Ni afadhali mara mia Yanga ipangwe na Mamelodi Sundowns kuliko ASEC Mimosas

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,649
9,239
ASEC inawajua vizuri sana wachezaji wa Yanga maana imewalea na kuwakuza kisoka kisha wakakulia hapo na mazoezini wamekabana sana na kocha Julio anawajua vizuri mno.

Aziz Ki, Pacome, Yao Yao bila kumsahau Guede, hawa wote ni zao la kocha Julio hapo ASEC pia hao vijana wake sidhani kama wanaweza kumsaliti au kumuumiza mwalimu wao wa zamani aliyewatoa kimaisha.

Yanga akipangwa na Mamelod ni salama zaidi sababu baada ya Motsepe kuinunua Mamelodi, Kocha wa kwanza alikuwa Gamond na ndiye muasisi wa soka safi mnalo liona hapo kwa Wabrazil wa South maarufu kama "Shoe shine and amapiano", yaani kubrashi viatu kwa mpira huku ukiumiliki na kuuchezea utakavyo.

Msije kusema sikuwaambia.
 
ni mbovu kwa sababu umeanza kuiangalia juzi ilivyocheza na simba hujui kuwa imeondokewa na striker wake SANKARA KARAMOKO ambaye licha ya kutokuwepo ila anaongoza kwa magori mpaka sasa
Kwahiyo kati ya wydad alieshindwa kufuzu na asec mimosa ni ipi timu yenye wachezaji mmoja mmoja wenye quality?
 
Hakuna timu yoyote ile kwenye port 1 ambaye Yanga anaiweza wanatafta Namna ya kujifariji Tu Mim naomba Mungu wapewe Wale jamaa wa Angola
Siku ya kwanza kupangwa makundi kwenye kundi la D kuna aliekajua kama Yanga ataingia robo halafu belouzdad asifuzu? Je kwenye kundi la simba kuna aliekajua kuwa wydad hatoingia robo fainal? Tuongee kisoka tuachane na mihemko ya balehe
 
ASEC inawajua vizuri sana wachezaji wa Yanga maana imewalea na kuwakuza kisoka kisha wakakulia hapo na mazoezini wamekabana sana na kocha Julio anawajua vizuri mno.

Aziz Ki, Pacome, Yao Yao bila kumsahau Guede, hawa wote ni zao la kocha Julio hapo ASEC pia hao vijana wake sidhani kama wanaweza kumsaliti au kumuumiza mwalimu wao wa zamani aliyewatoa kimaisha.

Yanga akipangwa na Mamelod ni salama zaidi sababu baada ya Motsepe kuinunua Mamelodi, Kocha wa kwanza alikuwa Gamond na ndiye muasisi wa soka safi mnalo liona hapo kwa Wabrazil wa South maarufu kama "Shoe shine and amapiano", yaani kubrashi viatu kwa mpira huku ukiumiliki na kuuchezea utakavyo.

Msije kusema sikuwaambia.
Tunamtaka huyo huyo.
 
Historia ni story za zaman a.k.a zilipendwa
Yanga ameshawah fuzu robo fainal ya CAF
Sipo kwa ajili ya kuweka mambo ya historia bali nazungumzia mpira wa leo hii ninapoona simba wanajifanya wenyeji mno wakati kwa uwekezaji uliopo Yanga na mafanikio aliyokawa nayo mwaka jana robo ni kitu cha kawaida tu
 
Back
Top Bottom