Yanga na jezi nyeusi

Wewe ndio utuambie wamevunja sheria ipi na kifungu kipi jezi zipo kwa ajili ya kuleta utofauti.

Hata ulaya mf Arsenal akicheza na Chelsea darajani anavaa jezi nyekundu, akicheza na Leeds,Man City, Spurs, Fulham,Wolves,Leicester anavaa nyekundu ambayo anaivaa nyumbani.

Madrid ndio usiseme.
 
Mganga wenu atawaponza
Hii hivi!
20221202_190917.jpg
 
Mbona mnhamisha mpira?.hapa hoja ni jezi ya Yanga nyeusi
Mazindiko FC
😀 😀 😀 😀 😀 😀
 

Jezi nyeusi Yanga yazua jambo​

Alhamisi, Desemba 01, 2022

JEZI nyeusi ya Yanga imezua jambo baada ya Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) kuziandikia barua klabu zote za Ligi Kuu kuhakikisha zinafuata na kuheshimu machaguo ya jezi za nyumbani na ugenini kwa mujibu wa kanuni.

Yanga ndio imekuwa ikitumia jezi hiyo mara kwa mara kwenye michezo ya hivi karibuni nyumbani na ugenini, lakini yameibuka mapya sio Yanga tu ambao wamekuwa wakivaa chaguo la tatu la jezi na ndio maana TPLB imetuma barua kwa timu zote.

Mwanaspoti hivi karibuni liliripoti kuhusu jezi nyeusi za Yanga kuonekana zenye bahati ya kuipa matokeo mazuri kila inapozivaa huku ofisa habari wa klabu hiyo, Ally Kamwe akionekana kukubaliana na hilo na kiungo nyota wa Yanga Feisal Salum ‘Fei Toto’ alisema inawajengea ari ya upambanaji.

Akizungumza na Mwanaspoti, ofisa habari wa TPLB, Karim Boimanda alisema sio sahihi kisheria na kikanuni ndio maana wameamua kuziandikia barua timu zote zinazokiuka kanuni hiyo kwa kuzitaka kuhakikisha zinazingatia.

“Yanga inazungumzwa sana kwa sababu hadi wao kama timu wamekuwa wakiipigia kampeni jezi yao nyeusi kama ndio inawapa matokeo na ndio maana kila mmoja anaitaja hiyo timu, lakini sio kweli ni wao pekee wamekuwa wakitumia jezi ya ziada,” alisema na kuongeza:

“Ni timu nyingi zimekuwa zikikiuka taratibu na sheria kwa kuvaa jezi ambazo ni za ziada na sio machaguo yao ambayo ni rangi ya nyumbani na ugenini, jezi namba tatu ni maalum kwa ajili ya kutumika endapo timu zitakutana na zinakuwa na rangi ambazo zinafanana lakini hivi karibuni kuna baadhi ya timu wanatumia kama jezi ya kuvaa nyumbani na ugenini.”

Kanuni namba 17 kipengele (5) inasema timu zitaheshimu uchaguzi wa rangi za sare zao kwa michezo ya nyumbani na ugenini/ya ziada (katika mazingira ya mgongano wa rangi), endapo itatokea timu ya nyumbani kukosa uzingativu wa rangi sahihi kwa sare zake kwa mechi za nyumbani katika kikao kitangulizi cha MCM timu ngeni itakuwa na haki ya kwanza ya kuchagua rangi ya sare katika mchezo husika.

 
(14) Timu zitakaguliwa kwenye vyumba vyao vya kuvalia na endapo rangi za sare za timu zote zitafanana timu ambayo haikufika kwenye kikao cha maandalizi italazimika kubadili jezi.
(i) Kila kilabu itasajili TFF rangi ya jezi zake kwa mechi za nyumbani na ugenini kabla ya kuanza msimu wa Ligi. Kilabu itakayokiuka itatozwa faini ya Tshs. 300,000/=

NB: Hizi ni kanuni za msimu wa 2009, huenda adhabu imebadilika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom