Yanga yaichapa 3, ankara sekerspor

Yanga yaichapa 3, ankara sekerspor

Danny green

Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
18
Reaction score
4
Young Africans imeanza vizuri katika kambi yake ya mafunzo nchini Uturuki baada ya kuifunga timu ya Ankara Sekerspor kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika pembeni kidogo ya eneo ililofikia katika mji wa Manavgat Antalya.
Kocha wa Young Africans aliwatumia wachezaji 18 jumla katika mchezo huo ambao wenyeji mara baada ya mchezo walimpongeza kwa timu yake kwa kucheza vizuri katika mchezo huo wa kirafiki.
Dakika ya 10 ya mchezo shuti lililopigwa na mganda Emmanuel Okwi lilishinda mlinda mlango wa Ankara Sekerspor ambapo aliutema mpira huo na kumkuta Didier Kavumbagu aliyeukwamisha mpira huo wavuni na kuhesabu bao la kwanza.
Timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Ankara Sekerspor 0 - 1 Young Africans.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na iliwachukua dakika moja Young Africans kujipatia bao la pili la mchezo kupitia kwa Emmanuel Okwi aliyeitumia vyema pasi ya mwisho ya kiungo Mrisho Ngasa aliywatoka walinzi wa Ankara Sekaspor na kumpasia mfungaji ambaye hakufanya makosa na kuukwamisha mpira wavuni.
Dakika ya 58 kocha Mkwasa alifanya mabadiliko, ambapo waliingia Hamis Kizza na Nizar Khalfani kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu na kiungo Hassan Dilunga.
Hamis Kizza aliipatia Young Africans bao tatu la mchezo na la ushindi dakika ya 61 ya mchezo baada mpira aliogongewa na Domayo kuwapita walinzi wa Ankara Sekerspor na kumkuta Kizza ambaye alipiga shuti liliomgonga mlinzi wa Ankara Sekerspor wakati akiokoa na kujaa wavuni.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Ankara Sekerspor 0 -3 Young Africans.

Mara baada ya mchezo kaimu kocha mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa alisema anashukuru vijana wake walicheza vizuri kwa kufuata malekezo na ndio maana wakaweza kupata ushindi huo,makosa yapo machache yaliyojitokeza na ataendelea kuyafanyia kazi.

"Mechi ilikua ni nzuri ukizingatia ndo mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki tukiwa na siku ya tatu tangu tufike hapa Uturuki, kwa mazoezi ya jana vijana wameosha mabadiliko na leo wameweza kucheza vizuri na kuweza kupata ushindi, kikubwa naamini kwa siku zilizobakia nitaendelea kufanya marekebisho na kukifanya kikosi kuendelea kuwa bora pindi kitaporejea nchini tayari kwa mzunguko wa pili wa Lig Kuu ya Vodacom" alisema Mkwasa

Kikosi cha Young Africans kilichocheza leo ni:
1.Juma Kaseja/Ally Mustafa "Barthez" (dkk 65), 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua/David Luhende(dkk 82), 4.Mbuyu Twite (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Frank Domayo/Ibrahim Job(dkk 80), 7.Haruna Niyonzima/Saimon Msuva (dkk72), 8.Hassan Dilunga/Nizar Khalfan (dkk 58), 9.Didier Kavumbagu/Hamis Kizza (dkk 58), 10.Mrisho Ngasa/Jerson Tegete (dkk 68), 11. Emmanuel Okwi/Said Bahanuzi

Credits: Global publishers Tanzania
 
Ugandan strikers Emma Okwi and Hamis Deigo Kiiza starred as Dar giants Young Africans (Yanga FC) beat Ankara Sekerspor 3-0 in a friendly match played at the Manavgat in Turkey.

Didier Kavumbagu opened the scoreline for Yanga in the tenth minute, a goal that saw them break for half-time while in the lead.

On resumption, mid-season capture Okwi double the lead with a 46th minute strike. Kiiza put the tie to rest in the 61st minute.

Ankara Sekerspor is a sports club in located in Ankara, Turkey and features for the Turkish Football Federation (TFF) Second League.

Credits: redpper ug
 
ujinga mtupu hawa waliocheza nao ni wapishi wa hotel waliofikia kiukweli yanga wanasikitiaha kukubali kutumika kama punda kusafilisha madawa ya manji...
 
