Yanga na Simba vitani in 24hrs | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga na Simba vitani in 24hrs

Discussion in 'Sports' started by MaxShimba, Jan 27, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  BAADA ya kufanya vizuri katika michezo yake ya katikati mwa wiki, Simba na Yanga keshokutwa na Jumatano zitarudi tena kucheza na Prisons na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu.

  TIMU hizo zitacheza michezo hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara zikiwa na mawazo tofauti.

  Yanga ndio itakuwa ya kwanza kucheza na Mtibwa Sugar keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ukiwa ni mchezo unaosubiriwa kwa hamu zaidi kutokana na historia ya timu zote mbili.

  Ukali wa mchezo huo unatokana na michezo miwili ya mwisho iliyozikutanisha timu hizo, katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi mwaka jana, Yanga iliifunga Mtibwa bao 1-0 katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

  Mtibwa iliweza kulipa kisasi kwa kuifunga Yanga idadi hiyo hiyo katika mchezo wa mwisho wa kundi A wa michuano ya kombe la Tusker uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Wakati Yanga ikiingia uwanjani na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons ya Mbeya, Mtibwa ina kumbukumbu nzuri pia ya kuifunga timu Kagera Sugar mabao 2-1.

  Katika mchezo mwingine wa Ligi hiyo utakaochezwa Jumatano, Dar es Salaam, Simba itakuwa na kibarua kigumu cha kulipa kisasi kwa Prisons itakayocheza nayo katika uwanja wa Taifa.

  Awali katika mchezo uliochezwa katika mzunguko wa kwanza wa Ligi hiyo, Simba ilifungwa bao 1-0 na timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza Tanzania, na kuanzisha balaa la kutofanya vizuri katika michezo mingine ya Ligi Kuu.

  Simba itaingia uwanjani ikiwa na hamasa kubwa, baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Villa Squad ya jijini katika mchezo wa mwisho tofauti na Prisons iliyofungwa bao 1-0 na Yanga.

  Michezo yote miwili ya kesho na keshokutwa inatazamiwa kuwa ya kulipa visasi kutokana na historia ya michezo ya mwisho iliyozikutanisha timu hizo.

  Yanga ndio inayoongoza Ligi hiyo kwa kuwa na pointi 36 ikifuatiwa na Kagera Sugar yenye pointi 23, ya tatu ni Mtibwa (21), Simba ya nne (20) na Prisons inashika nafasi ya tano kwa kuwa na pointi 19. Timu zote zimecheza michezo 13.

   
Loading...