Yanga kwa hili hapana mnatualibia vipaji

Yanga kwa hili hapana mnatualibia vipaji

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,393
hadi kufikia sasa klabu ya Yanga imefanikiwa kukamilisha kusajili idadi ya washambuliaji 8 ambao ni jerry tegete, kavumbagu,saidi bahanuzi, shabani kondo, lusajo, husein javu, hamisi kiiza(ameshamalizana na uongozi wa yanga leo) na mrisha ngassa(japo pia anaweza cheza kama kiungo wa pembeni) pia kuna mshambuliaji mnaigelia ogbu brenden anaendelea na majaribio ambae akifanikiwa atafanya washambuliaji kuwa 9, sasa hapa yanga itamudu vipi hawa wote kucheza? Nadhani kuna hatari ya baadhi ya vipaji kuozea benchi uku tukilalamika timu ya taifa haina washambuliaji wa kutosha kumbe wengine ni wazuri lakini hawapati nafasi nadhani ni bora timu ikasajili kulingana na mahitaji ya timu pia kwa manufaa ya taifa.'
 
Sasa wote hao wanini?Alafu ukute pesa iliyowasajili hao strikers wote ni mara mbili ya pesa ya ubingwa wa vodacom!
 
Sasa wote hao wanini?Alafu ukute pesa iliyowasajili hao strikers wote ni mara mbili ya pesa ya ubingwa wa vodacom!

mkuu huo ndo ukweli,nimeshindwa kuelewa gharama kubwa halafu hawata tumika
 
Huu usajili wa kukomoana unaua soka letu, sidhani kama mahitaji ya kocha yamezingatiwa, Javu nae anaenda tu kasahau ya Bahanuzi haya yetu macho.
 
Kwa kweli hili la javu kwenda yanga hata mm sijapendezwa nalo, ingawa ameenda timu ninayoipenda, ki mtazamo javu alikuwa anaweza kucheza vizuri zaidi kma angeendelea kucheza timu isiyo kuwa na lundo la mafoward wala presha, kma alipotoka mtibwa.
Pia dhana ya kuwa had uchezee yanga au simba ww ndio mchezaji, inawaponza wengi, hata kama kivutio ni maslai ila waangalie badae watakuwa wapi, isije kuwa msimu mmoja tu unaonekana hufai, wajifunze kwa wachezaji wengine kwa kilichowatokea baada ya kukimbilia timu hizo.
 
Sasa wote hao wanini?Alafu ukute pesa iliyowasajili hao strikers wote ni mara mbili ya pesa ya ubingwa wa vodacom!
Mkuu wanashangaa bure Wapare kuuza mbuzi ili ashinde kesi ya kuku kumbe na huku Jangwani wapo Wapare wa Kizaramo na Kihindi.
 
Hapo ndipo ninaamini yanayosemwa na wachambuzi wa soka kwamba Yanga ni sehemu ya kuulia vipaji. Walioshituka walikimbia mapema sasa hivi wanachukua zawadi y awachezaji bora wakiwa na timu zinazojua kukuza vipaji na wanazidi kuonekana na kung'ara kimataifa.

Acha wakaue soka lao huko wakiridhika na vihela mbuzi vya kuchukulia machangu SUNSIRO na Corner Bar.
 
hapo ndipo ninaamini yanayosemwa na wachambuzi wa soka kwamba yanga ni sehemu ya kuulia vipaji. Walioshituka walikimbia mapema sasa hivi wanachukua zawadi y awachezaji bora wakiwa na timu zinazojua kukuza vipaji na wanazidi kuonekana na kung'ara kimataifa.

Acha wakaue soka lao huko wakiridhika na vihela mbuzi vya kuchukulia machangu sunsiro na corner bar.

sputanza?
 
Mkuu ukumbuke mpira ndio ajira yao, anapaswa aangalie maslahi ya leo kwanza kabla ajafikilia mambo ya kukaa bench au kuua kipaji, kwa mfano ukiambiwa Mtibwa walitaka kumsajiri kwa 5m lakini Yanga wamempa 30m bado utamlaumu? kama angezikataa na kubaki Mtibwa kisha msimu ujao aumie goti na kipaji kiishie hapo itakuwaje? uoga wetu ndio umaskini wetu tunaogopa ajira binafsi zenye mshahara mkubwa kwa kulinda ajira za serikali zenye mshahara kiduchu kwa kusubiri kiinua mgongo ambacho hatuna uhakika kama tutakifikia.
Kwa kweli hili la javu kwenda yanga hata mm sijapendezwa nalo, ingawa ameenda timu ninayoipenda, ki mtazamo javu alikuwa anaweza kucheza vizuri zaidi kma angeendelea kucheza timu isiyo kuwa na lundo la mafoward wala presha, kma alipotoka mtibwa.
Pia dhana ya kuwa had uchezee yanga au simba ww ndio mchezaji, inawaponza wengi, hata kama kivutio ni maslai ila waangalie badae watakuwa wapi, isije kuwa msimu mmoja tu unaonekana hufai, wajifunze kwa wachezaji wengine kwa kilichowatokea baada ya kukimbilia timu hizo.
 
Soka ni ajira jamani kama mtibwa hawajatoa mpunga wa kutosha mlitaka ang'ang'anie? Tusubiri tuone nini hatma yake hapo jangwani.
 
Back
Top Bottom