Habari za uhakika mechi yenyewe haikuwa na refa,walikuwa wanacheza kama mazoezi tena timu pinzani haikuwa na jezi ikapewa jezi za yanga zile za njano na yanga yanga wakavaa za kijani na ilichezwa kwenye kiwanja kidogo cha hotel waliyofikia,baada ya kuona refa amekosekana ikabidi mkwasa achezeshe mwenyewe
 
Chezeni na galatasalay,fernebahce n.k sio wafanyakaz wa hotel
 
Habari za uhakika mechi yenyewe haikuwa na refa,walikuwa wanacheza kama mazoezi tena timu pinzani haikuwa na jezi ikapewa jezi za yanga zile za njano na yanga yanga wakavaa za kijani na ilichezwa kwenye kiwanja kidogo cha hotel waliyofikia,baada ya kuona refa amekosekana ikabidi mkwasa achezeshe mwenyewe
Nimegundua ni kwa nini ulikwazana na Nyenyere kwenye therad iliyohusu Yanga na Simba katika maandalizi...Maneno yako yamejaa unazi usio na mfano mkuu wangu....Sioni ajabu ulikwazana na Nyenyere .

Hivi (kwa mfano) ikitokea ni kweli Yanga walicheza mechi hiyo ya mazoezi na Mkwasa akawa refa kuna tatizo?....Hasa ikizingatiwa mechi yenyewe ilikuwa ni ya mazoezi......

Kwani Yanga ni timu ya kwanza ya kiafrica kwenda Ulaya kufanya mazoezi?.....Mbona Coastal Union wamekwenda Oman hamsemi?....Mbona Azam huwa wanakwenda RSA hamsemi?.....Kwa nini iwe kwa Yanga tu?......Wivu wa kijinga...

Mi nadhani suala la Yanga wamecheza na nani na wanajifunza vipi huko Antalya waachiwe Yanga wenyewe...Kama suala la gharama waachiwe Yanga wenyewe....Yanga wao wameona kufanya mazoezi Uturuki kunalipa zaidi kulikokufanya sehemu nyingine na wameona kwamba mwaka jana walifanya mazoezi Uturuki walivyorudi wakabeba ndoo ya VPL....

Btw achana na spinning za kizamani na ushabiki wa kizamani mkuu wangu........

Angalia clip hii hapa chini uangalie jinsi 'Mkwasa' anavyochezesha hiyo mechi na uwaone Ankara Skerspor walivyovaa 'jezi za Yanga'....

Last edited by a moderator:
ujinga mtupu hawa waliocheza nao ni wapishi wa hotel waliofikia kiukweli yanga wanasikitiaha kukubali kutumika kama punda kusafilisha madawa ya manji...

..................Ningekudungua!!!!
 
ujinga mtupu hawa waliocheza nao ni wapishi wa hotel waliofikia kiukweli yanga wanasikitiaha kukubali kutumika kama punda kusafilisha madawa ya manji...
Haya ni maneno ya Mkosaji Chifu.....

Hivi Coastal Unioni walivyoenda Oman wamepeleka Drugs?....

Na Azam wakienda RSA kwa trials huwa wanapeleka Drugs?.....

Kupanga ni kuchagua mkuu wangu......Yanga mwaka jana wameenda Turkey wamerudi wamebeba ndoo ya VPL....Wameona kule ni kuzuri zaidi kujiandaa kiufundi kilinganishwa na sehemu nyingine.....

Ulitaka Yanga ikafanye trials za kujiandaa na VPL na CAF CL kwa kucheza na KMKM ama Clove, Spice stars ama Simba, Mbeya City, Azam ambao tayari hucheza nazo wakiwa nchini.....

Acheni spinning na ushabiki wa kizamani usio na tija......Ndio maana Yanga baada ya kulalamikiwa na waandaaji wa Kombe la Mapinduzi kwa kujitoa walienda Unguja wakaonana na Mhe. Balozi Seif Iddi na kuomba radhi kwa yaliyotokea kisha wakatoa Tshs. milioni 10 kama mchango wao kwa Kamati ya Kombe la Mapinduzi mambo yakaisha....

Kiukweli mimi ni mmojawapo ya watu wa awali kabisa kuiunga Yanga mkono kujitoa katika Kombe la Mapinduzi maana zaidi ya kuyaenzi Mapinduzi matukufu mashindano hayo hayakuwa na msaada wowote kwa timu (kiufundi)......
 
ujinga mtupu hawa waliocheza nao ni wapishi wa hotel waliofikia kiukweli yanga wanasikitiaha kukubali kutumika kama punda kusafilisha madawa ya manji...

Tangu mmeshinda ile mechi ya kirafiki (mtani jembe) naona mna huu sana. Ligi mzunguko wa pili ukianza msikimbie humu.
 
Haya ni maneno ya Mkosaji Chifu.....

Hivi Coastal Unioni walivyoenda Oman wamepeleka Drugs?....

Na Azam wakienda RSA kwa trials huwa wanapeleka Drugs?.....

Kupanga ni kuchagua mkuu wangu......Yanga mwaka jana wameenda Turkey wamerudi wamebeba ndoo ya VPL....Wameona kule ni kuzuri zaidi kujiandaa kiufundi kilinganishwa na sehemu nyingine.....

Ulitaka Yanga ikafanye trials za kujiandaa na VPL na CAF CL kwa kucheza na KMKM ama Clove, Spice stars ama Simba, Mbeya City, Azam ambao tayari hucheza nazo wakiwa nchini.....

Acheni spinning na ushabiki wa kizamani usio na tija......Ndio maana Yanga baada ya kulalamikiwa na waandaaji wa Kombe la Mapinduzi kwa kujitoa walienda Unguja wakaonana na Mhe. Balozi Seif Iddi na kuomba radhi kwa yaliyotokea kisha wakatoa Tshs. milioni 10 kama mchango wao kwa Kamati ya Kombe la Mapinduzi mambo yakaisha....

Kiukweli mimi ni mmojawapo ya watu wa awali kabisa kuiunga Yanga mkono kujitoa katika Kombe la Mapinduzi maana zaidi ya kuyaenzi Mapinduzi matukufu mashindano hayo hayakuwa na msaada wowote kwa timu (kiufundi)......

Mkuu Balantanda, mwenyekiti wa Simba Rage amewaambukiza mashabiki wake ugonjwa mbaya sana! Wamekuwa too local and trivial...
 
.....ngoja warudi Kichapo kinawasubiri, hiyo Ankara Sekerpor ndo nini bwana!! Yanga wana-weweseka tu.
 
.....ngoja warudi Kichapo kinawasubiri, hiyo Ankara Sekerpor ndo nini bwana!! Yanga wana-weweseka tu.
Yaleyale.......

Ragephobia na Dalaliphobia.....

Kuapa kumpa 'kichapo' Yanga bila kuwa na maono ya mbeleni.....

Akili ya uongozi wa Timu na mashabiki inakuwa kwenye 'kumchapa' Yanga badala ya kufikiria kuchukua Ubingwa......

No wonder Simba iko nafasi ya 4 na Yanga iko kileleni.....
 
Wangecheza na Galatasaray maana zikutane timu zinazocheza ligi kuu kwao. Mnacheza na timu ya ndondo halafu mnasumbua humu.
 
ujinga mtupu hawa waliocheza nao ni wapishi wa hotel waliofikia kiukweli yanga wanasikitiaha kukubali kutumika kama punda kusafilisha madawa ya manji...

Toa ushahidi wako na sio kuandika uk
.................ku........
 
Yaleyale.......

Ragephobia na Dalaliphobia.....

Kuapa kumpa 'kichapo' Yanga bila kuwa na maono ya mbeleni.....

Akili ya uongozi wa Timu na mashabiki inakuwa kwenye 'kumchapa' Yanga badala ya kufikiria kuchukua Ubingwa......

No wonder Simba iko nafasi ya 4 na Yanga iko kileleni.....

hahaha!iko wapi?kileleni!teh teh teh unafikiri zile bao 3 za dume simba mnyama mchezo!lazma afikishwe huko mawenzi
 
hahaha!iko wapi?kileleni!teh teh teh unafikiri zile bao 3 za dume simba mnyama mchezo!lazma afikishwe huko mawenzi
Tatizo wewe unaongea utoto.......Mimi naongea facts.....

Narudia tena, Akili ya uongozi wa Timu na mashabiki (ukiwemo wewe) inakuwa kwenye 'kumchapa' Yanga badala ya kufikiria kuchukua Ubingwa......

No wonder Simba iko nafasi ya 4 na Yanga iko kileleni.....
 
Back
Top Bottom