Yanga waweka kambi Asec Mimosas na sasa ni Sankara Karamoko

Soloma TV Online

Senior Member
Jun 26, 2023
104
291
Timu ya soka ya Yanga ukiikaribisha Klabuni kwako hawana haraka ya kuondoka, wao ni wakarimu sana utakumbuka waliwahi kupiga hodi AS VITA ya Congo na baada ya kukaribishwa waliacha simulizi yao ambayo inadumu mpaka leo.

Na sasa ni pale Asec Mimosas walianza na Yao na sasa mkono umehamia kwa mchezaji huyu raia wa Ivory Coast anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji akiwa kijana wa miaka 20 tu na kama mambo yatakwenda vizuri Sankara atakuwa MWANANCHI.
 
waliona timu imefanikiwa wanafikiri walichukua wachezaji wao na wao watapata hayo mafanikio, hata Simba walipowafunga Tano wakaanza kusajili wachezaji wao.
 
Kila la heri kwa Wananchi. Bila shaka atakuwa ndiye mchezaji atakayekuja kuvaa jezi namba 6!
 
Wakati wanachukuwa wachezaji kutoa As Vita mlisema hivi hivi....kilichotokea nadhani mnaomba Mayele aondoke.....
Tena kipindi hicho walikuwa wanakejeli kuwa Yanga inataka kuanzisha bendi ya wacongoman.

Halafu mwisho wa siku makombe yote yakachukuliwa kwa misimu miwili mfululizo.
 
Back
Top Bottom