Yanga vs Al Ahly ni vita ya Waholanzi

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Yanga ahly.jpg

SAHAU rekodi za nyuma za Yanga dhidi ya timu za Misri, hususan National Al Ahly.

Hii ni soka, na lolote linaweza kutokea Jumamosi Aprili 9, 2016 wakati Yanga itakapoikaribisha Al Ahly kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Miaka 34 iliyopita wakati Yanga ilipopambana na Al Ahly kwa mara ya kwanza, vikosi vyao havikuwa na wachezaji waliopo sasa wala mabenchi ya ufundi hayakuongozwa na makocha waliopo.

Kilichopo zaidi hapa ni kwamba, hii itakuwa vita baina ya Waholanzi ...

Kwa habari zaidi, soma hapa => Yanga vs Al Ahly ni vita ya Waholanzi | Fikra Pevu
 
Naipenda Yanga lakini kitendo chao cha kutoonyesha game live ili washabiki wao wafurahie ni ujinga na ndio unaonifanya nisiiombee yanga kufika mbali katika mashindano ya kimataifa.
Viongozi wapo busy kupiga pesa tu!!
 
Acha Kukweza mambo hakuna Vita hapo Wamisri wanapita kirahisi hapo.
 
Acha Kukweza mambo hakuna Vita hapo Wamisri wanapita kirahisi hapo.
Juzi nilimsikia jerry muro anasema kuwa eti dawa yao ni kuwachezesha saa saba ya mchana!!na kwenye uwanja wenye vichuguu sana!!!kweli mpira wa tz bado unasafari ndefu sana huu upuuzi nao ni wa kuongea mbele ya watu tena kwenye chombo cha habari?!!!
 
Hii mechi ni sawa sawa na Pacman apambanishwe na Thomas Mashali....
Abajalo fc akutane na FC BARCELONA....

Kiufupi matokeo yashapatikana kabla hata ya mchezo....
 
Juzi nilimsikia jerry muro anasema kuwa eti dawa yao ni kuwachezesha saa saba ya mchana!!na kwenye uwanja wenye vichuguu sana!!!kweli mpira wa tz bado unasafari ndefu sana huu upuuzi nao ni wa kuongea mbele ya watu tena kwenye chombo cha habari?!!!

Huyo jerry muro zinamtosha kweli?
 
Hapa UZALENDO tupa kule, Ndala lazima wanywe maji yao pale ktk dimbwi lao, lazima wainame.
J'Mosi mapemaaaaa ndani ya uzi wangu nyekundu na nyeupe kuelekea taifa.
 
Yanga hana pakwenda hapo.Timu mbovu kiasi hicho! Matokeo tayari hapo yanga katolewa tayari.
 
Back
Top Bottom