Yanga SC 0-0 Club Africane | CAF Confederation Cup | Mkapa Stadium

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
FULL TIME

90' Zinaongezwa dakika 5 za nyongeza
88' Shambulizi kali langoni mwa Yanga lakini kipa Diarra anafanya kazi nzuri ya kuzuia
82' Morrison ametoka, ameingia Farid Musa
80' Wachezaji wawili wa Club African wapo chini, mchezo umesimama kwa muda
72' Yanga wanatengeneza mashambulizi lakini bado ngome ya Club African ni ngumu
53' Yanga wanapata kona lakini haizai matunda
50' Anatoka Kisinda anaingia Moloko upande wa Yanga
48' Kipa wa Club Africane anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda
Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO

45' Shambulizi kali langoni mwa Club Africane lakini walinzi wanaokoa
42' Presha ya mchezo inaongezeka
39' Benchi la Club Africane wanainuka na kulaumu kwa mwamuzi, mchezo unasimama kwa muda wakitaka penati
34’ Mchezo unaendelea timu zikipeana zamu kumiliki mpira
25’ Yanga ni kama wameshtukia mtego wa wapinzani wao, sasa wanaongeza kasi
20’ Mayele anapiga kichwa mpira unadakwa
15’ Yanga wameanza kuchanganya kasi, wamepata kona mbili ndani ya muda mfupi
10’ Yanga ni kama wanalazimishwa kucheza mchezo wa taratibu
5’ Mchezo umeanza kwa kasi ndogo

Mchezo umeanza

Timu zimeshaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo, wachezaji na benchi la ufundi la timu zote wanasalimiana

Yang.JPG
Timu zimeshaingia uwanjani kwa ajili ya kupasha miili joto, idadi ya watu siyo kubwa lakini wanaendelea kuingia uwanjani.

============
Leo saa 10:00 Jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki Yanga Sc watashuka dimbani kumenyana na Club Africaine ya Tunisia

Ikumbukwe kuwa Yanga Sc ndio wawakilishi pekee Kutoka Tanzania Kwenye kinyang'anyiro hiki Cha Caf Confederation Cup.

Hivyo wanawakilishi nchi yetu

Tutaleta live updates hapa kuanzia saa 9:00 jioni na mchezo utakuwa live kupitia Azam Tv chaneli ya Azam Sports One HD.
 
Huu ni utani tu kama ule alioufanya Hersi kuvaa jezi ya Kaizer Chief
Inaelekea wewe ni mshabiki wa juzijuzi tu, Yanga imecheza na Mazembe, Manji akatoa ofa mashabiki waingie bure, Simba wameingia na jezi za Mazembe na wanazo mpaka leo....eti useme ni mashabiki wao
 
Wapigwe kama ngoma hawana adabu ,wana viherehere kupokea wageni misimu minne iliyopita, yaani walikuwa wanahamasishana kuwa al hilal ni timu ndogo?

Hizi dharau Simba hakuwa nazo kabisa, aliheshimu timu zote japo walikuwa wapigwa hamsa ,hamsa ndio zimewajenga kufikia hapo. Hawataki kujifunza wanaingia uwanjani kwa slogan na hamasa, mpira unachezwa uwanjani.

Sina heri nao lolote liwakute.... wakishainda nitashangilia ,wakifungwa nitafurahi sana
 
Inaelekea wewe ni mshabiki wa juzijuzi tu, Yanga imecheza na Mazembe, Manji akatoa ofa mashabiki waingie bure, Simba wameingia na jezi za Mazembe na wanazo mpaka leo....eti useme ni mashabiki wao
Tofautisha uzito wa jambo hilo kufanywa na mashabiki na kiongozi wa ngazi za juu ya Club

Hersi alikuwa kiongozi hakutakiwa kufanya kitu kama hicho angeweza kukausha tu hata kinafki.

Mkaenda mbali zaidi kuweka madai ya uongo kuwa kuna madawa tume spray kwenye vyumba vya wapinzani. That is absurd
 
Hivi unaelewa huyu aliwa cost Yanga kutoa $5,000 ili atumie kwenye haya mashindano ya kimataifa?
Hayupo sawa nadhani ndio maana aliachwa huko Berkane sioni akicheza mpira huo unaotazamiwa kutoka kwake ni bora hata hao local wakina Ambundo na Nkane yaani huyo anabadilishwa na Kambole Mzambia nadhani tuna tatizo sehemu ila sio wa kumtoa Kambole awekwe Kisinda..
 
Back
Top Bottom