa TPL ni makamu mwenyekiti wa Azam FC ambaye ahauwezi kumtenganisha na Azam Media Limited.
Hauwezi kumtenganisha makamu mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed na Azam Media Limited, alisaini mkataba na Simba kama mkurungezi, jambo linalotufanya tusiwe na imani naye, alisema Sanga. Hatuoni sababu ya kuingia huko kwa sababu udhamini wao haulengi kutusaidia bali ni kutudidimiza,
sisi tunasimamia msimamo wetu wakutoonyeshwa kwani tunaamini Yanga ni klabu kubwa,alisema Sanga.
Timu nyingine zote ni shindani na haingii akilini kuamini kuwa Yanga ama timu nyingine yoyote itafanyiwa usawa mbele ya Azam ambao ndiyo wamiliki wakuu, alisema Sanga.
Kwa upande wa Mjmjumbe wa Kkamati ya Uutendaji ya Yanga, Musa Katabaro alisema Azam Media Limited haipaswi kuonyesha Ligi Kuu kwa sababu wao wana timu katika ligi hii. Katabaro alisema kwamfano Afrika Kusini, Super Sport hairuhusiwi kuonyesha ligi ya nchi hiyo kwa sababu wana timu katika mashindano hayo.
Bodi ya ligi kwa sasa imeteuliwa kwa muda na uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba, kwa nini kuwe na haraka ya kuingia mkataba na siyo tusubiri viongozi wapya watakaoingia madarakani,?alihoji Katabaro.


MCL

Huu ni wivu tu wa kibiashara alionao Manji na Yanga inatumika tu kuwasilisha hisia zake. Kama anaweza alete TV yake na yeye halafu washindane na Azam. Kumbuka Vilabu vidogo vimeona mwezi kwenye hili. Mnaposema klabu kubwa ni kwa sababu zipo klabu ndogo kama Rhino, Mgambo JKT. Ukubwa wa Yanga peke yake hauna maana katika mpira. Wacheni mambo ya kipuuzi Yanga. TV zipo hapa Tz kwa miaka karibu 20 iliyopita. Hatujaona mapinduzi ya TV katika soka. Leo hii anatokea serious mjasiriamali anayetaka twende angalau hatua mbili mbele mwaleta mambo yetu ya wivu wa kihindi hapa. AKILI NDOGO
 
nasikia yanga wamepata dili na pepsi cola la milion mia sita kwa mwaka ndio maana wamevimba kwa azam tv
 
Yanga tayari washaingia udhamini wa pepsi cola wa milioni 600,000,000/-we waache tff waendelee na ujinga wao. Na Azam watawatangaza pepsi cola kupitia yanga ktk mechi za ugenini
 
Huu ni wivu tu wa kibiashara alionao Manji na Yanga inatumika tu kuwasilisha hisia zake. Kama anaweza alete TV yake na yeye halafu washindane na Azam. Kumbuka Vilabu vidogo vimeona mwezi kwenye hili. Mnaposema klabu kubwa ni kwa sababu zipo klabu ndogo kama Rhino, Mgambo JKT. Ukubwa wa Yanga peke yake hauna maana katika mpira. Wacheni mambo ya kipuuzi Yanga. TV zipo hapa Tz kwa miaka karibu 20 iliyopita. Hatujaona mapinduzi ya TV katika soka. Leo hii anatokea serious mjasiriamali anayetaka twende angalau hatua mbili mbele mwaleta mambo yetu ya wivu wa kihindi hapa. AKILI NDOGO
Tujitahidi kufahamu zaidi yasiyosemwa na anayejitetea, kwa kuwa ndio huwa hataki tuyajue. Kwa nini uamini kwamba kati ya kauli mbili zinazopingana, ya Yanga ndio ya uongo? Kwa nini ya vilabu 13 vilivyobaki iwe ndio kweli? Walitoa ushahidi wowote anwai (kumbukumbu za mikutano, n.k) ambazo tuliziona tukajiridhisha kwamba Yanga walishiriki? Kwa nini tuamini tu kwa sababu wamesema? Mimi naamini vilabu 13 ndio havisemi kweli kuhusu hili, kwa sababu hawakujibu hoja ya Yanga kukataa kuonyeshwa rasimu ya mwisho ya makubaliano hayo. Kama Yanga ilishiriki kwenye vikao vya awali ama la, kitendo cha Kunyimwa rasimu hiyo ni sawa na kuwa haikushirikishwa, na ndio walichokisema. hawakusema kuwa hawakushiriki, walisema hawakushirikishwa. labda vilabu 13 havikuona tofauti ya mambo mawili hayo kwa uroho wao wa pesa, nawe wakakuambukiza makengeza yao. Hili la Yanga kunyimwa rasimu Vilabu 13 havikulikanusha. Kwa hivyo vyenyewe ndio havikusema kweli, licha ya longolongo nyingi za kutetea utamu walioonjeshwa na Azam. Usihadaike na wingi wao dhidi ya Yanga peke yake. Right is right even if everybody else says it is wrong. And wrong is wrong even if everybody else says it is right. Ligi yoyote duniani haipo kutetea vilabu vidogo wala vyovyote vingine. Ipo kwa ajili ya ushindani na kutengeneza fedha. Hilo haliji kwa kuvihurumia vilabu fulani kwa sababu yoyote. Kama ni hivyo maswala ya Ligi yangehamishiwa Ustawi wa Jamii badala ya Wizara za Michezo.
 
Yanga tayari washaingia udhamini wa pepsi cola wa milioni 600,000,000/-we waache tff waendelee na ujinga wao. Na Azam watawatangaza pepsi cola kupitia yanga ktk mechi za ugenini

Go Yanga hapo angalieni dau timu ifaidike, achaneni na huto tu milion 100 chukueni hizo 600
 
Komaeni sana Yanga,biashara ni ushindani si kuburuzwa............
 
Back
Top Bottom